Yamenikuta: Mashuleni sio sehemu salama tena kwa watoto wetu

Mimi wanangu japo niko mbali mazungumzo yangu nao (daily kwa Skype) ni jinsi walivyoshinda shuleni...
Mpaka baba yao anashangaa jinsi wanavyofunguka huku yeye yuko nao muda wote na hawamwambiii

Mfano watoto wangu uwa nawauliza hata maraifiki na maadui zao shuleni...maana siwezi kuvumilia mwanangu kuwa bullied...na ni kitu ambacho wazazi wengi hawakijui sababu hawana muda wala wazo la kuuliza...

Utasikia mama xx hataki kucheza na mimi anasema anipendi...namwambia you are 100 times better than him...kama mtu anakwambia hakupendi mwambie na wewe huna mpango nae...una marafiki wengi including me your mom...

Bullying inaua sana confidence za watoto kama mnakumbuka kuna watoto walikuwa wabeba mabegi ya wababe mashuleni...not my sons...

Hata la walimu kupiga wanangu sitaki...viboko si marufuku? Sitaki mwanangu aogope shule kisa fimbo...hii ni karne ya 21....viboko mashuleni vya kazi gani...?
 
......kama possible wapige marufuku hapo shuleni kukupigia binti yako.

Kama binti akifanya kosa lolote waambie wakupe taarifa......wewe kama mzazi ndio umpe mwanao adhabu.

Mimi kwa kweli sipendi mtu ampe mwanangu adhabu ya kupiga au yoyote ile. Mwanangu akifanya kosa niambie then mimi ndio mwenye mamlaka ya kumwadhibu.
 
......kama possible wapige marufuku hapo shuleni kukupigia binti yako.

Kama binti akifanya kosa lolote waambie wakupe taarifa......wewe kama mzazi ndio umpe mwanao adhabu.

Mimi kwa kweli sipendi mtu ampe mwanangu adhabu ya kupiga au yoyote ile. Mwanangu akifanya kosa niambie then mimi ndio mwenye mamlaka ya kumwadhibu.

,,,,,,,,,mh!mtoto anaweza kuwa mtukutu na kuhitaji vi adhabu mara kadhaa!Kila wakati tukuite um rectify behavior si itakuwa adhabu kwa mzazi?
 
Nikikumbuka tulivyokua tunatandikwa "midati" enzi hizooo kwa utundu shuleni...sina hamu.Na vichwa vilikuwa bright!
 
Malezi yamekuwa shida sana siku hizi.........kama ambavyo ualimu umekuwa shida pia. Ni kama walimu na wazazi ama wanawindana au hawaaminiani kuhusu nani anafanya yaliyo sahihi kwa mtoto.
 
Nimeumia sana ndani.

Kama mnavojua wanajamii, mahaba ya wazazi wa kiume kwa watoto wao wa kike, kwangu binti yangu ndio kila kitu, hili hata mke wangu anajua, wanajamii wanaonizunguka wanajua, hata binti yangu mwenyewe anajua! Sina na sitaki masihara katika malezi. Nimejitolea kuinvest kwa watoto wangu, mia kwa mia, ukifanya baya kwa bint yangu, utakuwa umenikosea katika kiwango ambacho hakimithiliki! Nitapambana mpaka tone la mwisho. Hapa nitakufa na mtu.

Nimepatwa na mtihani. Nina maumivu.

Kabinti kangu, first born kangu, only 9 yrs, kanasoma grade 4, shule moja ya english medium, ipo nje kidogo ya jiji. shule hii ni miongoni mwa utitiri wa shule za msingi hapa nchini zinazopenda kuajiri walimu wa kigeni, na hasa hawa jamaa zetu kutoka Uganda.

Mwalimu wa maths wa grade 4, ni Mganda. Huyu mwl sina uhakika na proffessional qualifications zake, lakini kwangu kama mzazi, nimemdisqualify - hafai kuwa mwalimu.

Binti yangu amekuwa akisakamwa na mwl huyu kwa kauli za kimasimango, na hasa akimdhihaki kwamba, amerudia grade 4 "kwa kuwa she is a lazy girl". Ni kweli sio genius, lakini ni sisi wazazi ndio tulioishinikiza shule mwaka jana, kuwa bint asiingie grade 5 mwaka huu, kwa hofu ya umri wake kuwa mdogo sana.

