Yamenikuta: Mashuleni sio sehemu salama tena kwa watoto wetu

Slim5

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
25,519
2,000
Nimeumia sana ndani.

Kama mnavojua wanajamii, mahaba ya wazazi wa kiume kwa watoto wao wa kike, kwangu binti yangu ndio kila kitu, hili hata mke wangu anajua, wanajamii wanaonizunguka wanajua, hata binti yangu mwenyewe anajua! Sina na sitaki masihara katika malezi. Nimejitolea kuinvest kwa watoto wangu, mia kwa mia, ukifanya baya kwa bint yangu, utakuwa umenikosea katika kiwango ambacho hakimithiliki! Nitapambana mpaka tone la mwisho. Hapa nitakufa na mtu.

Nimepatwa na mtihani. Nina maumivu.

Kabinti kangu, first born kangu, only 9 yrs, kanasoma grade 4, shule moja ya english medium, ipo nje kidogo ya jiji. shule hii ni miongoni mwa utitiri wa shule za msingi hapa nchini zinazopenda kuajiri walimu wa kigeni, na hasa hawa jamaa zetu kutoka Uganda.

Mwalimu wa maths wa grade 4, ni Mganda. Huyu mwl sina uhakika na proffessional qualifications zake, lakini kwangu kama mzazi, nimemdisqualify - hafai kuwa mwalimu.

Binti yangu amekuwa akisakamwa na mwl huyu kwa kauli za kimasimango, na hasa akimdhihaki kwamba, amerudia grade 4 "kwa kuwa she is a lazy girl". Ni kweli sio genius, lakini ni sisi wazazi ndio tulioishinikiza shule mwaka jana, kuwa bint asiingie grade 5 mwaka huu, kwa hofu ya umri wake kuwa mdogo sana.

Kwa mwalimu kutumia kauli ya dhihaka kwa mwanafunzi, kuna madhara makubwa ktk ukuaji wa akili wa mtoto, hii wataalamu wa psychology wanaelewa zaidi, pia kunamuondolea sifa stahiki mwl yule. Lakini hilo ni kwa upande mmoja, kwa upande wa pili, mwl amekuwa akiwaadhibu watoto wa kike kwa kuwachapa sehemu zao za siri, kwa kutumia rula kubwa ya ubaoni, bint yangu ni mhanga wa adhabu hii, niliumia sana kusimuliwa hivi na bint yangu.

Binti yangu amenilelezea namna mwl alivokuwa anawatisha endapo watoto wangeripot adhabu hii kwa wazazi, bint yangu ananambia amefanyiwa hivi mara 3. Nimemuuliza binti yangu kama mwalimu amewahi kumfanyia kitu chochote cha zaidi ama kinachofanana na hivo. Nikamuuliza kama ni yeye tu ama kuna wasichana wengine pia wameadhibiwa kama hivo, bint amenambia ni wasichana kadhaa wa darasa lao wamekuwa wakifanyiwa hivi na mwalimu.

Nimejiridhisha kwamba binti yangu hakuna madhara alioyapata kutokana na mateso/manyanyaso ya mwl huyu. Mungu mkubwa, namshukuru Mungu.

Nimechukua hatua kadhaa, ikiwemo kutaka maelezo sahihi kutoka kwa mwl mkuu, ambae akaniunganisha na mwl husika - hakukuwa na la maana ktk yale ambayo mwl amenielezea, japo mwl mkuu alionyesha kujali, na kuumia kwa utendaji mbovu wa mwalimu wake (mwl mkuu na huyu mwl wa maths - wote ni waganda), mwl mkuu amenisihi niwe na subira kipindi hiki ambacho shule zimefungwa, afanye uchunguzi zaidi, anasema hata yeye amefedheheka sana kwa hili, huyu mwalimu mkuu ni mwanamama.

Nimemuahidi mwalimu mkuu kuwa na mimi nitalifuatilia kivyangu ktk ngazi husika! Kwa kifupi wanajamii, najipanga, nataka iwe fundisho kwa walimu na wenye shule za binafsi wenye tabia za kuajiri hovyo hovyo hawa walimu wa kigeni, iwe fundisho pia kwa walimu wanaocheza na ustawi wa watoto wetu.

Lakini pia naomba nitoe angalizo kwa wazazi wenzangu, tuendeleze utamaduni wetu wa kuwa karibu na watoto wetu, watuambie yale ambayo watoto hawa wanalazimishwa kuyaweka mioyoni mwao, tuwaelimishe watoto wetu wawe na courage ya kusema chochote kile ambacho ni kibaya, tuwaambie kuwa vitendo (mzazi weka bayana mtoto ajue vitendo asivopaswa kufanyiwa) 1, 2, 3, 4 n.k ukifanyiwa ama ukiambiwa, na mtu yeyeto yule, shuleni, mtaani ama nyumbani, awe tayari kusema kwa mama, baba ama mlezi wake haraka sana! Tukijua magumu ya watoto wetu mapema, itatusaidia kuwaokoa kutoka katika hatari yoyote ile inayowakaribia!

Hali ni mbaya jamani, sasa hata mashuleni sio tena sehemu salama kwa watoto wetu.

Mungu walinde watoto wetu.
 
