Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,813
- 11,991
Mbunge Ndugulile amejibu kwa kuandika kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa “Nawashukuru sana JamiiForums kwa taarifa hii. Tumeipokea. Naahidi suala hili kufanyiwa kazi kwa haraka. Lengo letu ni wananchi kupata huduma nzuri na kwenye mazingira safi na salama.”
Mudu mfupi baadaye Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu naye akajibu Katika post hiyohiyo “Huu ndio uwajibikaji tunaoutaka. Asante sana Dr Faustine. Ukweli changamoto nyingi za wananchi kuhusu utoaji wa huduma za Afya nchini hazihitaji hadi Waziri wa Afya aseme. Endapo viongozi wengi tunafuatilia kwa karibu utoaji huduma za afya ktk maeneo yetu basi ni dhahiri kuwa lengo la Serikali la kuwafikia wananchi na huduma bora za afya tunaweza kulifikia hata kabla ya 2030. Hongera sana Dr. Ndugulile. Wana Kigamboni wamepata Mbunge makini👍. Kazi Iendelee."
Hoja ya Mdau ni hii hapa = Vyoo vya Hospitali ya Vijibweni Kigamboni ni vichafu na vimechoka kuliko maelezo