wakimataifa
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 942
- 169
Makada wawili wakongwe wa CCM Mgana Msindai na John Guninita wamemfungulia kesi ya madai DC wa Kinondoni Paul Makonda wakimdai milioni 200 kwa maneno ya kashfa na kushushiwa heshima aliyoyatoa Paul Makonda alipokutana na waandishi wa habari.
Kesi hiyo nambari 68 ya 2015 iko Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Wadai wanaiomba mahakama kumuamuru Paul Makonda awalipe milioni 100 kila mmoja. Pia wanaiomba mahakama imuamuru Paul Makonda kutotoa tena maneno ya aina hiyo dhidi yao.
Chanzo: Magazeti ya leo ya Tanzania
wanahaki ya kumshtaki makonda kwa sababu makonda aliwaambia UKWELI na wao wamezoea kusema UWONGO wa kumdanganya lowasa kuwa mgombea uraisi na wapate chochote kwa lowasa.
POLENI AKINA NCHIMBI NA MSINDAI ZAMA ZA UDIKTETA KWENYE SIASA ULISHAZIKWA