Himidini

JF-Expert Member
May 8, 2013
5,542
1,225
Fuatilia kwa umakini mwakani utupe mrejesho,itakuwa vema ikiwa utawadadisi pia watoto wengine wanaotajwa ktk hili, maana huwezi jua upande upi uko katika KWELI.
Pole sana Mkuu.
^^
 
Slim5

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
25,519
2,000
Fuatilia kwa umakini mwakani utupe mrejesho,itakuwa vema ikiwa utawadadisi pia watoto wengine wanaotajwa ktk hili, maana huwezi jua upande upi uko katika KWELI.
Pole sana Mkuu.
^^
Mkuu Himidini nitafuatilia kila hatua, nipo karibu sana na huyu mkuu wa shule!
 
Last edited by a moderator:

Heaven Sent

JF-Expert Member
Sep 27, 2013
21,085
2,000
Pole mkuu na hongera kwa Kuwa baba bora kwa binti yako. Hope utatupa mrejesho ya kipi kilichoendelea Kwa mwalimu Huyo. Kila la Kheri na uchunguzi unaoendelea
 
Sukula

JF-Expert Member
Jun 16, 2012
1,199
1,225
Pole mkuu, huyo mwl hana sifa ya kuwa mwl kbs. Ht km mtoto amerudia darasa yy inamhusu nini?
Fatilia mkuu ili iwe fundisho kwa walimu vilaza kama huyo.
 
steveachi

JF-Expert Member
Nov 7, 2011
6,500
2,000
pole sana mkuu kwa yaliyokukuta,kumbe slim5 ni jina lako?,mi nilivyoona heading yako tu nilijua umetumia ile midawa ya kupunguza uzito iyoitwa slim nini sijui,nikajua imekutenda,pole sana,endelea kufuatilia,sio janga dogo hilo kaka,asije kutuhribia binti yetu mwehu wa kiganda huyo
 
Last edited by a moderator:

Slim5

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
25,519
2,000
pole sana mkuu kwa yaliyokukuta,kumbe slim5 ni jina lako?,mi nilivyoona heading yako tu nilijua umetumia ile midawa ya kupunguza uzito iyoitwa slim nini sijui,nikajua imekutenda,pole sana,endelea kufuatilia,sio janga dogo hilo kaka,asije kutuhribia binti yetu mwehu wa kiganda huyo
steveachi nashukuru sana mkuu
 
Last edited by a moderator:

Slim5

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
25,519
2,000
Pole mkuu, huyo mwl hana sifa ya kuwa mwl kbs. Ht km mtoto amerudia darasa yy inamhusu nini?
Fatilia mkuu ili iwe fundisho kwa walimu vilaza kama huyo.
mkuu Sukula nashukuru sana!
 
Last edited by a moderator:

Mwana

JF-Expert Member
Aug 6, 2010
5,254
2,000
Yaani pole sana na vizuri ulivyochukua hatua ili si kumuokoa binti yako tu na wengine wa ambao wangekuwa chini ya himaya ya huyu mwalimu. Nami yalinikuta ya aina tofauti maana mwanangu alikuwa anasoma shule inayoondeshwa na wahindi. Wengi wa wanafunzi walitoka from well to do family kukawa kama kuna kadharau Fulani nilifunga safari mpaka kwa Mkurugenzi wa shule ambaye according tu mwanangu huwa anaruhusu wageni kwa nadra mi nili-insist kumuona yeye akanipa nafansi nilikuja juu akanituliza na kusema tutashughulikia na akafanya na haikujiruida. We are not saying watoto wadekezwe no, lakini wasionewe! Na wakati mwingine vitendo vinafanyika owners hawana habari.
Hongerah sanaSlim5, walu hujifunza psycology na wanatakiwa waitumie: equality kwa watoto inatakiwa despite their variation in performance!
 
kamagetac

JF-Expert Member
Jul 25, 2014
2,478
2,000
Fuatilia mpaka ujue mwisho wake walimu kama huyo wako wengi,mimi mwanangu wa kiume mwalimu wake alikuwa akimnyanyasa na siku moja alipomaliza kuandika akaenda kumuonyesha, alimmwagia chai ya moto kifuani na mtoto akaja kueleza nyumbani mbona aliachishwa kazi na wengine wamejirekebisha
 
yaaani kuna walimu wa hovyo sana kumbe kamagetac
 
Last edited by a moderator:

luckyline

JF-Expert Member
Aug 29, 2014
11,244
2,000
belie ahsante sana
anawapiga na rula sehem za siri??? hiii hainiingii akilini kafatilie hili kwa kina mengine ni kuhelimishana atabadilika. sio sifa kukurupushana na watu ama vipi mwamishe mwanao coz wew ndo unajua thaman yake
 
Last edited by a moderator:

Slim5

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
25,519
2,000
Yaani pole sana na vizuri ulivyochukua hatua ili si kumuokoa binti yako tu na wengine wa ambao wangekuwa chini ya himaya ya huyu mwalimu. Nami yalinikuta ya aina tofauti maana mwanangu alikuwa anasoma shule inayoondeshwa na wahindi. Wengi wa wanafunzi walitoka from well to do family kukawa kama kuna kadharau Fulani nilifunga safari mpaka kwa Mkurugenzi wa shule ambaye according tu mwanangu huwa anaruhusu wageni kwa nadra mi nili-insist kumuona yeye akanipa nafansi nilikuja juu akanituliza na kusema tutashughulikia na akafanya na haikujiruida. We are not saying watoto wadekezwe no, lakini wasionewe! Na wakati mwingine vitendo vinafanyika owners hawana habari.
Hongerah sanaSlim5, walu hujifunza psycology na wanatakiwa waitumie: equality kwa watoto inatakiwa despite their variation in performance!
Mwana ni kweli wangu (hii shule ya mwanao sio ileee .... baada ya daraja unaingia kushoto?)
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom