Yaliyojiri Mkutano wa CCM Viwanja vya Jangwani (Dar) Juni 9,2012

magufuli alielezea kwa kina sana juu ya sekta ya ujenzi akieleza kwa kina kwamba kwa sasa kuna kilometa 9000 za barabara za lami nchi nzima kwa maana ukitoka mtwara hadi mwanza kupitia dar,uende arusha kilimanjaro hadi tanga ni mwendo wa tax tu,hata kwa bajaji unaenda utakako bila kikwazo.
 
TEXT UPDATES:

Ni asubuhi tulivu ya Jumamosi na hali ya hewa ni nzuri kabisa.

CCM wanatarajiwa kufanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Jangwani ambavyo wapinzani wao wakuu walivibatiza kwa jina la viwanja vya CDM SQUARE.

Tayari shamrashamra zimeshaanza hapa uwanjani na shughuli za ujenzi na kupamba majukwaa zinaendelea.Mkutano huu utarushwa live na vituo kadhaa vya Television.

Tutakuwa hapa uwanjani kuwapa updates kila kitakachoendelea.

Updates:
Mpaka muda huu saa 8.30 watu wanaendelea kuja uwanjani ingawa kwa ujumla bado uwanja haujapendeza sana.Tunaendelea kusubiri zaidi huenda ni hizi foleni za Dar zinachelewesha watu.Wanachama kadhaa kutoka matawi mbalimbali wameshafika wakiwa kwenye mabasi na vyombo vingine vya usafiri.Baadhi ya wanachama wanadai wamekodisha kwa gharama zao na wengine wanadai wamekodishiwa na chama.Bado natafuta ukweli wa haya madai yao.

More updates.
Viongozi mbalimbali wanaendelea kutoa hotuba zao.Hotuba iliyoshangaza wananchi ni ya Nape Nauye aliyewashambulia kwa maneno makali waislam wa kikundi maarufu cha Uamsho Zanzibar kwamba ni MAJAMBAZI wakubwa.Wengi hawajafurahishwa na maneno yake na wanaona kama ameutukana Uislam.Idadi kubwa ya watu iliguna baada ya kauli hiyo ya Nape.

More updates....
Mkutano umemalizika lakini kwa ujumla katika wazungumzaji wote wa CCM na mawaziri walioongea aliyeonekana kuwagusa watu wengi ni Waziri wa uchukuzi Dr Harisson Mwakyembe ambaye alitoa hadi namba yake ya simu 0782242526 kumpigia wakati wowote mwananchi atakapokumbana na adha yoyote kwenye sekta ya usafiri. Mwakyembe kwa kujua anaangaliwa nchi nzima kupitia Television hakumalizia kwa kusifu CCM kama wenzake bali yeye alimalizia kwa kusema Dar Hoyeeee!

Baadhi ya kadi za CDM na bendera zimerudishwa lakini hakuna hata kiongozi mmoja wa ngazi yoyote aliyejitambulisha hadharani kwamba amejitoa CDM kitu kinachotia shaka malundo ya kadi za CDM zilizorudishwa.Sintofahamu nyingine ni karibia kadi zote za CDM zilizorudishwa hazikuwa na picha ya mwanachama na nyingine hazijapigwa mihuri.

Mwisho Pamoja na CCM kujitahidi kukusanya watu wengi kwenye mkutano huu wa leo kiuhalisia mkutano huu wa CCM haujaweza kuvunja rekodi ya mkutano wa CDM uliofanyika wiki mbili zilizopita na kuhudhuriwa na maelfu kwa maelfu ya wananchi kiasi kwamba Jiji la Dar lilisimama kwa zaidi ya masaa 6.

Well balanced report, ukweli wote umeusema na hiki ndicho hakipo kwa sasa ungekuwa CDM, ungelalia huko, ungekuwa CCM ungelalia huko

hata kama ni member wa any of those parties, lakini umwekea utu na uzalendo wa kusema kinachoonekana kwa uhakika

Kindly receive my congratulations!!
 
conclusion huwa ni kama mjumuisho, na wewe wabe unaamini huu mwisho wake? kuwa jiji la dar lilisimama zaidi ya masaa 6! kweli ?? Hivi mnafikili kila mtu anapenda haya mambo ya siasa kiasi cha kusimamisha shughuli zao!
 
Nimemsifu kwa habari alivyoileta na sio maoni yake..........
 
Well balanced report, ukweli wote umeusema na hiki ndicho hakipo kwa sasa ungekuwa CDM, ungelalia huko, ungekuwa CCM ungelalia huko

hata kama ni member wa any of those parties, lakini umwekea utu na uzalendo wa kusema kinachoonekana kwa uhakika

Kindly receive my congratulations!!

Ni kweli kamanda.Pamoja sana.Kutokusema ukweli siku hizi ndiko kunakoangamiza vyama vyetu...Hakika anahitaji pongezi zetu.
 
Mwakyembe anapiga kazi mbaya, hapa nape hajapata alichokua anategemea, anasema ukikutana na madereva au watu wengine wanafanya upuuzi katika sekta ya uchukuzi basi we kamata details zote afu mpigie katika 0782242526
Mwakyembe sasa ni mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani? Ukiona mtu anaingilia kazi ya mtu mwingine, tambua kuwa kazi yake haijui.
 
Mwakyembe sasa ni mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani? Ukiona mtu anaingilia kazi ya mtu mwingine, tambua kuwa kazi yake haijui.

na ukiona mtu hajui kuwa usafirishaji uko chini ya wizara ya uchukuzi ujue ufahamu wa huyo mtu ni mdogo
 
Back
Top Bottom