Tiba za nyumbani: Matatizo ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula

Surveyor_1

Member
Jan 2, 2022
48
29
Habari za asubuhi wana JF,

Leo nimependelea kushare nanyi baadhi ya tiba za nyumbani za matatizo ya mfumo wa umeng'enyaji chakula ambazo zinaweza kutumika kama huduma ya kwanza au tiba ya kuponya kabisa katika mazingira yetu ya nyumbani.

Sitojikita kuelezea magonjwa kwa ajili ya kutorefusha mada, lakini pia kwa kutarajia kuwa yameelezewa sehemu nyingi humu JF na nje ya hapa.

Bali nitakuwa nikiyaelezea kwa ufupi pale penye ulazima na kwenda moja Kwa moja kwenye kuelezea matibabu yake.
 
#1. KUKOSA CHOO (CONSTIPATION)

Hali ya kupata choo mara chache au kupata choo kigumu, au ugumu wa kupitisha choo.

VISABABISHI

Kukosa choo kunatokana na sababu tofauti tofauti ikiwemo :

- Lishe yenye upungufu mkubwa wa nyuzi nyuzi (fibers)

- Unywaji mdogo wa maji.

- Matumizi ya baadhi ya dawa mf. Antibiotics

- Huzuni na msongo wa mawazo.

- Ujauzito kutokana na mabadiliko ya homoni.

- Mwili kukaa muda mrefu bila kujongea

- Bawasiri.

- Na nyinginezo.

Pale sababu ya tatizo inapojulikana inatakiwa itibiwe.

TIBA

(i) ULAJI wa matunda na mboga za majani kwa wingi pamoja na kupunguza ulaji wa nyama na ngano iliyokobolewa.

(ii) KUNYWA maji kwa wingi.

(iii) UWATU (FENUGREEK)
Matumizi ni kijiko cha chai 1-2 mara 2-3 kwa siku kwenye maji vuguvugu
  • Upo wa unga na WA mbegu, wa unga ni rahisi zaidi kwa matumizi
  • Unapatikana kwenye maduka ya viungo na ya dawa za asili.

ANGALIZO : Haitakiwi kutumika na mjamzito.

- Jitahidi kunywa maji kwa wingi unapotumia uwatu kwa kuwa una kawaida ya kunyonya maji kwa wingi ili kusaidia mjongeo katika mfumo wa chakula.


(iv) UKWAJU (TAMARIND)

Matumizi : Unaweza kutumia kama juisi kwa kadiri ya mahitaji

ANGALIZO : Tumia kiasi, matumizi yaliyopitiliza huweza kuchochea kiungulia/acid reflux


TIBA zifuatazo zinatakiwa kutumika kama chaguo la mwisho kwa tatizo sugu na kwa muda mfupi kwa kuwa huwa zina nguvu sana na zinaweza kusababisha matatizo ya kiafya kama zikitumika kwa muda mrefu.

(v) MAFUTA YA NYONYO (CASTOR OIL)
Matumizi ni 5ml mara 2-3 kwa siku.

USITUMIE zaidi ya siku 8.

ANGALIZO : Haitakiwi kutumika na mjamzito.

(vi) SANA MAKKI (SENNA)
Matumizi : Kutegemeana na maelekezo ya daktari/tabibu wako.

ANGALIZO : Usitumie zaidi ya wiki moja.


• WADAU WOTE MCHANGO WENU NI WENYE KUHITAJIKA.
• MWENYE NYONGEZA, MAREKEBISHO KARIBU SANA.
 
Mtanisamehe Wana JF ntakapochelewa kupost, ni kutokana na muingiliano wa majukumu mengine.

Nitakuwa nashare Kwa uchache post za tiba za ugonjwa mmoja kila siku 1-3.

Yeyote mwenye maarifa juu ya mada iliyopo mezani anakaribishwa pia.
 
Mtanisamehe Wana JF ntakapochelewa kupost, ni kutokana na muingiliano wa majukumu mengine.

Nitakuwa nashare Kwa uchache post za tiba za ugonjwa mmoja kila siku 1-3.

Yeyote mwenye maarifa juu ya mada iliyopo mezani anakaribishwa pia.
Sawa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom