Yaliyojiri wakati wa ukarabati wa JF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yaliyojiri wakati wa ukarabati wa JF

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by ZeMarcopolo, May 31, 2009.

 1. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Imeripotiwa kuwa wanachama mbalimbali ambao Dr.JF amewadaiagnoz na ugonjwa wa adikshen ya JF walikuwa katika wakati mgumu wikiend hii wakitafuta shughuli mbadala nje ya JF, pale ambapo JF haikuwa richabo kwa ajili ya matengenezo.

  Mitaa ya mbagala inaripotiwa kuwa Yo-Yo alionekana akifanya mazoezi ya kukimbia au kwa jina la kitalaam jogging.
  Taarifa toka vingunguti zinasema kuwa watoto wa BabaDesi wamegundua kwa mara ya kwanza kuwa baba yao ana pengo. Inasemekana watoto hao walikuwa hawajawahi kumuona baba yao akicheka pembeni ya kioo cha kompyuta.

  Masanilo alionekana mitaa ya fukwe Fulani akirandaranda na kamera mkononi, hata hivyo juhudu za kumpata ili kutoa ufafanuzi wa alichokuwa akifanya hazikufanikiwa kutoaka na simu yake kutopatikana.

  Naye Kibunango alionekana akisimamia ufuaji wa suruali aina ya jinsi ambayo inasemekana ilikuwa imesimama dede, hata hivyo haikuweza kufahamika jinsi hiyo ilikuwa mali ya nani.

  Mahakama ya akimu mkazi kisutu imethibitisha kupokea shitaka toka kwa Mzee Mwanakijiji (MM) akiishitaki kamati ya ukarabati ya JF kwa kuchelewa siku aliyoapanga kutimiza posts elfu 15. Mwanakijiji ambaye alitarajiwa kutimiza post hizo 15,000 kabla ya mwezi Mei mwaka huu sasa anakadiriwa kufanya hivyo mwanzoni mwa mwezi Juni. Ripota wetu anampongeza MM in advansi kwa kutimiza post elfu 15.

  Kutoka Dodoma, JF ripota anatuletea taarifa kuwa Mbunge na Mwana JF Zitto Kabwe ameandika karatasi nyingi za yale aliyodhamiria kuyapost JF kipindi hiki cha wikiend ili aweze kuzipost mara tu JF itakaporudi hewani. Akitoa makadirio ya idadi ya karatasi hizo ripota wetu anasema wingi wake umezidi kidogo zile alizoshika mh. Rais JK wakati akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Marekani BO.

  Ripota wetu toka Dodoma pia anatuletea taarifa kuwa mbunge wa Igunga mh. RA amejing’ata mara chache zaidi tangu mwaka huu uanze. Watu wa Tabora huamini kuwa mtu akitajwa bila yeye kuwepo huwa anajing’ata.Aliposikia kuwa JF imefungwa kwa matengenezo ilimiwia bayana ni kwanini kipindi hiki cha wikiend hakujing’ata sana.

  Naye Gembe alionekana kwenye satelaiti akiwa huko bondeni kwa Zuma ameshika kopi ya gazeti la Mwananchi, kalamu na karatasi katika kioski cha kuuza nyama ya kuku wa kukaanga toka Kentuky(KFC).Juhudi za kuthibitisha kama anaandaa makala kwa ajili ya gazeti hilo au lah bado zinaendelea.

  Naye Kitila Mkumbo aloulizwa hisia zake juu ya kusimamishwa kwa muda kwa JF alisema ‘’I miss DARUSO’’ bila kutoa ufafanuzi zaidi.

  Naye FMES a.k.a mzee wa inside stories anatuletea taarifa kuwa kikao cha usalama yaani sekyurite brifing cha jumatatu kimeahirishwa kutokana na katibu wa kikao hicho kukosa desa toka JF. Habari toka hukohuko ikulu pia zinaelezea kijana msaidizi wa rais amesikitishwa na kukatishwa kwa mjadala ulioanzishwa na mwanaharakati mwanadada katika mazingira maalum kwa sababu zinazoaminika kuwa maalum. Kijana huyo alionekana akiongea kwa simu kwa muda usiopungua masaa sita! Jitihada za kupata maoni ya Kelly juu ya hili hazikufanikiwa baada ya simu yake kuwa bize kila alipopigiwa.

  Inaaminika kuwa Mama amefanya overtime ya masaa 15 kipindi hiki cha wikiend ili kujikip bize.Aliyetuletea habari hizi pia alitiarifu kuwa Mkamap alionekana katika viwanja Fulani akiwa amevaa bukta na nyumu kuashiria kuwa alikuwa tayari kwa mpira wa mguu.

  Kutoka majuu tumeletewa habari kuwa Nyani Ngabu(NN) amedhihirisha kunufaika na ban ya mwezi mmoja aliyopewa kwa kuwa hakuonekana kuathiriwa na kusimamishwa kwa huduma za JF.Hali ilifanya ripota wetu kushauri ban ziwe zinatolewa kwa rotesheni ili memba waweze kuadapt maisha mengine.Alipouliza maoni yake juu ya memba wengine kuathirika na kutokuwepo kwa huduma ya JF NyaniNgabu alisema ‘’miafrika ndivyo tulivyo’’.

  Mitaa ya Upanga jijini Dizim kulikuwa na kasheshe pale mzee wa ‘’embe lililoivia mtini’’ alipobaini kuwa kijana wake amekuwa na mwamko tofauti kisera tangu alipojiunga JF. Mzee huyo ambaye hukosa muda wa kuongea na mwanae kutokana na mwanae kuwa bize na JF alisema anataka kuitisha kikao cha familia kupiga marufuku matumizi ya JF kwa wanae wote. Kisa kizima kilianze pale mzee huyo alipokuwa akisimulia yale yaliyojiri toka kwenye kampeni huko Busanda, ambazo alipewa jukumu ya kuziongoza kwa upande wa sisiemu. Mara ikasikika kijana ambaye ni memba mpya wa JF ‘’kwa jina lake’’ akitumia lugha ya ‘’kipinzani’’ ikiwa ni pamoja na kuwaita baadhi ya viongozi mafisadi. Mzee alishangaa kuona kijana ambaye alikuwa na misimamo inayoendana kabisa na yeye kubadilika ghafla.Baadae ilibainika kuwa JF imem revolutionalaizi kijana huyo. Hata hivyo habari ambazo bado hazijathibitishwa zinasema kuwa kijana huyo ni memba wa muda mrefu wa JF ila alikuwa anatumia jina tofauti.

  Invisible alipotafutwa kutoa taarifa ya jinsi ya kuwareskyu wana JF hawa ili waendelee kuishi maisha ‘’ya kawaida’’ hakuweza kupatikana. Hata hivyo jirani yake invisible alishauri wana JF washiriki zaidi kwenye kutoa michango ya risosi ili JF iwe na weki fosi ya kutosha na kuweza kuwa na ukarabati wa mara kwa mara kwa muda mfupi.ushauri huo wa jirani ulimkumusha ripota wetu ujumbe wa kibunango – Changia JF mkono mtupu haulambwi!

  Muda mfupi kabla ya kuchapa habari tulipata taarifa kuwa Blueray,Saikosis,Masaka, Bubu ataka kusema na Ab-tichaz wamepata nevasi brekidawni kwa kukosa huduma ya JF na wanapewa msaada wa kitaalamu katika hospitali ya mwananyamala.

  Jitihada za kujua jinsi wana JF wengine walivyoathirika na kukosa huduma kipindi cha wikiend zinaendelea.Hivi sasa ripota wetu yuko katika mahojiano na Rev. Kishoka ambaye alikuwa kwenye sala maalum kuiombea JF irudi hewani mapema, kwa sababu wanaoathirika sio membaz peke yao bali hata wale ‘’only vyuaz’’.
   
 2. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2009
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  This is cool.

  Ubunifu wa hali ya juu sana.

  Congs man!
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kwa kweli nimekukubali....
   
 4. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Yah! Kweli this is Babkubwa
   
 5. O

  Ogah JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  You made my day Zemar........kwi kwi kwi kwi kwi
   
 6. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  ZeMarcopolo,

  Makala safi sana ila mleta ujumbe huo hakuwa Kibunango. Kibunango anasema "Save Water Drink Beer. "Alcohol doesn't solve any problems,
  But, if you think again, neither does milk."
   
 7. Z

  Zero One Two JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2009
  Joined: Sep 16, 2007
  Messages: 9,390
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Hawa waliotajwa hapa ndio viongozi wa JF? Wanafaa kuwa viongozi wa Taifa la Tanzania lenye neema na maisha bora kwa kila Mtanzania? Utafiti utaendela juu yao.

  Asante.
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,443
  Likes Received: 81,492
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha ha ha BAK aliambiwa alazwe kwa siku mbili ili afanyiwe uchunguzi zaidi lakini alipewa tandiko kwenye sakafu ambalo alitakiwa ashee na wagonjwa wengine sita. :)

  Lakini baada ya kupata simu toka kwa Mbu kwamba JF imerudi hewani, BAK aliwaambia madaktari kwamba yeye yuko fit kabisa na alikuwa hana tatizo lolote kiafya. Alionekana akichukua Tax na kumuomba tax driver amshushe kwenye internet cafe iliyo jirani ili akasome yaliyojiri JF wakati ilipokuwa haiko hewani.
   
 9. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #9
  May 31, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Inafurahisha kwa kweli!
   
 10. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #10
  May 31, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  JF imekuwa inatufanya tukose vingi.....wengi wanaokaaa masaa mengi jf hawana mashori wakali...fanyeni tafiti....
   
 11. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #11
  May 31, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Bangi hizo!
   
 12. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #12
  May 31, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Aisee hii inawezekana ila kuna point fulani katika graf zitakuwa ziko nje ya mean data value maana taarifa nilizonazo ni kwamba shori wa Mkandara aliwahi kushinda miss Tanzania mwaka fulani.
  Unasemaje kuhusu kina WomenofSubstance nao, je wanao mahandsome boy?
   
 13. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #13
  May 31, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Hahahahahahah kwikwikwikwikwi teh teh teh... aisee hii ya kigodoro imenivunja mbavu kwelikweli.Naaona hapo meseji imekuwa sent kwa staili ya ki-joke joke, haya Mwananyamala hospital fanyieni kazi ujumbe huo.
   
 14. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #14
  May 31, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Naona hapo mwandishi alichanganya majina kidogo na alikosi JF kwa riferensi!
   
 15. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #15
  May 31, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  This is unacceptable Mkuu!
  Dont cross the line kwenye utani.
   
 16. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #16
  May 31, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  My bad, sorry WoS.
   
 17. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #17
  May 31, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  hawakujui hawa vijana....

  kwikwikwikwikwi ungeshitakiwa sasa hivi....
   
 18. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #18
  May 31, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  nakuomba usisemee ubaya hilo jani....
   
 19. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #19
  May 31, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Mmmh Yo-Yo yamekuwa hayo ndugu yangu!?
   
 20. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #20
  May 31, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  kama huamini utani kwa TGNP na ile dini ya wanyenyekevu usijaribu kabisa....
   
Loading...