Yaliyojiri Mkutano wa CCM Viwanja vya Jangwani (Dar) Juni 9,2012

Balantanda na ritz nasubiri picha wakuu.
attachment.php
 
Jamani watanzania sio wa kudanganya ndo maana umeona watu wanaondoka kabla mkutano kuisha,pole magamba hamna jipya,mmechokwa kapumzike,pipoz power
 
CCM imedhihirisha tena kuwa ni chama kinachoongoza nchi na kisochofanya madudu ya uongo.

Leo nimewaonea sana huruma chadema walipoanza kuchanwa na Nape, wakaja kina Wasira, Maghembe, Magufuli, Tibaijuka. Wakaeleza kwa ufasha kabisa na kujiamini jinsi CCM inayotimiza ahadi zake.

Wasira akagusia jinsi chadema wanavyoiba hoja na kuwahi kuzitangaza kama ni zao. Magufuli akawakumbusha miradi ya barabara za lami ambayo haijawahi kuonekana barani Afrika kwa kiwango hiki kwa muda mfupi.

Nawaonea huruma chadema wanavyopita wakidanganya Watanzania, leo magwanda ya khaki wameumbuka.

Waislam wa UAMSHO wametukanwa du kweli nape kichaa tena hataki kura zao
 
Watu wote wamekaa kwenye viti unasema uwanja umefurika! Kweli Tanzania ina ma-bogus wengi
 
Kumbe mkutano umehudhuriwa na watoto wengi mpaka wamepotea nadhani hata watoto wa zomba,ritz,katiba mpya wamo.
 
Nyinyiemu (CHama cha Magamba) ni wapumbavu sana,

Hivi wanatuona sisi hatujui hesabu au aje? eti watu elfu 4 sijui elfu ngapi wamerudisha kadi, hebu watuambie hapo uwanjani kuna jumla ya watu wangapi waliohudhuria? kwa haraka haraka hawafiki watu elfu tano, unataka kuniambia wote hao waliohudhuria ni watu wa upinzani waliorudisha kadi? na walipata wapi hizo sare zao za kupigia deki chooni walizovaa? na je, ina maana hakuna wanachama wao nyinyiemu waliohudhuria?

Kweli Chadema inawapeleka mbio hadi wanaamua kudanganya uongo ambao hata mwanangu kaukataa.

Me nakereka sana pia na suala la waziri ambaye anahudumia wananchi wote bila kujali chama, anasimama hapo na kujitambulisha e.g mama tibaijuka eti mimi ni waziri, damn it, amesimama pale kama tibaijuka mwanachama wa ccm au mbunge wa ccm kupitia alikotoka au kama ni mjumbe wa ngazi yoyote ndio aitaje, hawatakiwi kutumia title zao za uwaziri katika mikutano hii. halafu wanaongea uongo hadi mwanangu anashangaa


aaaaaaah
 
wakati mkutano unamalizika mkutano wa wana ccm jangwani leo;kumetolewa taarifa ya kukusanywa kadi za wanachama wa chadema 4000 wanaotakakuhamia ccm, je kupata idadi kubwa ya wanachadema kuhamia ccm mkutano umejibu kiu na kero ya maisha magumu ta watanzania, kama ilivyoainishwa na wasira?
 
Watu ni wengi sana kaka, mi nipo Jangwani, ni wengi kuliko ule mkutano wetu, ila wao wamepanga viti halafu daladala zimemwagwa kama mvua.



Mkuu hapo hamna watu.Kiti kimoja kinachukua nafasi ya watu watatu..Ukiangalia kwa nyuma pia watu hawapo.Tulijua ni kweli mabasi na malori lazima, ila wametoka nje ya DSM. Kingine ni bora kueleza mipango mikakati jinsi gani itasaidia kupunguza maisha makali kwa mtanzania.NDUGU MAISHA NI MAGUMU KWELI.
 
Hivi urudishaji wa kadi unakuwaje? CDM wao huonyesha wazi watu wanaorudisha kadi na wengine kupandishwa jukwaani kusalimia wananchi, Vipi nyinyim, mbona kimyakimya tu? Siyo maigizo kweli?
 
Kumbukeni hao wamesombwa na kupewa posho kuanzia buku 2-5 mwisho mkutano ngumi huwa zinapigwa kudai hela
 
Si kawaida chama kikubwa kama hiki kuhitimisha hotuba yake saa 10:30 jioni, chama chenye mengi ya kutujuza baada ya uchaguzi. Hii inatia shaka. Walishindwa kumleta hata mbunge wa mtera?
 
Sijaona jipya katika mkutano huu zaidi ya mipasho na kuangalia nani kavaa tenge zuri la kijani, shati gani la kijani na njano. Hakuna sera zozote zaidi ya kuonyesha CCM ina hofu kubwa na Chadema!
 
Kaunga lets go....lets go.....there is nothing here....this meeting was much trumpeted but alas, I am confused as to what they really wanted to achieve

umeona mpwa eeeh, mi sijaelewa ujue muda wote huo lipi la maana lililoongelewa!
 
Kuna watu wanarudisha kadi naona tisheti ya cuf imeshikwa na kijana hapa. Naona kadi kibao za chadema. Komba na tot wanaburudisha.
Danganya toto hiyo hakuna hata kadi moja ya CDM imerudishwa wameandaa kadi hizo feki kuudanganya uma!!!
 
Back
Top Bottom