Kwa mwalimu kutumia kauli ya dhihaka kwa mwanafunzi, kuna madhara makubwa ktk ukuaji wa akili wa mtoto, hii wataalamu wa psychology wanaelewa zaidi, pia kunamuondolea sifa stahiki mwl yule. Lakini hilo ni kwa upande mmoja, kwa upande wa pili, mwl amekuwa akiwaadhibu watoto wa kike kwa kuwachapa sehemu zao za siri, kwa kutumia rula kubwa ya ubaoni, bint yangu ni mhanga wa adhabu hii, niliumia sana kusimuliwa hivi na bint yangu.

Binti yangu amenilelezea namna mwl alivokuwa anawatisha endapo watoto wangeripot adhabu hii kwa wazazi, bint yangu ananambia amefanyiwa hivi mara 3. Nimemuuliza binti yangu kama mwalimu amewahi kumfanyia kitu chochote cha zaidi ama kinachofanana na hivo. Nikamuuliza kama ni yeye tu ama kuna wasichana wengine pia wameadhibiwa kama hivo, bint amenambia ni wasichana kadhaa wa darasa lao wamekuwa wakifanyiwa hivi na mwalimu.

Nimejiridhisha kwamba binti yangu hakuna madhara alioyapata kutokana na mateso/manyanyaso ya mwl huyu. Mungu mkubwa, namshukuru Mungu.

Nimechukua hatua kadhaa, ikiwemo kutaka maelezo sahihi kutoka kwa mwl mkuu, ambae akaniunganisha na mwl husika - hakukuwa na la maana ktk yale ambayo mwl amenielezea, japo mwl mkuu alionyesha kujali, na kuumia kwa utendaji mbovu wa mwalimu wake (mwl mkuu na huyu mwl wa maths - wote ni waganda), mwl mkuu amenisihi niwe na subira kipindi hiki ambacho shule zimefungwa, afanye uchunguzi zaidi, anasema hata yeye amefedheheka sana kwa hili, huyu mwalimu mkuu ni mwanamama.

Nimemuahidi mwalimu mkuu kuwa na mimi nitalifuatilia kivyangu ktk ngazi husika! Kwa kifupi wanajamii, najipanga, nataka iwe fundisho kwa walimu na wenye shule za binafsi wenye tabia za kuajiri hovyo hovyo hawa walimu wa kigeni, iwe fundisho pia kwa walimu wanaocheza na ustawi wa watoto wetu.

Lakini pia naomba nitoe angalizo kwa wazazi wenzangu, tuendeleze utamaduni wetu wa kuwa karibu na watoto wetu, watuambie yale ambayo watoto hawa wanalazimishwa kuyaweka mioyoni mwao, tuwaelimishe watoto wetu wawe na courage ya kusema chochote kile ambacho ni kibaya, tuwaambie kuwa vitendo (mzazi weka bayana mtoto ajue vitendo asivopaswa kufanyiwa) 1, 2, 3, 4 n.k ukifanyiwa ama ukiambiwa, na mtu yeyeto yule, shuleni, mtaani ama nyumbani, awe tayari kusema kwa mama, baba ama mlezi wake haraka sana! Tukijua magumu ya watoto wetu mapema, itatusaidia kuwaokoa kutoka katika hatari yoyote ile inayowakaribia!

Hali ni mbaya jamani, sasa hata mashuleni sio tena sehemu salama kwa watoto wetu.

Mungu walinde watoto wetu.

Very sad. Pole dear. Ni kuwaombea watoto wetu ili Malaika Wa Mungu wawalinde. Inauma duh pole sana. Naungana na wewe usikubali mpaka sheria ifanye kazi yake, hiyo ni child abuse. Thanks!
 
Mkuu taja shule please ikiwezekana na jina la huyu mwalimu mshenzi
asipo ondolewa watu wakamchape vibao.....this is serious
 
Mkuu taja shule please ikiwezekana na jina la huyu mwalimu mshenzi
asipo ondolewa watu wakamchape vibao.....this is serious

I can't imagine anyone violating my little girl.

