Yametimia: CCM kuimaliza CHADEMA muda mfupi ujao

Yametimia: CCM kuimaliza CHADEMA muda mfupi ujao

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
26,476
Reaction score
40,100
Kuimaliza ama Kuiliza all the same.

Kupitia mitandao hasa JF, kulitolewa maonyo na mikakati kadhaa ya maazimio ya CCM juu ya mikakati mahsusi ya kuidhibiti CHADEMA kupitia mitandaoni. Sehemu ya mkakati huo ilikuwa ni kuwaandaa vijana kuweza kushambulia Upinzani hasa viongozi wa juu ili wasiweze kupenya nyoyo za Watanzania kwa 2015.

CHADEMA ndiye lengo kuu. Na sote tumeshuhudia kuibuka kwa vijana ndani na nje ya CHADEMA ambao wamekuwa wakivuruga malengo ya chama na kuwatukana viongozi wa juu. Kinachonivunja moyo ni kwamba CHADEMA wanalifahamu hili na hawakujipanga namna ya kulikabili na sasa wanaelekea kuwa ktk hali mbaya kisiasa. Kuibuka kwa Masalia na kundi la vijana wa facebook wanaoshambulia moja kwa moja viongozi wa juu wa CHADEMA ni sehemu ya UTEKELEZAJI huo.

CHADEMA waliitumia vizuri sana mitandao ya kijamii kujijenga na hasa hapa JF waliweza kushawishi umma kuwakubali na kuweza kupeleka malengo yao kwa wananchi. Lakini kukaa kwao iddle bila kuzikabili hizi mbinu za CCM ktk kuwamaliza ni wazi upinzani unaelekea kwenye pigo jingine.

Kutojiandaa kuna dalili nyingi sana kwa mfano unapoona watu wanajibu kwa kutukana badala ya kujibu hoja ni mojawapo ya dalili. Nasikitika kusema kwamba CHADEMA kimejikita kwenye majibishano zaidi ya vitendo yaani ile kazi ya M4C inaelekea kumezwa na issue ya masalia na msuguano wa uongozi kwenye taasisi za chama.

Ushauri wangu ni kwamba CHADEMA ikae chini ipange mkakati wake wa kukabiliana na changamoto zinazojitokeza kila siku na hata kuchukua hatua kijamii kwa wale wanaopotosha taarifa za Chama ili UMMA utambue na kujenga imani zaidi. Majibu wanayotoa kwa umma yawe yanajitosheleza kwa sababu kuna hoja zingine ni propaganda na lengo lake ni kuwaingiza viongozi wakuu mtegoni na kusababisha kuhamisha mijadala ya kitaifa hadi kuanza kuzungumzia issues za kitoto. Kwa mfano hoja ya kadi ya Slaa, pamoja na issue ya Ruzuku inayojitokeza sasa.

CHADEMA msipojipanga, hesabuni mmeumia na tutakuwa na historia ya kuwa na chama makini kilichoshindwa kufikia lengo.

#JustSaying
 
Hooray CHADEMA yawakosesha usingizi ,embu tupe uthibitisho kama hawa wanaoposti hapa hawana ID zaidi ya mia ,wanaandika na kujijibu wenyewe CHADEMA hata ukirudi tumboni mwa mama ako ili uzaliwe upya haitakufa kwa sababu ni nguvu ya umma
 
Ulichokandika ni kama tu jina lako, eti CCM wanatumia JF hata kama hukwenda shule vyakutocha fanya hata uchunguzi mdogo kuona wanaochangia humu jf wana itikadi gana utagundua wengi wanataka mabadiko sasa unahisi mabadiko hayo yataletwa na CCM?, hebu wakati unafikiri usikae maana labda sehemu unayokalia ndio unatumia kufiri
 
Maslia hawawezi kuitisha CHADEMA,

Masalia wanatapatapa tu kama kuku aliyekatwa kichwa.

Huu ni mwaka wa nguvu ya uma na M4C ya mwaka huu itakuwa babkubwa kuliko zote zilizotangulia.

stay tuned
 
I hate stupid things done by CCM. Always they are after Chadema! They ought to be after Tanzanians' wel-fare...economic development is waht we need! pity of them! what are they going to tell us in 2015...what did they do for us! what are they going to do for our next generation...always 'pride' of CCM is 'porvety' in this land of plenty! we were not supposed to be such poor people! they are cheaters...they cheated a large number of Tanzanians who depend on agriculture with 'wild dudu' known as KILIMO KWANZA, only in exchange of their votes in 2010 election!
:flock: :flock: :flock:
 
Msanii; Hebu ondoa usanii wako humu kama ulivyo!

