Yaliyojiri Mkutano wa CCM Viwanja vya Jangwani (Dar) Juni 9,2012

ujinga mtupu kwa CCM
wanashindwa kushughulikia matatizo ya wananchi watumia pesa nyingi kuhadaa wananchi
hao waliohudhuria walikuwa na matarijio ya kupewa chakula na nauli.
nashangaa tu anaejiita mwanaCCM bila kujaua wanaowahutubia na kuwahadaa
ndio hao haowanaouza rasilimali zetu kwa wageni huku wakilimiliki majengo na mgarari ya kifahari.
amkeni watanzania mtajikuta mnuzwa ninyi na watoto wenu.

Wauzwe mara ngapi?
 
View attachment 55925ccm imeshindwa kuadress matatizo muhimu badala yake mnatumia kodi zetu kulisha watu ubwabwa hapo jangwani.
Walishaona Thamani yenu ubwawa wewe unataka kipi kingine! Watanzania wengi hatueleweki wala hatuaminiki! leo chadema kesho ccm tatizo kubwa elimu halafu hatujitambui! hatuji matatizo yetu chanzo chake nini na nani kayaleta ndio maana mtu akipewa bakuli la ubwabwa mbichi anakula na kurudisha kadi kesho wakija chadema anarudisha kadi anachukua nyingine!!!
 
ccm imesema wanaongelea matatizo yanayowasumbua wananchi na ufumbuzi wake,
Mbona hawajaongelea Ufisadi na Rushwa ambavyo ndio maadui wakubwa Watanzania?
 
mwakyembe.....1%281%29.jpg


Waziri wa Uchukuzi, Dk.Harrison Mwakyembe

Waziri wa Uchukuzi, Dk.Harrison Mwakyembe, ameapa kuwa hataogopa vitisho vyovyote kuwafukuza kazi watumishi wa mashirika, taasisi na idara za serikali zilizopo chini ya wizara yake wanaokwenda kinyume cha utendaji kazi kwani kama ni suala la kufa alishaonja kufa kipindi alipougua.

Alisema hayo juzi wakati akizungumza na wafanyakazi wa Chuo cha Bahari kilichopo jijini Dar es Salaam baada ya kukitembelea ikiwa ni siku moja baada kutembelea Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

"Nawahakikishia bandari itanyooka, nitapigana hadi dakika ya mwisho, sitaogopa kufa maana kama ni suala la kufa tayari nilishaonja kufa nilipougua sana,"alisema Dk.Mwakyembe.

Alisema nchi hii haisongi mbele kimaendeleo kutokana na maneno kuwa mengi na kwamba katika ziara yake aliyoifanya katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) amekuta kuna uozo mwingi na kuahidi kusafisha wale wote ambao wanatuhumiwa kuhusika na kashifa mbalimbali bandarini hapo.

Dk.Mwakyembe alisema wakati anachukua hatua za kusafisha kwa kuwang'oa watumishi wabadhirifu katika taasisi, idara, mashirika yaliyopo chini ya Wizara ya Uchukuzi, wanafunzi waliomaliza darasa la saba, kidato cha nne na sita wakae mkao wa kula kwa ajili ya kuziba nafasi hizo.

"Na katika hili sitanii, hapa nitaomba kabisa wale wanafunzi waliomaliza darasa la saba, kidato cha nne, sita na chuo kikuu waanze kujioorodhesha kabisa majina yao maana nitawafukuza kazi watu wengi sana katika wizara hii," alisema Dk.Mwakyembe.

Aidha waziri huyo aliutaka uongozi wa Chuo cha Bahari kuwa wawazi kwa wafanyakazi wao kwa kuwaeleza mapato na matumizi ili watumishi wasiwe wanajenga hoja kwamba fedha zao zinaliwa.

Aliutaka uongozi kukipatia ofisi tawi la Chama cha Wafanyakazi haraka na kwamba hakuna sababu ya kuviona vyama hivyo kama vyama vya upinzani katika sehemu za kazi.

Dk.Mwakyembe alisema kama uongozi wa chuo hicho utashindwa kukupatia Chama cha Wafanyakazi ofisi wasishangae atakapochukua maamuzi kwa kugawa sehemu ya Mkuu wa Chuo hicho kuwa ofisi ya chama cha wafanyakazi.



CHANZO: NIPASHE
 
ujinga mtupu kwa CCM
wanashindwa kushughulikia matatizo ya wananchi watumia pesa nyingi kuhadaa wananchi
hao waliohudhuria walikuwa na matarijio ya kupewa chakula na nauli.
nashangaa tu anaejiita mwanaCCM bila kujaua wanaowahutubia na kuwahadaa
ndio hao haowanaouza rasilimali zetu kwa wageni huku wakilimiliki majengo na mgarari ya kifahari.
amkeni watanzania mtajikuta mnuzwa ninyi na watoto wenu.
M4C Dar9[4]hhhh.jpg
Usanii juu ya Usanii
 
Mbona sijasikia aliye zungumzia maisha bora kwa kila Mtanzania? Changa la macho hili. Yaani wazazi wetu wanalala saa kumi na mbili kwa vile hawawezi kununua tena mafuta ya taa kisa kulinda biashara za vigogo wa Ccm?
 
Mwenye kukufuru ni nani? sema wewe kama kweli umkweli wa nafsi yako.

Anayeabudu "Mother and Child Cult"...Moon (Goddess-Mother), Star (Child). Muanzilishi ni Nimrodi na Semiramis (Babylon).
 
Hivi wabongo mna matatizo gani? Mnasubiri Yesu au Mohammad aje awatangazie ukombozi? Pale Jangwani palikuwa na watu 3000 kweli? Mbona mnapenda kudanganywa?
 
Baada ya kuona mkutano wa CCM leo pale jangwani kusema kweli CCM wamefuta ujio wa CDM na kuiangusha Chadema kifudifudi.
Nilijua tu mbio za CDM (Makobe) zitafikia ukingoni mida si mrefu ,na kweli Chadema sasa wana wakati mgumu kuliko wakati wowote ule na wasipoangalia watachawanyika kuliko ya mbuzi.

Bado CUF ambayo iaonekana kama haipo ,imezama na inaiangalia hali ya kisiasa inavyokwenda wakisubiri kupiga kwa style ya Checkmate.
Nafikiri wapo njiani kutayarisha mkutano wa aina yake hapo hapo Jangwani.
Kumbe lengo lao ni kufuta ujio wala sikujibu tuhuma zinazowakabili za wananchi.
 
Ama kweli kizuri ni kizuri na chenye ubora ni bora. ChaChaMa wameishiwa, hawana jipya ndo maana wakuu wao wameingia mitini mkutanoni.
 
Nasubiri kwa hamu hicho watakachokisema kuhusu UAMSHO...!
Shauku niliyokuwanayo kabla ya mkutano sasa imetulizwa... Nape, you made my day...ngoja nikaikamilishekamilishe siku kwa kuangalia magoli ya Euro 2012...CCM Oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee....!
 
KUNDI la akina SITA,MWAKYEMBE na NAPE limejinadi vizuri na limetumia fursa ya leo pasipo CCM Kuwashtukia kujijenga.Hakika NAPE ni mjanja mambo yake ni mkakati wa RAIS ajae atoke kundi lao.
 
Back
Top Bottom