Yaliyojiri: Mkutano wa Dr.Slaa Kyela

Yaliyojiri: Mkutano wa Dr.Slaa Kyela

Dr Slaa anakadi ya CCM,

Mbowe kala hela za CCM,Mkono na Rostam,

Ila Zitto akihusishwa na CCM anaonekana msaliti na mhaini!!

He! kumbe na walio kuzimu mnaruhusiwa kuchangia JF?
 
MAADILI NI NGUZO MHIMU YA UONGOZI.

Kumekwepo na jitihada ama za makusudi, ama za kutokujua, ama za kile kinachoitwa kumsafisha mbowe.

Niweke wazi kwamba sikumkosoa mbowe kuhusu mambo ya mahusiano anayosemekana kuwa nayo na wabunge wake wa viti maalumu, bali ni kuhusu KUKIUKA KWAKE MAADILI YA UONGOZI.

1) Kitendo cha kukatisha ziara ya mbunge wake wa kazi maalumu ili wakakutane Dubai kwa kazi maalumu badala ya kazi ya nchi aliyotumwa tena arudi toka marekani mpk Dubai kwa fedha za serikali ni matumizi mabaya ya fedha za umma na ni ukosefu wa maadili ya uongozi. Angemrudisha kwa gharama zake yaani kwa fedha zake hapo ingekuwa mambo binafsi. Kufanya mambo binafsi kwa fedha ya umma haiwezi ikawa jambo binfsi. Hivyo sikukosoa mapenzi yao bali matumizi ya kodi za masikini kwa mambo binafsi.

2) Kumlazimisha Afisa wa bunge abadili tiketi ileile iliyokuwa aende kwenye shughuli ya bunge sasa ageuze aende kwenye kazi maalumu hili sio jambo binafsi ni matumizi mabaya ya madaraka. Ni kukosa huruma kwa hali ya juu kwa watanzania.

3) Kumlazimisha mbunge wake wa kazi maalumu kuachana na safari ya kikazi na kuacha nchi ikose mwakilishi kwenye kikao hicho huku tayari akuwa ameshagharamiwa safari hiyo, huku tayari akiwa ameshaziba fursa hiyo ambaye mbunge mwingine angeweza kwenda kuliwakilisha taifa halafu mbowe na mtu wake wakaenda kwenye kipaombele chake cha kuburudika dubai ni ukosefu wa uzalendo kwa Taifa na ni ukosefu wa maadili ya kiuongozi.
Tumeongea kwakuwa wametumia fedha za umma, tumesema kwa sababu wameacha kazi ya umma huku wakiwa wamechukua fedha kwa ajili ya kwenda kuiwakilisha Tanzania na tunasema kwakuwa wamewanyima fursa wabunge wengene ambao wangekwenda kuwakilisha Taifa endapo fursa hiyo hangepewa mtu elibadilishiwa safari ya ya taifa na kuitwa kwa kazi maalumu.

"Ukipewa kazi ya nchi lazima ujiheshimu" NITASHANGAA SANA NITAKAPORUDI BUNGE LIJALO NIKIKUTA MBOWE BADO NI KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI

Ni vizuri ukatuwekea risiti za ticket,boarding pass na maneno yalioandikwa kwenye text nama ya nymbay Dubai na video ya watu wakifanya mapezni hapo tutakuwa na mjadala lakini sio maneno maneno tuu ya kupatia book 7 wewe mwenewe umelelewa na baba wa kambo mbona h uuulizi baba yako mkinga yuko wapi madili unyaoona kwa wengine nemuliz mama yako kwanza
 
Slaa 2015 Ikulu
sio rahisi kama kumsukuma mrevi vile,sio rahisi kama tunavyochapa maandishi ktk simu zetu ama komputa zetu,sio rahisi kama kurusha chopa angani.
kuingia ikulu sio rahisi kama kuingia msalani ukiwa umebanwa na haja.kuingia ikulu sio rahisi kama kumnywesha mgonjwa uji.
Ni lazima kuiombea ccm njaa ili cdm ipate nafasi ya kuingia ikulu,ni lazima kuiombea ccm isimamishe mtu asiyekubalika ktk jamii ndio cdm itaingia ikulu,ni lazima tuiombee ccm isambaratike ndipo nafasi ipatikane.
Lakini kama ccm itaendelea kuwa imala na kumsimamisha mgombea atakayeungwa mkno na kila mtu na cc ya chama hizi ndoto za kwenda ikulu msiwe nazo kabisa,ingawaje mnaweza ongeza nafasi za udiwani ama kupunguza lakini si kwenda ikulu 2015

Nasema hivi
ili vyama vya upinzani viweze kushika dola ni lazima ccm ibomoke vipande vipande,la sivyo haiwezekani.
 
