Yaliyojiri Mkutano wa CCM Viwanja vya Jangwani (Dar) Juni 9,2012

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
1.jpg


223982_326580184087944_1568170980_n.jpg


SAM_2361.JPG


SAM_2354.JPG



SAM_2355.JPG



SAM_2357.JPG



SAM_2358.JPG




TEXT UPDATES:

Ni asubuhi tulivu ya Jumamosi na hali ya hewa ni nzuri kabisa.

CCM wanatarajiwa kufanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Jangwani ambavyo wapinzani wao wakuu walivibatiza kwa jina la viwanja vya CDM SQUARE.

Tayari shamrashamra zimeshaanza hapa uwanjani na shughuli za ujenzi na kupamba majukwaa zinaendelea.Mkutano huu utarushwa live na vituo kadhaa vya Television.

Tutakuwa hapa uwanjani kuwapa updates kila kitakachoendelea.

Updates:
Mpaka muda huu saa 8.30 watu wanaendelea kuja uwanjani ingawa kwa ujumla bado uwanja haujapendeza sana.Tunaendelea kusubiri zaidi huenda ni hizi foleni za Dar zinachelewesha watu.Wanachama kadhaa kutoka matawi mbalimbali wameshafika wakiwa kwenye mabasi na vyombo vingine vya usafiri.Baadhi ya wanachama wanadai wamekodisha kwa gharama zao na wengine wanadai wamekodishiwa na chama.Bado natafuta ukweli wa haya madai yao.

More updates.
Viongozi mbalimbali wanaendelea kutoa hotuba zao.Hotuba iliyoshangaza wananchi ni ya Nape Nauye aliyewashambulia kwa maneno makali waislam wa kikundi maarufu cha Uamsho Zanzibar kwamba ni MAJAMBAZI wakubwa.Wengi hawajafurahishwa na maneno yake na wanaona kama ameutukana Uislam.Idadi kubwa ya watu iliguna baada ya kauli hiyo ya Nape.

More updates....
Mkutano umemalizika lakini kwa ujumla katika wazungumzaji wote wa CCM na mawaziri walioongea aliyeonekana kuwagusa watu wengi ni Waziri wa uchukuzi Dr Harisson Mwakyembe ambaye alitoa hadi namba yake ya simu 0782242526 kumpigia wakati wowote mwananchi atakapokumbana na adha yoyote kwenye sekta ya usafiri. Mwakyembe kwa kujua anaangaliwa nchi nzima kupitia Television hakumalizia kwa kusifu CCM kama wenzake bali yeye alimalizia kwa kusema Dar Hoyeeee!

Baadhi ya kadi za CDM na bendera zimerudishwa lakini hakuna hata kiongozi mmoja wa ngazi yoyote aliyejitambulisha hadharani kwamba amejitoa CDM kitu kinachotia shaka malundo ya kadi za CDM zilizorudishwa.Sintofahamu nyingine ni karibia kadi zote za CDM zilizorudishwa hazikuwa na picha ya mwanachama na nyingine hazijapigwa mihuri.

Mwisho Pamoja na CCM kujitahidi kukusanya watu wengi kwenye mkutano huu wa leo kiuhalisia mkutano huu wa CCM haujaweza kuvunja rekodi ya mkutano wa CDM uliofanyika wiki mbili zilizopita na kuhudhuriwa na maelfu kwa maelfu ya wananchi kiasi kwamba Jiji la Dar lilisimama kwa zaidi ya masaa 6.
 
Wanabodi,

kwa sasa nimeshawasili hapa jangwani kuangalia kinachojiri,pilikapilika za upangaji wa viti vya plastic vyeupe unaendelea na uandaaji wa jukwaa umepamba moto huku mabango nayo yakiandikwa.

Mpaka sasa kuna bango kubwa la kitambaa limewekwa junction ya Morogoro road na kawawa limeandikwa;"KUHUSU VURUGU ZA UAMSHO CCM KUTOA TAMKO LEO SAA SITA''

Ugawaji wa T-shirt unaendelea hapa Jangwani na mambo mengine mtapata jinsi time inavyojiri.

Natumia laptop ndogo nimeificha kiaina staweza kutupia picha.

Watu ni wengi wameletwa na magari toka sehemu mbali mbali za dar hilo halina mjadala,
Lengo limeelezwa ni kujibu mapigo kwa upinzani.
Wasira kafika na gari la serikali akiwa amelala na kasema kachoka sana kwani kaja toka J,burg leo.
Niko jirani na mjumbe wa NEC CCM ana samsung galaxy anachukua picha huku akilinganisha na ule wa CDM,hajasema lengo nikujaza watu au nini?
Zaidi TV na Radio ziko live kwa sasa jongeeni.
 
sa kama huwezi kutuma picha umeanzisha thredi ya nini?
Mi mwenyewe sitakua na nafasi japo nipo mitaa ya jangwani, nikaona sina sababu ya kuanzisha thredi, au unataka thredi yako ndo iwe ya kwanza kuchangiwa?
 
Umenena mkuu nami niko eneo la tukio, ni bora ukajua mbinu na udhaifu wa adui yako ili iwe rahisi kumumaliza.

Safi sana kamanda.Tusaidiane kumwaga updates kwa wadau kila tukio litakalotokea.Tunaomba na thread zote zitakazoanzishwa ziunganishwe hapa.
 
Mimi nipo barabara ya Kilwa Road Mafuso yaliyo kodishwa na CCM nayapiga picha. zamani kabla hawaja filisi ile kampuni ya mabasi ya Scandinavia walikuwa wanayatumia sana
 
Wanabodi,

kwa sasa nimeshawasili hapa jangwani kuangalia kinachojiri,pilikapilika za upangaji wa viti vya plastic vyeupe unaendelea na uandaaji wa jukwaa umepamba moto huku mabango nayo yakiandikwa....
Mkuu tutakuwa pamoja
 
Back
Top Bottom