Yaliyojiri Mkutano wa CCM na waandishi wa habari Peacock Hotel

Kwani mnadhani wangeongea nini zaidi ya hicho walichoongea, hakuna sehemu LOWASA aliyotaka ajibiwe, alichofanya EDO ni kusema ukweli khs mhusika wa RICHMOND.........sasa mlitegemea CCM wajibu nini na tangu lini ukweli ukajibiwa?
 
Ule mkutano wa CCM uliotangazwa kwa mbwembwe zote, ukitarajiwa kujibu mapigo ya Edward Lowassa aliyehamia Chadema, umegeuka kuwa kituko baada ya CCM kumtuma katibu mwenezi mkoa wa Dar, Juma Gadafi Simba kuzungumza.
Awali waandishi wa habari waliokuwa wamejikoki vilivyo katika hotel ya Peacock hawakuamini macho na masikio yao kumwona kada huyo wakidhani Nape ndio anakuja kuzungumza.
Mmkutano huo ulikuwa unarushwa live na Azam TV ambao hawakuamini kinachoendelea kwani kada huyo aliishia kiwashukuru tu waandishi kwa kupokea Dr. John Magufuli na kujigamba kuwa atashinda kwa kishindo.

Baada ya mazungumzo yake mafupi, waandishi walimuuliza maswali mengi hadi akachanganyikiwa na kukataa kuyajibu. Waandishi walimfuata hadi nje ya ukumbi na akakimbilia kwenye lift na kuondoka.
Katika mkutano huo alikuwepo msaidizi wa Nape, Chongolo na mpigapicha wa CCM, Bashiri Nkoromo, waliomtaka Gadafi kusitisha mkutano.

My take: CCM wamechanganyikiwa na kuondoka kwa Lowassa

Vikao vyao hufanyika Lumumba sio kwenye mahotel
 
Mbona hakuna kitu hapo..

Yani mnamtuma huyo aliyeifilisi Simba team mapato ya mlangoni ndo awasemee?

Juma Simba QADAFI ni mchumia tumbo wa manzese na aliwahi kuwa mwanachama wa CUF
 
ukiona mgonjwa anazidi vituko cku baada ya cku fanya mpango uanze kuwaita ndugu wa mbali wasogee karb kwan mgonjwa anakarbia ku die
 
...adui amechanganyikiwa hajui hafanye nini, moja haikai mbili haikai imekuwa ni full kuweweseka...
 
kidogo ccm wamefuata ushauri wetu sisi kina gogo la shamba wangekuwa wanafuata ushauri wetu tangu awali asinge wakuta yote yaliyowakuta
 
Mkuu ni majanga!

Kwanza kaja tu mtu ambaye hata sijawahi kumsikia anaitwa Juma Simba Gadafi wakisema ni Katibu wa uenezi mkoa wa Dar es salaam.

Kaanza kuongea kwa kusema hoja iliyomleta ni kuwashukuru wananchi kwa kuwa mchakato wa kumpata mgombea wa kiti cha urais kupitia CCM umekwishafanyika na wamempata mgombea anayekubalika hivyo watashinda katika uchaguzi ujao. Baada ya kusema hayo asema amemaliza. Hapo sasa waandishi wakaguna akasema kama kuna swali uliza.

Mwandishi akauliza kuwa kuanzia jana CCM imealika waandishi wa habari kisa ni kuwashukuru tu wananchi? Kama hivyo si wangetoa tu taarifa na sio kuwasumbua waandishi wa habari?

Waandishi wakamuuliza na vipi kuhusu tukio la kuhama kwa Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa kujiunga CHADEMA. Jamaa kajibu Lowassa alipoingia CCM aliingia kwa hiari yake na sasa ameamua kuondoka kwa hiari yake.

Alipoulizwa kwa nini hakuna hata kiongozi mmoja wa kitaifa aliyeambatana naye kasema Nape yupo Mtama anapiga kampeni na wengine wana majukumu mengine. Waandishi walipotaka kumuuliza maswali mengine jamaa kasema inatosha hawezi kujibu maswali yote. akaondoka ukumbini.

Waandishi na wahariri wa habari wame-mind kwelikweli lakini hali ndio hiyo wakuu.

KIUFUPI unaweza kusema mambo si shwari CCM.

Chama Cha Majambazi kimekwisha. October watatueleza vizuri mali za watanzania wote nani anazila.

IPTL
Meremeta
EPA
Escrow (Haswa Fuso na viroba vya Stanbic)
....

JK atakuwa kapiga simu "usikurupuke kujibizana na Lowassa humuwezi, Chama kizima 6milion wameshindwa itakuwa jeshi la mtu mmoja Nape?"
 
Nilijua tu huyu kaka yetu Simba 'Ghadaffi'' tunayekunywa naye gahawa Magomeni Mapipa jijini DSM asingeweza kabisa kuwa msemaji hata wa mkoa wa CCM DSM huu ni utani mkubwa sasa naamini maneno ya Mzee Kingunge Ngombale Mwiru kuwa CCM mambo yanaendeshwa bila utaratibu na matokeo yake hata nchi yetu inaendeshwa kienyeji pia kama kijiwe cha gahawa.
Mkuu hiyo gahawa ananywea shibam au?
 
Mkuu usiandike kishabiki, walisema wanamkutano na Waandishi wa habari hakuna sehemu waliyosema watamjibu Lowassa. Hicho walichoongea ndio kilichopangwa, usiwaze kushabiki twende haki tu kwa hoja, mimi nilikuwepo hapo.

Sasa mbwembwe zilikuwa za nini kumbe mkutano wenyewe ulikuwa wa kakatibu ka mkoa, aha acheni hizo na muwe wakweli, hapa hakuna visingizio kwani siasa ni ushabiki, bila ushabiki hakuna siasa. Siasa ni uchaguzi pasipo ushabiki hakuna uchaguzi.
 
ukawa ni gharika kuuuuu....haya tokomeza hao mafisi....2015 for change
 
Ule mkutano wa CCM uliotangazwa kwa mbwembwe zote, ukitarajiwa kujibu mapigo ya Edward Lowassa aliyehamia Chadema, umegeuka kuwa kituko baada ya CCM kumtuma katibu mwenezi mkoa wa Dar, Juma Gadafi Simba kuzungumza.
Awali waandishi wa habari waliokuwa wamejikoki vilivyo katika hotel ya Peacock hawakuamini macho na masikio yao kumwona kada huyo wakidhani Nape ndio anakuja kuzungumza.
Mmkutano huo ulikuwa unarushwa live na Azam TV ambao hawakuamini kinachoendelea kwani kada huyo aliishia kiwashukuru tu waandishi kwa kupokea Dr. John Magufuli na kujigamba kuwa atashinda kwa kishindo.

Baada ya mazungumzo yake mafupi, waandishi walimuuliza maswali mengi hadi akachanganyikiwa na kukataa kuyajibu. Waandishi walimfuata hadi nje ya ukumbi na akakimbilia kwenye lift na kuondoka.
Katika mkutano huo alikuwepo msaidizi wa Nape, Chongolo na mpigapicha wa CCM, Bashiri Nkoromo, waliomtaka Gadafi kusitisha mkutano.

My take: CCM wamechanganyikiwa na kuondoka kwa Lowassa
Tatizo ni hofu ya kushindwa.
 
Back
Top Bottom