Na mimi nimeumia, kumbe CHADEMA wanafanya maamuzi huku wanaumia lakini wanaendelea kuyafanya. Hawa watu wanatufaa hawa.

Endelea kusikitika pole hamjiamini tena baada ya CCM kuwa mapande mapande mara Nape anasema yake ,Kinana yake,Lugola yake Sitta yake Lowassa ndio kabisa chama limemeguka linazikwa likiwa limeshakatika mapande
 
tutaendelea kupambana na wasaliti mpaka tuwamalize kabisa bila woga tumepambana na chama chetu miaka 22 ilopita halafu ukiharibu hatutakubali tena akina zito na masalia menzake.
 
vipi yule anayeenda kuvinjari na mahawara huko dubai huku wamechukua posho za bunge na yule aliyepora mke wa mtu

Inaelekea huna taarifa ya maelezo ya ufafanuzi yaliyotolewa na katibu wa Bunge Mh. Kashilila juu ya safari hiyo ya Mbowe, usingekuja tena hapa na hiyo hoja.
 
Ulitaka azae na dada yako. Au mama Mbowe kalalamika. Walitaka mtoto wanaye kaongeza familia linakuuma nini
 
Hayo aliyotaja slaa yote yeye ndiye mhusika mkuu wala asimrushie mtu mwingine.
 
Nadhani huwajui wazinzi mmojawapo yupo magogoni pale ana watoto kila aina ya ukoo

teh teh teh teh.......watu mumejipindia munatoa tu yaliyo moyoni,naamini amekusoma na hatarudia.
 
CCM waingiwa hofu



CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza msimamo mzito kwamba endapo vijana milioni tano wasipoandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kitasusia kura za maoni ya Katiba.

Msimamo huo ambao mara ya kwanza ulitangazwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, ulitangazwa rasmi tena jana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa michezo wa Shule ya Msingi Matarawe mjini Songea jana, Dk. Slaa alisema CHADEMA imekuwa ikipigia kelele suala hilo kwa muda mrefu, lakini Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imepuuza kwa madai kuwa haina pesa za kuandikisha wapiga kura hao.

Aliitaka serikali kuhakikisha inawaandikisha watu wote 5,300,000 ambao hawakuandikishwa kwenye daftari hilo baada ya kupoteza shahada zao kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo baadhi yao kuziuza wakati wa uchaguzi mkuu, kubadilishana na mbolea na baadhi ya vijana wengi waliofikisha umri wa miaka 18 kutoandikishwa katika daftari hilo.

"Nasema kuwa kama serikali haitakuwa tayari kukubali ushauri huo, basi itambue kwamba tutasusia kupiga kura ya maoni ya Katiba na tutazunguka nchi nzima kuwahamasisha wananchi kususia zoezi hilo kwani suala la katiba si la chama chochote cha siasa bali ni mali ya wananchi, sasa ni kwa nini liendeshwe kisiasa siasa?" alihoji Dk. Slaa.

CCM waingiwa hofu
Katika hatua nyingine, baadhi ya viongozi wa CCM na watendaji wa serikali wameingiwa hofu na hatua ya CHADEMA kuanzisha operesheni hiyo inayojulikana kama M4C Pamoja Daima.

Wakizungumza na Tanzania Daima jana kwa sharti la kutotaka kutajwa majina, viongozi hao walisema kuwa CCM ina wakati mgumu wa kuhakikisha wananchi wanaendelea kukiamini chama hicho.

Alisema kuwa hatua ya CHADEMA kuamua kutumia chopa na kuzunguka maeneo mbalimbali ya nchi, itaendelea kubadilisha upepo wa kisiasa uliojengwa na uongozi wa CCM miezi michache iliyopita.

