Yaliyonikuta na Basi la Kilimanjaro Express

Yaliyonikuta na Basi la Kilimanjaro Express

BM nao hivyo hivyo.....Nilipanda Luxury yao, nilitaabika mno. Nilishindwa nyoosha miguu kwani siti zimebanana mno. Bahati mbaya siti ya mbele yangu ilikuwa haiwezi kuwa adjusted hivyo ikawa inanibana kishenzi!
Ni kweli baadhi ya BM siti zake zibana ila sio zote

Ukitaka kuenjoy panda
Kidia One DWL/DTC
Tahmeed
Marangu Coach
Tilisho Safari
Kilimanjaro DMH/DPT/DHY au namba E
Esther Luxury
Extra Luxury
Dar Express DWU
 
Ni kweli baadhi ya BM siti zake zibana ila sio zote

Ukitaka kuenjoy panda
Kidia One DWL/DTC
Tahmeed
Marangu Coach
Tilisho Safari
Kilimanjaro DMH/DPT/DHY au namba E
Esther Luxury
Extra Luxury
Dar Express DWU
Alooo
We ni unazurura balaa 😂😂

Marangu mm first day tu nilipata boreko. Nikaconclude ni wabovu siwezi warudia

Kidia one never disappoints
 
Kwa tunaosafiri sana kuelekea mikoa ya Kaskazini tunatambua nafasi na heshima ya kampuni ya mabasi ya Kilimanjaro Express, iliyojiwekea kwa kipindi kirefu. Tuliamini ilichukua nafasi ya Dar Express, ikawa hawana mpinzani.

Ila hivi karibuni imekuwa tofauti, nimesikia mara nyingi watu wakisema hawapandi tena mabasi ya Kilimanjaro, ni kama sikuelewa hadi yaliyonisibu jana.

Safari ilianza saa moja na nusu asubuhi, Arusha. "Disappointment" ya kwanza ni kwenye gari tulilokuta stendi, tofauti na matarajio yangu. Tuliambiwa gari ni "luxury", kwa nauli ya 40,000/-. Lakini kitu pekee cha ki-luxury ndani ya basi hilo kilikuwa ni choo, hakuna zaidi.

"Seat covers" chakavu, zulia la chini lilikiwa na vumbi lilitimka kila watu walipopita.

Gari halikuwa na kiyoyozi, hii sikutegemea kabisa, hasa kuwa nilishaandaa koti la kuvaa nikiwa ndani.

Safari iliendelea lakini gari hakikuwa na mwendo wa kuridhisha, na kufika eneo la Makuyuni, Korogwe, likazima kabisa. Muhudumu wa ndani ya gari akatangaza kuomba radhi na kuwa abiria wasubiri kidogo. Hapo abiria wakawa wakali wakihoji sababu ya kusubiri. Hapo ndipo nikajua wengi hawakuwa wameridhika na hali ya basi lile.

Tukateremka, watu wakajitafutia hifadhi kwenye vivuli vichache na wengine kwenda madukani kujitafutia chochote kitu. Baadae sana dereva akatafuta basi dogo la abiria kutuchukua hadi hitelini kwao Korogwe.... hapo sasa tulikaa kuanzia saa saba na nusu mchana hadi saa mbili na nusu usiku tulipopata nafasi kwenye basi jingine la kampuni hiyo hiyo.

Tarehe 8 Desemba, nilipanda tena basi Lao la mchana kuelekea Arusha. Tulipofika kipande cha kuanzia Same hadi Njia Panda kulikuwa na mvua kubwa. Sikutegemea, ila basi lilikuwa linavuja na nililazimika kusimama hadi Moshi, bikapata nafasi ya kukaa baada ya abiria kadhaa kushuka. Hapo nilitambua pia kuwa kulikuwa na siti zingine kadhaa zimelowa. Hii ni aibu kwa basi la kampuni ya Kilimanjaro.

Hii inanitafakarisha, kwa nini kampuni za kitanzania zinashindwa kuendelea baada ya kufika kilele cha mafanikio, zinaporomoka. Hadithi ilikuwa kwa Scandinavia, ikaja kwa Dar es Express na sasa Kilimanjaro Bus linaelekea kulekule.

Ni kuwa tunalewa mafanikio au tunashindwa kuwa na fikra za mbali zaidi?

Ningependa kujua maoni ya wengine, ila kwa sasa, naona nitasimama kwanza kupanda mabasi ya Kilimanjaro, safari za kubahatisha ni hatari.
Scandinavia mabasi yake hayakuchoka, kampuni ilikufa kama binti mrembo
 
Tiketi ulikatia wapi Mkuu ofisini kwao au kwa mpiga debe/dalali? Maana kama ofisini na wakakuambia gari ni luxury na ukalipa nauli ya luxury. Aise ulikosea sana kupakia hilo gari.

Usingepakia kabisa na haya mengine yote usingekutana nayo Mkuu. Ila pole sana
 
Back
Top Bottom