KERO Mabasi ya kichina ni matakataka. Sijui TBS iko wapi

KERO Mabasi ya kichina ni matakataka. Sijui TBS iko wapi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

bikira latifah

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2016
Posts
836
Reaction score
2,805
Kama una Bawasili sugu au Uti wa mgongo haupo sawa basi achana na safari za mabasi ya kichina na ukikuta siti za nyuma kata for your own risk

Nipo kwenye bus siti ya nyuma limepita kwenye tuta tu nimerushwa hadi kichwa kimedunda kwenye roof na nundu juu

Mabasi ya kichina hayapo comfortable kabisa hasa linapokuja swala la matuta au mashimo, ukikaa nyuma kule yanaweza kukuua. Hapa nasafiri na toleo lao jipya d14 Yutong ila ni hovyo kabisa. Seat ya nyuma likikanyaga tuta unarushwa juu, si hatari hii?

Hapa ndani kulikuwa na kampuni ya Dar Coach, walikuwa wanajitahidi mlikubaligi vipi kuruhusu hizi takataka hadi kile kiwanda kikafa?

Mabasi ya kichina yachunguzwe ubora wake yatakuja kuua. Mtu ukitaka panda gari kama Tahmeed, Katarama, Kilimanjaro zile scania huwezi kuta unaumia gari ikipita kwenye tuta hata zile Bus za Dar coach made in Tz walikuwa wanajitahidi.

Basi za mchina zimejazwa urembo tu ila yale ni matakataka siti za nyuma ni risk mimba inaweza chomoka
 
Back
Top Bottom