Yaliyonikuta na Basi la Kilimanjaro Express

Karibu KIDIA ONE, njoo uone tofauti, wako on time, hawana mbambamba njiani
Hilo basi liko njema sana nimeshalishuhudia safari za toka Dar kwenda Zoo na Toka Dar kwenda Moshi.

Yote kwa yote tuzidi kumwomba Mungu tukiwa safarini atusaidie tusipatwe na ajali.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
You joined Dec 2022 unakumbukumbu ya zamani ipi hiyo?
Nmsuna hakika kama nimeelewa point yako..ila huku rasmi, ndio nimejoin December, lakini magari ya Kilimanjaro ya mwanzo yenye rangi ya Kijani nilikuwa nayaona Ubungo bus stand tangu wakati nasoma, mwanzoni mwa miaka ya 2000, ndio zamani ninayoizungumzia....
 
Itakuwa vizuri ukituambia ni Bus yenye Reg no ngapi uliyopanda. Ikiwa na Sit mbovu na hiyo iliyokuwa inavuja ili kumsaidia msafiri kuchukua tahadhari na hata mmiliki mwenyewe kufanyia marekebisho...... La sivyo twaweza fikiri una lengo la kuharibu Biashara ya Mtu.
Ticket ni hizi hapa mzee
20230214_011603.jpg
20221206_170426.jpg
 
Yes, wapo..
Wana route za Kaskazini kupitia Bagamoyo au Chalinze...ni wewe utachagua kitu unapenda...

Huduma zao nzuri... Magari ya kutosha..View attachment 2515864
Nimekusifu.

Kweli Jf ni kisima cha maarifa!

Mtu mnapiga stori, unashangaa na picha anakuwekea!

Ninachoshangaa si namna ya kuweka picha, isipokuwa namna mtu anavyoweza kuweka ushahidi wowote katika jambo lolote!

Unakuwa unajiuliza, alijiandaaje kwa mazungumzo kama haya ili aje kuweka kielelezo?
 
Kwa tunaosafiri sana kuelekea mikoa ya Kaskazini tunatambua nafasi na heshima ya kampuni ya mabasi ya Kilimanjaro Express, iliyojiwekea kwa kipindi kirefu. Tuliamini ilichukua nafasi ya Dar Express, ikawa hawana mpinzani.

Ila hivi karibuni imekuwa tofauti, nimesikia mara nyingi watu wakisema hawapandi tena mabasi ya Kilimanjaro, ni kama sikuelewa hadi yaliyonisibu jana.

Safari ilianza saa moja na nusu asubuhi, Arusha. "Disappointment" ya kwanza ni kwenye gari tulilokuta stendi, tofauti na matarajio yangu. Tuliambiwa gari ni "luxury", kwa nauli ya 40,000/-. Lakini kitu pekee cha ki-luxury ndani ya basi hilo kilikuwa ni choo, hakuna zaidi.

"Seat covers" chakavu, zulia la chini lilikiwa na vumbi lilitimka kila watu walipopita.

Gari halikuwa na kiyoyozi, hii sikutegemea kabisa, hasa kuwa nilishaandaa koti la kuvaa nikiwa ndani.

Safari iliendelea lakini gari hakikuwa na mwendo wa kuridhisha, na kufika eneo la Makuyuni, Korogwe, likazima kabisa. Muhudumu wa ndani ya gari akatangaza kuomba radhi na kuwa abiria wasubiri kidogo. Hapo abiria wakawa wakali wakihoji sababu ya kusubiri. Hapo ndipo nikajua wengi hawakuwa wameridhika na hali ya basi lile.

Tukateremka, watu wakajitafutia hifadhi kwenye vivuli vichache na wengine kwenda madukani kujitafutia chochote kitu. Baadae sana dereva akatafuta basi dogo la abiria kutuchukua hadi hitelini kwao Korogwe.... hapo sasa tulikaa kuanzia saa saba na nusu mchana hadi saa mbili na nusu usiku tulipopata nafasi kwenye basi jingine la kampuni hiyo hiyo.

Tarehe 8 Desemba, nilipanda tena basi Lao la mchana kuelekea Arusha. Tulipofika kipande cha kuanzia Same hadi Njia Panda kulikuwa na mvua kubwa. Sikutegemea, ila basi lilikuwa linavuja na nililazimika kusimama hadi Moshi, bikapata nafasi ya kukaa baada ya abiria kadhaa kushuka. Hapo nilitambua pia kuwa kulikuwa na siti zingine kadhaa zimelowa. Hii ni aibu kwa basi la kampuni ya Kilimanjaro.

