WENYELE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 1,467
- 1,565
Leo nimepigiwa simu ya shukrani, mama wa binti akilia machozi ya furaha, binti yake kapata mtoto.
Mwaka 2024 mwishoni nilienda kijijini nilikozaliwa, nikakutana na binti aliyemaliza degree na badaye aliolewa na mtumishi mmoja wa serikali
Lakini nilipokutana na huyo binti, kwa rika ni km mdogo wangu wa kunifuata mara tatu, alikua hana haiba, kachoka na kuchakaa kabisa, kulingana na mwonekana wake sikufuatilia sana nilijua tu labda ni stress za maisha na kukosa ajira, ukichukulia kuwa kamaliza degree halafu hajapata ajira km mwaka wa nne hivi.
Baadaye niliondoka zangu nikarudi mjini, siku moja yule binti alinipigia simu, huku akilia (kumbuka ni mdogo wangu km ndugu wa damu ukichukulia ni wa hapo kijijini na kasoma pia). Alinieleza mkasa wake kuwa ameolewa ni mwaka wa nne yaani alimaliza degree na kuolewa, na kwa muda wote huo hajawahi kushika mimba!
Na kama jamii zetu zilivyo, matusi na masimango yote yanaangukia kwake na mama yake, kazungushwa kwa waganga wa kienyeji na hospital kote lakini hakuna matokeo! Mme wake pia ashaanza kumchoka, hali ni mbaya na anatamani tu hata kukatisha maisha yake.
Alinieleza mambo mengi sana, mwisho kabisa akaomba nimpe nauli aende Dar kuombewa kwa Mwamposa.
Kiukweli niliumia sana as a brother, na pia mtu wa karibu wa familia, lakini wakati anaongea nilimsikiliza kwa sikio la ndani kabisa, nikajua tena huenda ashaanza kupata metal health issues/ depressions.
Baada ya kuniambia hivyo, sikumpa jibu la hapo kwa hapo, nikamwambia nitakurudia; baada ya hapo nikamcheki mke wangu nikamwelezea, pia nikamtafuta na mama mmoja tunaheshimiana sana nikawaambia waongee na huyu binti ili kumfariji na kumtoa kwenye stress ya kukosa mimba.
Wamwambie mimba ni majaliwa but uhai na mktadha wake ni wa thamani sana ktk dunia hii; km mme wake anazingua pia, ni maswala ya kawaida kwenye ndoa hasa kukiwa na uncertainities!
Pia nilipambana kutafuta madaktari wa magonjwa ya akina mama; kuna outreach ya specialist ikatokea, nikamwambia akaenda; walimpima akaambiwa hana shida na mme wake hana shida ila tu binti anasumbuliwa na mambo ya hormones.
Baada ya muda mambo yakawa mabaya; alizorota kiafya, kiakili na kiuchumi, ilibidi nifunge safari kwenda kijijini kwetu tena; nikiwa pamoja na mke wangu. Tulienda kuonana naye pamoja na mama yake mzazi.
Kiukweli km mnavyojua jamii za kijijini, mama binti naye alikua kachoka, ana stress ya binti yake kutoshika ujauzito.
Lakini pia niligundua wanatumia madawa bila mpangilio na nikahisia pia ndo yanaharibu.
Nilipoona hivyo, nilikaa na yule binti, nikamwambia kama utaweza, acha kutumia dawa yoyote kwa muda wala kuwaza kuhusu mimba.
Usinywe wala kutumia chochote na wala usiende sijui wapi kuombewa au kufanya chochote sababu ya ndoa au kupata mtoto. Pumzika sasa, pumzisha mwili na akili, baki na Mungu wako na nafsi yako tu, anza kujihusisha na mambo ya uchumi na kuwa busy; Mke wangu naye aliongea naye kwa sana badaye tukakubaliana tukamkatia bima ya afya.
Ni kweli yule binti alifuata ushauri wetu, from no where akaja kupata ujauzito; amelea bioa shida na mwezi huu kajifungua.
Mama yake amepiga simu kushukru, akiwa analia kwa furaha.
Nasi tumefarijika kusikia binti yake kapata mtoto.
Hakika MUNGU hamtupi mja wake