Slim5
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 28,108
- 37,644
Nimeumia sana ndani.
Kama mnavojua wanajamii, mahaba ya wazazi wa kiume kwa watoto wao wa kike, kwangu binti yangu ndio kila kitu, hili hata mke wangu anajua, wanajamii wanaonizunguka wanajua, hata binti yangu mwenyewe anajua! Sina na sitaki masihara katika malezi. Nimejitolea kuinvest kwa watoto wangu, mia kwa mia, ukifanya baya kwa bint yangu, utakuwa umenikosea katika kiwango ambacho hakimithiliki! Nitapambana mpaka tone la mwisho. Hapa nitakufa na mtu.
Nimepatwa na mtihani. Nina maumivu.
Kabinti kangu, first born kangu, only 9 yrs, kanasoma grade 4, shule moja ya english medium, ipo nje kidogo ya jiji. shule hii ni miongoni mwa utitiri wa shule za msingi hapa nchini zinazopenda kuajiri walimu wa kigeni, na hasa hawa jamaa zetu kutoka Uganda.
Mwalimu wa maths wa grade 4, ni Mganda. Huyu mwl sina uhakika na proffessional qualifications zake, lakini kwangu kama mzazi, nimemdisqualify - hafai kuwa mwalimu.
Binti yangu amekuwa akisakamwa na mwl huyu kwa kauli za kimasimango, na hasa akimdhihaki kwamba, amerudia grade 4 "kwa kuwa she is a lazy girl". Ni kweli sio genius, lakini ni sisi wazazi ndio tulioishinikiza shule mwaka jana, kuwa bint asiingie grade 5 mwaka huu, kwa hofu ya umri wake kuwa mdogo sana.
Kwa mwalimu kutumia kauli ya dhihaka kwa mwanafunzi, kuna madhara makubwa ktk ukuaji wa akili wa mtoto, hii wataalamu wa psychology wanaelewa zaidi, pia kunamuondolea sifa stahiki mwl yule. Lakini hilo ni kwa upande mmoja, kwa upande wa pili, mwl amekuwa akiwaadhibu watoto wa kike kwa kuwachapa sehemu zao za siri, kwa kutumia rula kubwa ya ubaoni, bint yangu ni mhanga wa adhabu hii, niliumia sana kusimuliwa hivi na bint yangu.
Binti yangu amenilelezea namna mwl alivokuwa anawatisha endapo watoto wangeripot adhabu hii kwa wazazi, bint yangu ananambia amefanyiwa hivi mara 3. Nimemuuliza binti yangu kama mwalimu amewahi kumfanyia kitu chochote cha zaidi ama kinachofanana na hivo. Nikamuuliza kama ni yeye tu ama kuna wasichana wengine pia wameadhibiwa kama hivo, bint amenambia ni wasichana kadhaa wa darasa lao wamekuwa wakifanyiwa hivi na mwalimu.
Nimejiridhisha kwamba binti yangu hakuna madhara alioyapata kutokana na mateso/manyanyaso ya mwl huyu. Mungu mkubwa, namshukuru Mungu.
Nimechukua hatua kadhaa, ikiwemo kutaka maelezo sahihi kutoka kwa mwl mkuu, ambae akaniunganisha na mwl husika - hakukuwa na la maana ktk yale ambayo mwl amenielezea, japo mwl mkuu alionyesha kujali, na kuumia kwa utendaji mbovu wa mwalimu wake (mwl mkuu na huyu mwl wa maths - wote ni waganda), mwl mkuu amenisihi niwe na subira kipindi hiki ambacho shule zimefungwa, afanye uchunguzi zaidi, anasema hata yeye amefedheheka sana kwa hili, huyu mwalimu mkuu ni mwanamama.
Nimemuahidi mwalimu mkuu kuwa na mimi nitalifuatilia kivyangu ktk ngazi husika! Kwa kifupi wanajamii, najipanga, nataka iwe fundisho kwa walimu na wenye shule za binafsi wenye tabia za kuajiri hovyo hovyo hawa walimu wa kigeni, iwe fundisho pia kwa walimu wanaocheza na ustawi wa watoto wetu.
Lakini pia naomba nitoe angalizo kwa wazazi wenzangu, tuendeleze utamaduni wetu wa kuwa karibu na watoto wetu, watuambie yale ambayo watoto hawa wanalazimishwa kuyaweka mioyoni mwao, tuwaelimishe watoto wetu wawe na courage ya kusema chochote kile ambacho ni kibaya, tuwaambie kuwa vitendo (mzazi weka bayana mtoto ajue vitendo asivopaswa kufanyiwa) 1, 2, 3, 4 n.k ukifanyiwa ama ukiambiwa, na mtu yeyeto yule, shuleni, mtaani ama nyumbani, awe tayari kusema kwa mama, baba ama mlezi wake haraka sana! Tukijua magumu ya watoto wetu mapema, itatusaidia kuwaokoa kutoka katika hatari yoyote ile inayowakaribia!
Hali ni mbaya jamani, sasa hata mashuleni sio tena sehemu salama kwa watoto wetu.
Mungu walinde watoto wetu.