I just can't!

I feel this dad's pain and I must commend him for his show of restraint.

Because if it were me......only god knows what I'd have done to that pervert (and I'm an agnostic saying that).
 
I can't imagine anyone violating my little girl.

I just can't!

I feel this dad's pain and I must commend him for his show of restraint.

Because if it were me......only god knows what I'd have done to that pervert (and I'm an agnostic saying that).


Huyu mwalimu kwa vyovyote vile ni sexual predator
anachofanya now ni kuandaa mazingira for future attacks
so ndo maana namtaka amtaje au ikiwezekana ataje shule
akichunguzwa huyu mwalimu utakuta kuna wanafunzi huko Uganda au popote alipopitia ambao alisha waa attack
sexually.....

sion reason why asitajwe...au shule isitajwe sabau hii ishu ni usalama wa wanafunzi wengi..

ni public security ishu
 
Huyu mwalimu kwa vyovyote vile ni sexual predator
anachofanya now ni kuandaa mazingira for future attacks
so ndo maana namtaka amtaje au ikiwezekana ataje shule
akichunguzwa huyu mwalimu utakuta kuna wanafunzi huko Uganda au popote alipopitia ambao alisha waa attack
sexually.....

sion reason why asitajwe...au shule isitajwe sabau hii ishu ni usalama wa wanafunzi wengi..

ni public security ishu

Hatari!
Upo sahihi mkuu , wanaanziaga mbali ili kuweza kuwadominate prey wao ili mwisho wa siku wakitenda yao victim asiweze kuchukua hatua stahiki.
Huyo mtu ni hatari kwa mustakabali wa watoto wetu.
 
Huyu mwalimu kwa vyovyote vile ni sexual predator
anachofanya now ni kuandaa mazingira for future attacks
so ndo maana namtaka amtaje au ikiwezekana ataje shule
akichunguzwa huyu mwalimu utakuta kuna wanafunzi huko Uganda au popote alipopitia ambao alisha waa attack
sexually.....

sion reason why asitajwe...au shule isitajwe sabau hii ishu ni usalama wa wanafunzi wengi..

ni public security ishu

Hivi sisi tuna hata sex offender registry ya uongo na kweli?
 
Hivi sisi tuna hata sex offender registry ya uongo na kweli?

aisee hatuna record za aina yeyote
unaweza endesha gari huku umelewa ukagonga na kuua...
halafu kesho yake ukaendesha tena gari ingine
hatuna hata suspension za mda za leseni au ku revoke watu wasiendeshe magari ya abiria for a while
sisi ni mambo full kienyeji...
 
C'mooooon dude how can u wait till january..!
Hastahili kabisa kua mwalimu uyo nyang'au na unavyosubiri unampa nafasi ya kujipanga na mkuu ukichukulia ni Mganda mwenzie wanaweza kukuzidi maarifa u better take next step ASAP.
Duh mimi nisingeweza kukaa meza moja nae kujadiliana nae kama wewe lazima ningelizua.
 
Jamani its very pain, very pain . I can't imagine anybody to touch my daughter like that , God knows. Hivi bongo ndivyo tunavyoelekea? Eeee Mungu tusaidie, yaani nimefikiria sana hii Bado sijaielewa kwa Kweli . Mmmhh, No its not suppose to be this way, Mhhuuhh No kwa Kweli. Ndugu Nashukuru sana kwa kulileta hapa, binafsi imenipa upeo ,especially Nina mpango Wa kurudi kwetu for good in the future , so hata nikiamua kurudi nitakuwa muuangalifu kuhusu shule gani mwanangu/ wanangu wasome kwa Kweli. Ingekuwa Huku uh huyo mwalimu tungeshamsahau longtime ago. Kwa sababu sheria si mchezo. Angepoteza mpaka license yake ya Kazi . Government nyumbani wanafanya nini kwenye hili swala kwa maana hili swala inaelekea lilikuwa before na litaendelea tuu God forbid jamani eehee Mungu , waokoe watoto wetu . Duuh machozi hayaishi honestly . Nina hasira na huyo Mwalimu yaani acha tuu. Thanks!
 
Back
Top Bottom