Hii inanitafakarisha, kwa nini kampuni za kitanzania zinashindwa kuendelea baada ya kufika kilele cha mafanikio, zinaporomoka. Hadithi ilikuwa kwa Scandinavia, ikaja kwa Dar es Express na sasa Kilimanjaro Bus linaelekea kulekule.

Ni kuwa tunalewa mafanikio au tunashindwa kuwa na fikra za mbali zaidi?

Ningependa kujua maoni ya wengine, ila kwa sasa, naona nitasimama kwanza kupanda mabasi ya Kilimanjaro, safari za kubahatisha ni hatari.
Panda tirihisho hautojutia mkuu
 
Dar Express imejifia kabisa basi mbovu hazina mfano, Tangu Mzee Mremi Akabidhi watoto kampuni hata makondakta wamekua madume wachafu huduma mbovu, Shida unakua mmiliki afu tena wewe wewe ndio manager wewe ndio fundi, Waajiri watu wawafanyie kazi kwa weledi waache ubabaishaji
 
Kwa tunaosafiri sana kuelekea mikoa ya Kaskazini tunatambua nafasi na heshima ya kampuni ya mabasi ya Kilimanjaro Express, iliyojiwekea kwa kipindi kirefu. Tuliamini ilichukua nafasi ya Dar Express, ikawa hawana mpinzani.

Ila hivi karibuni imekuwa tofauti, nimesikia mara nyingi watu wakisema hawapandi tena mabasi ya Kilimanjaro, ni kama sikuelewa hadi yaliyonisibu jana.

Safari ilianza saa moja na nusu asubuhi, Arusha. "Disappointment" ya kwanza ni kwenye gari tulilokuta stendi, tofauti na matarajio yangu. Tuliambiwa gari ni "luxury", kwa nauli ya 40,000/-. Lakini kitu pekee cha ki-luxury ndani ya basi hilo kilikuwa ni choo, hakuna zaidi.

"Seat covers" chakavu, zulia la chini lilikiwa na vumbi lilitimka kila watu walipopita.

Gari halikuwa na kiyoyozi, hii sikutegemea kabisa, hasa kuwa nilishaandaa koti la kuvaa nikiwa ndani.

Safari iliendelea lakini gari hakikuwa na mwendo wa kuridhisha, na kufika eneo la Makuyuni, Korogwe, likazima kabisa. Muhudumu wa ndani ya gari akatangaza kuomba radhi na kuwa abiria wasubiri kidogo. Hapo abiria wakawa wakali wakihoji sababu ya kusubiri. Hapo ndipo nikajua wengi hawakuwa wameridhika na hali ya basi lile.

Tukateremka, watu wakajitafutia hifadhi kwenye vivuli vichache na wengine kwenda madukani kujitafutia chochote kitu. Baadae sana dereva akatafuta basi dogo la abiria kutuchukua hadi hitelini kwao Korogwe.... hapo sasa tulikaa kuanzia saa saba na nusu mchana hadi saa mbili na nusu usiku tulipopata nafasi kwenye basi jingine la kampuni hiyo hiyo.

Tarehe 8 Desemba, nilipanda tena basi Lao la mchana kuelekea Arusha. Tulipofika kipande cha kuanzia Same hadi Njia Panda kulikuwa na mvua kubwa. Sikutegemea, ila basi lilikuwa linavuja na nililazimika kusimama hadi Moshi, bikapata nafasi ya kukaa baada ya abiria kadhaa kushuka. Hapo nilitambua pia kuwa kulikuwa na siti zingine kadhaa zimelowa. Hii ni aibu kwa basi la kampuni ya Kilimanjaro.

Hii inanitafakarisha, kwa nini kampuni za kitanzania zinashindwa kuendelea baada ya kufika kilele cha mafanikio, zinaporomoka. Hadithi ilikuwa kwa Scandinavia, ikaja kwa Dar es Express na sasa Kilimanjaro Bus linaelekea kulekule.

Ni kuwa tunalewa mafanikio au tunashindwa kuwa na fikra za mbali zaidi?

Ningependa kujua maoni ya wengine, ila kwa sasa, naona nitasimama kwanza kupanda mabasi ya Kilimanjaro, safari za kubahatisha ni hatari.
Embu njoo BM Coach wewe uone mambo,,jana saa saba na dk 49 chuma kutoka dar imenishusha mianzini arusha.
 
Back
Top Bottom