Kiongozi huyo alisema kuwa CHADEMA inapofanya mikutano yake inawafanya wananchi kuwa na uelewa wa masuala mbalimbali yanayojitokeza nchini na kama itaendesha harakati za kupinga mchakato wa Katiba mpya kama inavyotishia, inaweza kukwamisha kila kitu.

"Hivi sasa kuna suala la Bunge la Katiba ninaamini kuna changamoto itakayojitokeza katika hoja hiyo maana chama hicho kitatoa elimu itakayotumiwa na wananchi kuhoji juu ya suala hilo," alisema.

Alisema kuwa mara zote chama hicho kinapofanya operesheni zake kinachangia wananchi kuwa na uelewa na kuhoji masuala mbalimbali kwa undani tofauti na CCM inapofanya mikutano yake.

"Wananchi wamekabiliwa na mambo mengi na wanakosa sehemu ya kuyawasilisha hivyo kitendo cha CHADEMA kuzunguka na chopa zao kuna mambo yatakayowafanya wananchi wabadilike na kuzidi kuichukia serikali, hasa likiwemo suala la kupanda kwa gharama za umeme ambalo linamsumbua kila mwananchi," alisema.

Kiongozi huyo alisema kuwa iwapo CHADEMA itafanya mikutano katika Jimbo la Kalenga lililokuwa linashikiliwa na CCM, kuna uwezekano wa jimbo hilo kuchukuliwa na chama hicho.

"Kuna kazi huko tuendapo …tuwe tayari kuzomewa na kushambuliwa kwa maneno hasa pale inapotokea hakuna utekelezaji wa masuala ya msingi yanayopaswa kufanywa na serikali," alisema.

Juzi CHADEMA ilianza operesheni mpya inayoongozwa na viongozi wake waandamizi, akiwamo Mwenyekiti, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa, katika mikoa yote ya Tanzania Bara, kwa kutumia helikopta tatu.

Wengine wanaoshiriki operesheni hiyo iliyobatizwa jina la ‘Pamoja Daima', ni wabunge, wakurugenzi wa makao makuu, wajumbe wa Kamati Kuu (CC), viongozi wa kanda, mikoa, wilaya na majimbo yote ya chama.

Mbowe alisema kuwa operesheni hiyo inafanyika katika mikoa, wilaya pamoja na majimbo yote ya uchaguzi ya Tanzania Bara, isipokuwa mikoa ya Lindi na Mtwara.


Chanzo:
Tanzania daima
 
Kwani hata wakisusia shida iko wapi make walitangaza kususia tangu mwanzo wa mchakato mbona wamenywea kwanza chadema ni slaa,mbowe na mtei sasa hawa watu watatu hata wakisusia shida ipo wapi.
 
Wao wasusie hata bunge la katiba sawa tu japo hawawezi kususia bunge kwa vile kunaposho hupewa hivyo hawawezi kuziacha.
 
Kati ya Hawa viongozi wa kisiasa ni nani anaesomesha mwanae kwa shule hizi za kata?
 
CCM inatafuta mchawi kutoka nje ilhali inajiloga yenyewe,kiukweli JK kawapa CDM mtaji mkubwa kwa kurudisha mawaziri mizigo,NAPE na KINANA watasema nini wakirudi kwa wananchi.......ila tusilalamike sana pengine ni mpango wa Mungu ili tukomboke,hongera CDM na operation yenu,kiukweli CCM kuna waka moto japo wanajaribu kuuzima huku nje tusione,ila ni swala la muda tu punde moshi utatanda hewani.
 
Kwani hata wakisusia shida iko wapi make walitangaza kususia tangu mwanzo wa mchakato mbona wamenywea kwanza chadema ni slaa,mbowe na mtei sasa hawa watu watatu hata wakisusia shida ipo wapi.

Yaan ktk watu ambao hawana akil ni ww No 1 kama chadema ni cha mzee mtei na Ccm ni yani? Unalopoka tu, kwahiyo ww unaona sawa kwa hao vijana ambao hawakuingizwa kwenye daftar la kudumu, mbona huna akili ww?
 
Back
Top Bottom