Feisal Salumu: Nimeondoka Yanga kutokana na manyanyaso, nilizungumza na Rais wa Yanga kwa saa 6, nikamwambia nataka kuondoka

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,203
12,720
1685608021302.png

"niliambiwa na viongozi wa Yanga kuwa nauza mechi iliniuma sana na nikipokuwa nawapigia simu hao viongozi waliokuwa wanatamka hayo maneno hawapokei simu yangu.

"Viongozi walikua wanamtukana mama yangu na kutoa matusi ya kumnyanyasa hata ingekua ni wewe ndugu mwandishi usingekubali kutukaniwa mzazi"

"Kula ugali kwa sukari sikula saivi nilikula kipindi kile timu bado ilikua ipo chini kiuchumi na kuna muda tulicheleweshewa mishahara lakini Mama aliniambia vumilia mwanangu maana alikua ni mpenzi wa mkubwa wa Yanga.

"Mama kuna muda mwingine alinipa pesa yake tulipokua tumecheleweshewa mshahara."

Mwandishi: Tueleze umepitia manyanyaso gani?

"Naambiwa nauza mechi, viongozi wananitukana na nikiwaambia familia wanasema nivumilie.

"Mama yangu alikuja Dar wakamtukana na kuanza kumpa maneno ya kejeli."

"Huyo huyo Raisi anatuma watu wamtukane mama yangu wanamuita mama yangu andazi "

Wanitukane Mimi lakini siyo mama yangu maana mama yangu ni pepo yangu"

"Nimekaa masaa sita na Engineer Hersi kuwa hapa nilipofikia nataka niachane na Yanga na Hers alisema kuwa bado anahitaji huduma yangu"

Raisi: anampigia simu mama na mama aliniambia niende kusaini mkataba na mama alimwambia mpe Fei mkataba wa miaka miwili"

Hers aliongeza mwaka mmoja badala ya miaka miwili"

"Mimi sijui kiingereza walinipa mkataba wa miaka mitatu"

"Signing fee sijapewa kwa wakati nilipewa kidogo kidogo tena kwa kutumiana meseji za vitisho"

"Nataka kukusanya milioni 60 niende CAS na watanzania wengi wananichangia na utaratibu umeanza tunasubiri invoice"

"Unajua yanga ni taasisi kubwa na Mimi ninawapenda wanayanga nilimwambia hers ata Kama alinikosea Ila nilimwambia tukae chini tumalizane na hers alikili makosa yake lakini Mimi nilitaka tuachane nikatafute maisha sehemu nyingine"

"Nilimwambia eng Hers bmkubwa alikuambia Miaka miwili lakini ukanipa mitatu lakini hers hakunijibu"

"Familia yangu wanaipenda Yanga lakini kilichonitoa Yanga ni manyanyaso"

"Hakuna timu inayonitaka na ndiyo maana nilitaka kuvunja mkataba niende kutafuta maisha yangu pengine"

"Tumekaa na familia yangu niliona Bora tuvunje mkataba na niliwaomba viongozi tuachane nilichangiwa pesa na familia"

"Mimi siwezi kula dhuluma siwezi kula pesa ambayo siifanyii kazi na ndiyo maana wakituma pesa zinarudi"

"Mimi sipendi hizi kelele nataka hili Jambo liishe na nafsi yangu haitaki kucheza Yanga na ndiyo maana nilikaa nao chini viongozi chini tuyamalize nikatafute maisha sehemu nyingine"

",Kama Jambo litakua haliishi ni bora nikae nyumbani maana ndiyo mwenyezimung atakua amepanga hivyo" kipaji kuisha.

"Hers anasema nauza mechi kun pass moja nilimpa Mayele aongeze magoli mbele ya kipa lakini Mayele alikosa hapo Hers akaanza kusema kuwa nauza mechi"

"Nilimtafuta GSM aje kutafuta suluhu lakini hakupokea simu zangu lakini aliposikia sakata Hili ndiyo akaanza kunitafuta na Mimi sikupokea simu yake"

"Nilikutana Hers akasema kuwa anataka nirudi Yanga nilikataa basi akaniambia niende CAS"

"Hers anadharau kubwa sana na Msolwa alikua ni mkarimu sana"

"Watu hawajiulizi ni kwa nini Fei hajaondoka katika kipindi kile Cha Yanga ngumu lakini nimeondoka kipindi hiki kizuri".

"Mimi nina matatizo na Raisi wa club Sina Tatizo na club Ila hers ndiyo Raisi wa club ndiyo Nina tatizo nae"

"Mpaka Sasa hela haijatosha Ila nashukuru Watanzania wameshanichangia kiasi cha shilingi milioni tisa (9)

"Mimi Nina rafiki na ndugu na wengine wapo humo humo ndani ya klabu ya yanga ndiyo walinichangia kurudisha pesa ili nivunje mkataba."

"Naitakia kila la heri Yanga katika fainali yake huko Algeria na nitaiombea Dua mungu ifanye vizuri"

"Mimi nimeongea yote lakini nafsi yangu haitaki kurudi kabisa Yanga sc"
 
"Baada ya kuwasumbua sana ndio wakaniongezea Million 20 zingine baaae."

Mazungumzo yalikua nilipwe signing fees million 100 Kwa mkupuo, baada ya kusaini wananiambia kua mkataba unasema nitalipwa Kwa mafungu. Mkataba ni wa Kingereza na mi sikijui".
 
Nipo upande wake lakini hapo kwenye kutokujua mkataba unasemaje sababu ni wa kingeleza namlaumu. Kwanini asaini dili kubwa kama hii bila kuwa na mtalamu wa hata mambo
Walishaongea kabla ya kusaini mkataba kwanza, kwahivyo yale mazungumzo Faisal ndo akayapeleka kwenye mkataba ambapo baadaye yaliyotokea ni kwa Hersi miaka mitatu na kwa Feisal ni miaka miwili.

Alikariri mazungumzo waliongea kabla ya kusaini mkataba wa Kingereza.
 
Back
Top Bottom