Yaliyonikuta na Basi la Kilimanjaro Express

Yaliyonikuta na Basi la Kilimanjaro Express

Tarehe 8 Desemba, nilipanda tena basi Lao la mchana kuelekea Arusha. Tulipofika kipande cha kuanzia Same hadi Njia Panda kulikuwa na mvua kubwa.

Huwa tunapotea njia wakati wa kwenda, sasa wewe ulipoteaje njia hiyohiyo wakati wa kurudi
Safari ilianza saa moja na nusu asubuhi, Arusha. "Disappointment" ya kwanza ni kwenye gari tulilokuta stendi, tofauti na matarajio yangu. Tuliambiwa gari ni "luxury", kwa nauli ya 40,000/-. Lakini kitu pekee cha ki-luxury ndani ya basi hilo kilikuwa ni choo, hakuna zaidi.
Kimsingi hakuna luxury bus Tanzania
 
Okay!...sijawahi kulisikia kusema kweli....wapo route hizi hizi za kaskazini ?
Yes, wapo..
Wana route za Kaskazini kupitia Bagamoyo au Chalinze...ni wewe utachagua kitu unapenda...

Huduma zao nzuri... Magari ya kutosha..
Screenshot_20230213_121735_Instagram.jpg
 
Itakuwa vizuri ukituambia ni Bus yenye Reg no ngapi uliyopanda. Ikiwa na Sit mbovu na hiyo iliyokuwa inavuja ili kumsaidia msafiri kuchukua tahadhari na hata mmiliki mwenyewe kufanyia marekebisho...... La sivyo twaweza fikiri una lengo la kuharibu Biashara ya Mtu.
 
Tanzania Luxury bus almost hakuna mengi ni fix tu,utakuta nje ya bus wameandika free WiFi wakati hata dereva mwenyewe hajui hicho kitu ni kitu gani?
Tz kuna bus za bora kufika nothing special.
Kuna safari nilipanda Upuuzi unaitwa GREEN LINER aiseee zile sio bus ni takatakaaa za chooni kabisaaa... nje wamechora wifi sijui nini yani ndani yamejaaa Kungunii na mendeee nilijuta ile safari siji kusahauuu ni Gari mbayaa mnooo bora upande bajajiii aisee sio ule uchafu.
 
Kwangu Mimi kupanda Basi lenye choo ndani ni
1. Unatembea na uchafu
2. Ni ushamba
3. Choo sio luxury

Najua nauli n 35,000 Ila mie KiukweliBora nipande saibaba au harambee naul 15,000 tuu na njian nakuwa huru kabisa sasa Ile balance iliobaki nikifika nnapoenda ndio huifanyia malipizi na moyo unakuwa safiii
 
Kwangu Mimi kupanda Basi lenye choo ndani ni
1. Unatembea na uchafu
2. Ni ushamba
3. Choo sio luxury

Najua nauli n 35,000 Ila mie KiukweliBora nipande saibaba au harambee naul 15,000 tuu na njian nakuwa huru kabisa sasa Ile balance iliobaki nikifika nnapoenda ndio huifanyia malipizi na moyo unakuwa safiii
Unatembea na uchafu! Ooh! Ndiyo sababu utembeapo nzi wa kijani hukufuata mgongoni!
 
Tanzania hakuna Luxury bus kuna ordinary tu. hata ile kuandika Luxury bus ule ni utapeli.

Wanafanya utapeli na wanaachwa kila siku.
Scandinavia walikua wanajitahidi hawa wengine
wote ni ujanja ujanja tu.
Wanatumia bus za kichina kwanza haziko comfortable ikiwa speed kidogo kama inasukumwa na upepo.

Bus za kichina ni takataka.
 
BM ndo basi kwa sasa ambalo nalo baada ya miaka 7 litakuwa sio basi la kupanda.

Biashara hufa maana katika kilele cha mafanikio hawa matajiri ufungua miradi mingine na kukopa sana.

Kitendo cha kukopesheka sio sababu ya kukopa bila mipango, hapa ndo wanaharibu, Kilimanjaro ishakufa.
Uzi ufungwe. Wewe ndo umetoa sababu ya kitaalamu ambayo haitajwi sana. Mikopo ndo inatumaliza kwa kweli.
 
Back
Top Bottom