Yamenikuta mwenzenu. Ushauri tafadhali

May 20, 2017
73
166
Wakuu salam kwenu

Poleni kwa Covid-19

Ngoja niwape mkasa niliona nao kwa sasa

Mnamo mwaka jana mwezi wa 7 niliingia kwenye mahusiano na binti fulani ambaye kwa sasa ana miaka 19

Nimetoka na huyu binti tangu mwaka Jana hadi sasa ,ni mwanachuo ila kwa sasa keshamaliza yupo field

Sasa hivi majuzi kaniambia ana mimba ,mi nikamkatalia ila kasisitiza sana mimba ni Yangu

Nikamwambia mi nina familia ya watoto wawili na mke ingawa tunaishi mbalimbali

Nikamwambia hiyo mimba inabidi itolewe (hapa mnisamehe tu najua watu mtanitukana) kwa sababu sijajiandaa kulea mtoto yoyote kwa sasa na isitoshe hatukupanga kuzaa mtoto Mimi na wewe so mimba itolewe angali changa

Binti kagoma, na isitoshe haoneshi ushirikiano wowote, kiukweli nashindwa kumwelewa huyu binti ananitafuta nini?

Nipeni ushauri jamani nifanyaje manake naona atakuja kuniletea msala tu mbeleni.
-------------------------------------------------------------
UPDATE
-------------------------------------------------------------
BINTI KAKUBALI YAISHE ,AMETOA

Baada ya binti kumshawishi aitoe mimba ambayo hatukuitarajia na akagoma

Niliamua kuachana nae,ila juzi nimekaa zangu home kanitumia msg amekubali aitoe kwa sababu ana wasi wasi kwao watamzingua

Nikamwambia poa ,tukakutana hotelin nikachukua room

Mtoto katumia dawa ndani ya masaa mawili mimba ikatoka na sasa anaendelea vizuri buheri was afya

ONYO: Wanaume wenzangu tuache/tupunguze michepuko na tuangalie wanawake wa kudate nao

Pia tujitahidi kukojolea nje kama tumeshindwa kutumia condom.
 
We jitoe wewe kwanza kwenye dunia...
Kama una mke yeye ulikuwa unamchezea..?

Bado unataka kuua...
Ushauri ni simple tu...

Mpigie mkeo na umuueleze,na umuulize Anakupa ushauri gani...
Pi Acha tamaa mkuu,Tena koma koma kabisa...
 
Mwanakulifind mwana kulipata.

Mnanajisi ndoa zenu wenyewe halafu baadae mnaanza kumsaka mchawi.
Kwani uliambiwa ukizini bila kondom matokeo yake ni mahindi? Vuna ulichopanda.

Mungu amsaidie mkeo isije ikawa haujavuna mimba tu kuna na magonjwa na mabalaa ya kiroho.
 
Kwanza unatembea na binti mdogo...,Miaka 19 sahivi inaashiria mlianza kudate ana miaka 17 au 18 huko... Halafu unamshauri binti afanye unyama je huyo mtoto akija kuwa rais kama jiwe... Wewe unafaa jela tu.
 
Mimba ina miezi mingapi?

Nenda kapime kama ni yako lea......maana kama aliyenayo tumboni kakataa kuitoa huwezi ukajinyesha vidonge ikatoka.

Kikubwa yako. Kakataa kutoa...then lea.
 
Acha ujinga ww si ndo ulimtafuta na sio yeye, acha azae single mother waongezeke na pia utaoa mke wa pili.

Kutoa mimba inaweza toka salama au ikatoka ila akawa mgumba kama wema sepetu, ataishia kule midoli tu.

Hii dhambi mbingu na peponi mtapasikia tu kwenye bible labda unikute getini ndo utaingia peponi
 
Hivi ndo viwanda vya kutengeneza ma single mama, alafu mkishawazalisha mnaanza kuwatukana huku mitandaoni

Alafu naamini kabisa ulimficha kuwa huna mke na ndo maana baada ya mimba una kiri umemwambia una mke yupo mkoa mwingine

Men:Be careful, madhambi mnayofanya kuna siku yatawarudia mnatengeneza kizazi kilichojaa machungu na maumivu kwa tamaa zenu wenyewe

Imagine una date katoto ka 19 yrs, ni aibu mnooooo, at least kama ni lazima kwako basi ungedate hata na 23,24,25 wanakuwa wamepevuka akili hata kuzuia mimba wanajuwa

Sina mengi zaidi ila malipo ni hapa hapa duniani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
You took advantage of the poor 19 year old girl. Yawezekana ulimuona mkubwa ila hajakomaa kiasi cha kufanya maamuzi makubwa.Yawezekana hakua na uhuru wa kukwambia utumie condom au hakujua kuna P2...probably you controlled her.
Ulishindwa kupata mtu saizi yako ukaenda mparamia mtoto wa watu???
Kwa utu uzima huo wa mke na watoto wa wawili ulifikiri kwa huyo binti unamwaga uji au maji??? Uliona ubahili kununua condom???

1. I hate abortion but akikubali shukuru sana and make sure you take her to the best medics usimtie ulemavu na majuto ya baadae mtoto wa watu kwa tamaa zako make sure anapata huduma nzuri.

2. Akishikilia msimamo wa kutunza mimba na kuzaa pia m-support kwasabu utakua umevuruga ramani yake ya maisha....hata kama ataendelea na masomo ila utakua umetia doa kwenye maisha yake.

3. I hope she has a strict family that will stand by her and support her.A family that will also take legal measures againts you ikibidi upigwe mvua za kutosha kwa ujinga wako.

4. Katika hao wanao wawili I hope una binti ambae by the time anafikisha miaka 17 libazazi lingine lijisevie na wewe uone machungu na ugumu wa kuharibiwa mtoto.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha ujinga ww si ndo ulimtafuta na sio yeye, acha azae single mother waongezeke na pia utaoa mke wa pili.

Kutoa mimba inaweza toka salama au ikatoka ila akawa mgumba kama wema sepetu, ataishia kule midoli tu.

Hii dhambi mbingu na peponi mtapasikia tu kwenye bible labda unikute getini ndo utaingia peponi
Hold on, Wema sepetu ni mgumba?
 
Ila wanaume Mungu anawaona jamani, hivi mbona huwa hamfikirii ndoa zenu? maagano yenu ya mbele za Mungu? Hapo mke wako akijua atakaa nafsi inafurukuta kwamba mume wangu alikosa nini kwangu hadi katoka nje ya ndoa kumbe ubazazi wako tu unakusumbua. Na kwanini uue? Lea mtoto huyo na mama yake. Halafu kwenye uzi wa single mother mpo siti ya mbele kabisa kuchangia kumbe ndio kazi zenu kuzalisha watoto wasio na hatia.
 
Unamatatizo wewe..kama unajua unafamilia ulimgegeda ili iweje.jiandae kulea mtoto.
 
Game imeshaisha hiyo
Lea mzigo wako tu huwezijua huyo mtoto anabaraka gani


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom