Ninawapenda sana walimu wangu

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Japo ni miaka mingi sijaonana na wengi wao, lakini ningali nikiwakumbuka sana.

Wapo walionifundisha shule ya Msingi, wengine Sekondari, wengine High School na wengine Chuo Kikuu. Wote hao ni walimu wangu na ninawaheshimu wote.

Kama ningetakiwa nitoe kipaumbele katika kuwaheshimu, ningeanzia na wa shule ya Msingi na kufuatiwa na wa Sekondari. Walinijengea msingi imara ambao umechangia kwa namna moja au nyingine kuwa nilivyo. Hata kama nimewazidi wengi kwa kipato, hasa ikizingatiwa kuwa wengi wao walishastaafu, lakini heshima yangu kwao haitokaa ipungue.

Nawakumbuka walimu wangu! Nawaheshumu walimu wangu!

Hivi nitaanzaje kumsahau Mwl Mtui, aliyeanza kunifundisha nikiwa sijui hata kushika penseli?

Nitaanzaje kumsahau Mwl. Munisi aliyenilea kama mwanaye ingawa kiumri alikuwa sawa na dada yangu?

Nitawezaje kumsahau Mwl Kisasaka aliyenifanya nilipende somo la English tokea nikiwa darasa la tano?

Nitaanzaje kumsahau Mwl Mariki aliyeniamini kiasi cha kunifanya na mimi kujiamini na hivyo kushikilia nafasi ya kwanza mpaka nahitimu darasa la saba?

Nitawezaje kumsahau aliyekuwa Mwalimu wetu mkuu, Mwl Minja, Mwalimu aliyekuwa na moyo wa ubaba kwa wanafunzi wake? Ndiyo maana hata tulipokuwa darasa la saba, ilipogundulika kuwa tuliiba past papers na mafaili matupu kwenye ofisi ya walimu kwa lengo la kutunzia rundo la past papers tulizokuwa tukizimiliki, kesi ilipofika kwake, aliuliza tu kama kuna kitu kingine kilichopotea. Alipofahamu kuwa hakipo, alisema tusamehewe. Alijua kuwa lengo letu lilikuwa ni jema japo tulilitekeleza isivyo halali.

Nitawezaje , kwa mfano, kumsahau Mwl Abraham, headmaster bora kupata kumfahamu? Ilikuwa ni kawaida yake kutuusia na kututia moyo mara kwa mara tusome kwa bidii. Hamasa yake ilitupeleka tushike nafasi ya pili kimkoa katika mitihani yetu ya Form Two.

Ilikuwa ni kawaida yake Mwl Abraham kututemblea bwenini mara kwa mara saa nane za Usiku akiwa na gobore lake kuwaamsha form two na four kwa ajili ya kwenda kujisomea. Nitawezaje kumsahau baba kama huyo?

Siyo bure, hata baada ya kustaafu Uheadmaster, wanafunzi wake wengi waliendelea kumkumbuka.

Alipopokea mafao yake, alienda Dar kununua gari la kutembelea. Bila kutarajia , alienda kwenye showroom ya mmoja wa vijana aliowahi kuwafundisha. Alilipata gari alilolihitaji, lakini hakulipia hata shilingi. "Wanafunzi" wake waliokuwa wanafanya biashara Dar walijulishana na wakaamua kushirikiana kumnunulia gari alilolihitaji.

Nitawezaje kumsahau Mwl Manase ambaye alinichukulia kama mdogo wake japo tulifahamiana nikiwa form two? Nilipokuwa nikihitaji kupiga simu nyumbani, alikuwa akinipa simu yake bila hata kunitaka niifidie vocha ambayo ilikuwa ghali kidogo kipindi hicho ambacho ni watu wachache tu ndiyo waliokuwa na simu kijijini kwetu.

Nitawezaje kumsahau Mwl Urassa, Mwl aliyenifanya nilipende somo la Jiogragia? Ndiye aliyenichochea hata nikaingia kwenye baraza la Serikali ya wanafunzi kama kiranja wa Nidhamu na Elimu!

Ilikuwa nikikosa nauli, nilijua pankwenda kichukulia. Kama si kwa Mwal Urassa, basi ni Manase au mhasibu wetu, Ngaka. Nilikuwa nikiwakopa na kuwarejeshea tunapofungua shule.

Nawezaje kumsahau Mwl Mjie, bingwa wa Historia aliyekuwa akiogopwa na wanafunzi wengi lakini mimi nikawa kama rafiki yake?

Nawezaje kumsahau Mwl Majaliwa, bingwa wa kufundisha Chemistry bila kutumia notes za kwenye madaftari?

Nawezaje kumsahau Mwl wangu wa English "O" level aliyenifanya niwe tayari kulijibu swali lake kila aingiapo darasani?

Hao ni wachache tu miongoni mwa wengi, wa shule ya Msingi na Sekondari.

Ninawaheshimu sana walimu wangu!

Ninawakumbuka sana walimu wangu!

Ninawapenda sana walimu wangu!

Nimewamisi sana walimu wangu!

Wengi wanaweza wakawadharau walimu wao, lakini kamwe mimi sitafanya hivyo.

Ikimpendeza Mungu, iko siku nitawafanyia "surprise"

Naweza nisiwafanyie wote, lakini nikiweza kuwanunulia IST alau watatu, nitakuwa nimefanya jambo la maana sana.

Iko siku🙏
 
Hongera sana, ni wachache sana wako wewe, wengi wanawatukana humu JF.
 
Back
Top Bottom