Kama wamekutuma kawaambie ya kwamba watu wako macho zaidi ya mjuavyo,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,hakuna mtu wa kudanganyika tena
 
Last edited by a moderator:
I hate stupid things done by CCM. Always they are after Chadema! They ought to be after Tanzanians' wel-fare...economic development is waht we need! pity of them! what are they going to tell us in 2015...what did they do for us! what are they going to do for our next generation...always 'pride' of CCM is 'porvety' in this land of plenty! we were not supposed to such poor people!

Hapo kwenye red,
Angalia nukuu hii toka kwa William Malecela......!


"@ LE MUTUZ STRAIGHT TALK!!:
Leo kuna habari njema sana kwetu CCM, kwamba Mwenyekiti wa Chadema ameamua kujitoa kugombea Urais 2015, so I told you OUR OPERATION CHAOS is working kwani our never ending online attacks zimemfanya ajipime, ok now one more to go, next on line ni Dr. Slaa, naye ni lazima ajitoe kugombea ili our best interest Zitto ndiye awe mgombea wao 2015!

- NILIWAAMBIENI HAWA HAWANA MGOMBEA URAIS 2015, SO SASA WALE WOTE TUNAOSHIRIKIANA KUWADHOOFISHA KWA KUTUMIA MITANDAO TUZIDISHE MASHAMBULIZI KAMA ILIVYO SASA, NINALO BOMU MOJA LA KIONGOZI WAO MMOJA MAARUFU KUTAKA KUMBAKA DEMU MMOJA MAJUU NA KESI IPO MAHAKAMANI NA DOCUMENTS ZIPO, INA MAANA HUYU AKIPEWA KUGOMBEA CHADEMA AKAPATA URAIS HATARUHUSIWA KWENDA HIYO NCHI, SASA TUTAKUWAJE NA RAIS AMBAYE NI LIMITED KWENYE INTERNATINIONAL COMMUNITY? SAAFI SANA MHESHIMIWA MBOWE KWA KUJIPIMA NA KUACHIA NGAZI SASA MSHAURI NA MWENZAKO SLAA AJIPIME!!

KIDUMU CCM!

KIDUMU CHAMA TAWALA!!

HA! HA! HA! HA!

- LE MUTUZ!!"

 
Ningemshauri huyo aliyefanya analysis na kuona kama vyama vinakufa ama kujiimarisha kwenye mitandao ya kijamii amekosea hiyo methodology. The BEST indicator ni umma, hivyo muitikio wa umma ndiyo unaweza kudhihirisha kuwa chama kinakufa ama kuimarika. Nenda kafanye assignment yako upya kwa ku-observe umma na kusikia maoni/upendeleo wao.
 
....hata ukirudi tumboni mwa mama ako ili uzaliwe upya haitakufa kwa sababu ni nguvu ya umma
Ulichokandika ni kama tu jina lako, ....hebu wakati unafikiri usikae maana labda sehemu unayokalia ndio unatumia kufiri
Msanii; Hebu ondoa usanii wako humu kama ulivyo!..
Msanii,
Nadhani hawa wachangiaji hawakusoma vema hoja yako; au wameona tu maandishi bila kukuelewa?! Mbona umewapa tahadhari lakini bado wamethibitisha ulichotahadharisha hapa!:
Kutojiandaa kuna dalili nyingi sana kwa mfano unapoona watu wanajibu kwa kutukana badala ya kujibu hoja ni mojawapo ya dalili....
 
kelele za mlango hazimnyimi mwenye nyumba usingizi, na kamwe haiwezekani kufuta fikra za binadamu kwa ujumla wake ila historia inaweza kufutika ghafla katika vichwa vya binadamu ikiwa utamuudhi au utambughudhi katika katika fikra zake au anachokiamini.
 
Mkuu, CHADEMA inaelekea wamejipanga sana. ukiona wana kila ushahidi juu ya kila usaliti unaoendelea au unaopangwa ujue huo ushahidi haukupatikana kwa bahati ila umepatikana kimkakati. Kwani unafikiri Ben saanane kusamehewa ilikua Ben ana bahati au ni mkakati wa chama na intelijensia yake? Huwezi kumjua adui yako vizuri usipokua naye karibu.

Mi nadhani tuzidi kuwatia moyo hawa ndugu walioko kwenye uongozi, wazidi kupambana na mikakati yao iende sawia. Binafsi sina wasiwasi na sisiemu kwa maana miili ya wana CCM wengi ipo sisiemu ila nafsi/upendo wao upo CHADEMA kwa sababu Watanzania wengi ni wapenda haki na angalao CHADEMA haki inaonekana ikitendeka.
 
Wasaliti wate huu ni mwaka wao, we nenda tu kachukue mlungula wa mafisadi, tutakudaka juj juu kama masalia.
 
mie nilifikiri shida zote za wtz zimeisha kumbe umbeya...jitahidi utaongezewa posho
 
Hivi lile Gazeti la Msanii Afrika la Sahara Communication Group ya Gamba Diallo bado lipo?
 
Back
Top Bottom