CCM wanatakiwa kujua kuwa watanzania wanataka issue za 'pocket'. Yeye kama mtu binafsi hawezi kula madaraja, au ahadi. CCM ilitakiwa kuja na mkakati wa kuondoa ugumu wa maisha na kuongeza ajira, hayo mengi ni secondary issues.
CCM walitakiwa kujibu hoja kwa Miswada na programme za kuipeleka Tanzania mbele ili 2015 watu waweze kuwapima. Haya si mapinduzi ya nani kapata watu wengi, haya ni mapinduzi ya kifikra. Kama mimi ningekuwa ni CCM strategy ningepata shida sana kuona mikutano yangu ikihudhuriwa na kina mama na wazee, wakati vijana ambao ndiyo wanabeba mustakabali wa chama na Taifa in the future hawapo.