Yametimia: Wenye nyumba sasa kulipa kodi

Yametimia: Wenye nyumba sasa kulipa kodi

Kweli imedhamiriwa tuwe mashetani,khaa!kila sehemu kukamuliwa jamani.
 
Serikali ya ze mbululaz, yaani haifikirii vyanzo vipya kwenye Madini, Utalii, na natural resources zingine wao wanawaza kumlundikia kodi mwananchi tu

Jamani hili si la kushangilia tu kwa sababu sisi si wenye nyumba lakini tujiulize nani ataumia ktk haya? In short hapo ni wote

Mtu huyo huyo ulipe KODI YA KIWANJA, KODI YA JENGO (Property Tax), na bado awekewe KODI YA NYUMBA kwenye KODI YA NYUMBA, let's rethink on this
 
Katika uzi huu, inafaa kabla hujachangia unadeclare interest kwanza kama wewe ni mpangaji ama mwenye nyumba. Mleta uzi bila shaka ni mpangaji kwa kadri alivyoandika maana kwa malipo ya Ufipa mpaka ujenge nyumba itachukua miaka 50

Duuu! Kwa hiyo lumumba kwa ujinga mnaoandika humu mnalipwa? Lakini hata kama mnalipwa muwe na adabu basi maana mnatukana mpaka baba zenu humu ndani kisa hivyo vi posho vya lumumba!
 
kwa maoni yangu kodi iwekwe, lakini iundwe bodi itakayo regulate bei za pango kulingana na hadhi ya nyumba .kama sumatra wanavyo regulate bei za mabasi na wameziwekea amadaraja
 
Naunga mkono hoja ya serikali kupeleka mswada bungeni utakao wataka wenye nyumba kulipa kodi kwa serikali.

Niukweli usiopingika kwamba kwa sasa biashara ya upangishaji nyumba ni soko huria.

Utakuta mwenye nyumba anapangisha nyumba isiyo na hadi kwa bei kubwa sana tena wengine kwa fedha za kigeni.

Jambo hili ni jema sana, japo wengine wataona kama serikali inataka kuwa umiza wananchi wake.

Lakini jambo hili litaleta nafuu sana kwa wapangaji kama serikali itatunga sharia kali juu ya wamiliki wa nyumba na kumlazimisha mwenye nyumba kwenda na bei Elekezi itakayopangwa na sarikali kutokana na ubora wa nyumba husika.

Siyo unapangisha nyumba ya room 2 mwenye nyumba anakulipisha laki 5 kwa mwezi, hapa serikali itilie mkazo na iweke sheria kali kumlinda mlaji ambaye ni mpangaji, ili mpangaji alipe kutokana na ubora wa nyumba na siyo ulafi wa mwenye nyumba.

Naipongeza sana serikali kwa kuliona jambo hili, na kuiomba itunge sheria kali kwa wenye nyumba watakao kaidi kufanya jambo hili na kupelekea kuwaumiza walaji.
 
Wenye nyumba wapi? Hujaeleweka, yaan nimejenga nyumba Yangu naishi mwenyewe halafu nalipa kodi ? Kama kodi ya kiwanja /property tax mbna IPO miaka mingi
Property tax inatakiwa kuwa proportional na thamani ya nyumba siyo kulipia kiwanja tu. I unaona wamiliki wa agari wanalipia miliki za magari pia?
 
Sijui serikali huwa inapitia maoni yetu humu JF au vipi ila habari kuu katika gazeti la Mtanzania inasomeka: "Muswaada wa fedha,wenye nyumba sasa kuisoma namba" .

Mtangazaji wa Channel 10 alikuwa anasoma magazeti amesoma kidokezo cha habari kuwa wenye nyumba sasa watatakiwa kutozwa kodi kutoka kwenye zile kodi wapangaji wanazolipa.

Chanzo:Mtanzania

Hata hivyo,kama wengine tulivyowahi kushauri hapa mtandaoni wakati tunapendekeza kodi hii ianzishwe,tulipendekeza pia serikali iweke kodi elekezi ambapo wenye nyumba watapaswa kuifuta maana bila hivyo,wapangaji ndio wataisoma namba.
Kodi wakusanye maana nayo ni mapato. Lakini hoja ya kupanga bei sikubaliani nazo kabisa! Hii ni kasumba ya ujamaa.! Hapo naomba nitofautiane na wewe mkuu. Mimi ni miongoni mwa watu tunaopinga ujamaa, na kasumba zake zote. Hata udikteta unaoendelea sasa hivi nchini ni kasumba ya ujamaa. Tazama demokrasia na haki za binadamu kwenye mataifa yote yaliyokuwa ya kijamaa!
 
Sasa unadhani shida itakuwa kwa mwenye nyumba ama mpangaji? Bei elekezi haijawahi kuzaa matunda nchini hivyo sihitaji kufikiri juu ya hilo!
Hivi bei elekezi ya shule imefikia wapi. Nyumba ina vionjo vingi (mahali ilipo, decoration, utilities etc) ngumu kupanga bei elekezi.
 
Serikali ya ze mbululaz, yaani haifikirii vyanzo vipya kwenye Madini, Utalii, na natural resources zingine wao wanawaza kumlundikia kodi mwananchi tu

Jamani hili si la kushangilia tu kwa sababu sisi si wenye nyumba lakini tujiulize nani ataumia ktk haya? In short hapo ni wote

Mtu huyo huyo ulipe KODI YA KIWANJA, KODI YA JENGO (Property Tax), na bado awekewe KODI YA NYUMBA kwenye KODI YA NYUMBA, let's rethink on this
Makampuni ya madini yote yatalipa kodi kuanzia mwaka huu wa fedha. hata hivyo ni kampuni moja tu ya ACACIA ndio haikuwa ikilipa CIT (Corporate Income Tax) ambayo ni 30% ya faida. Mwezi March ilipokea amri ya Serikali kufanya hivyo kuanzia fiscal year hii. President wa ACACIA aliyekuja kwa wito wa Prof. Muhongo alipokea na kutii amri husika. Sasa Tanzania inarejea kwenye uchumi wa ushindani wa soko (market forces) hasa. Viwango vya kodi za pango vitakuwa vikishuka na kupanda wakati kutakuwa na nyumba zitakazokosa wateja kusubiri rent equilibrium. Enzi zetu hapo pangekuwa patamu kwa form six economics 'research' papers. Maana graph zingeonekana kabisa zikipanda na kushuka kulingana na tukio fulani ambalo ingeonekana kuathiri real estate business/speculations. Ahsante JPM kwa kuua ndege 2 kwa jiwe 1.
 
Kwamba serikali ilikuwa haikusanyi kodi kwenye nyumba ni habari kichaa. Nyumba ni chanzo cha kodi cha halali kwa serikali karibu dunia nzima.

Serikali ikianza kukusanya kodi ijue kwamba hizo kodi zinatakiwa kutumika kutoa huduma. Siyo kwenda kufanya kampeni za CCM.

Haiyumkiniki watu watoe kodi za nyumba halafu kusiwe hata na huduma za kukusanya takataka au zimamoto.

Hiyo kodi elekezi haitakiwi katika mfumo wa soko huria. Serikali haitakiwi kupanga bei. Inatakiwa kupanga mazingira yatakayoleta mashindano ya bei kiasi kwamba bei itakayopatikama iwe nzuri.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom