Yaliyojiri Mkutano wa CCM na waandishi wa habari Peacock Hotel

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
2,436
4,430
Kesho saa 7 mchana CCM watazungumza na waandishi wa habari Lumumba. Ajenda kuu ni Lowassa kujiunga CHADEMA.
CLA85fCWsAICtzh.png

Chanzo: Taarifa ya CCM kwa wahariri.

========================

UPDATES;
attachment.php


2.Update:

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Juma Simba Gadafi amesema:

CLFesNlUkAEiI68.jpg:large

"Nawashukuru Waandishi wa habari kwa kuja, CCM tumewaita hapa, kuwashukuru kwa kushirikiana nasi katika Mikutano iliyokuwa ikiendelea Dodoma. Tunaomba Tume ya Uchaguzi iongeze Muda wa kujiandikisha na mashine za BVR, ili watu waweze kujiandikisha kwa wingi, ili ifikapo 25 OCt CCM iweze kushinda kwa Kishindo kwani Dar es Salaam ndio Ngome ya CCM".

- Pia, Gaddafi amesikitishwa na kitendo cha waandishi wa habari kumuuliza maswali kuhusiana na kujiengua kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa JMT, Edward Lowassa kutoka CCM na kuhamia CHADEMA na kusisitiza kwamba hayo ni maamuzi binafsi ya Mhe. Lowassa na hayana athari yoyote kwa CCM, kwani yeye sio wa kwanza kufanya hivyo, huku akitolea mfano kwa wakina Mhe. Agustino Lyatonga Mrema na Dr. Slaa ambao walishawahi kukitumikia chama hicho kabla ya kuhamia Upinzani.

Akifafanua kuhusu kutokuwepo kwa viongozi wakuu wa CCM katika Mkutano huo, Katibu Juma Simba ameeleza kuwa yeye ndiye Msemaji Mkuu wa CCM kwa Mkoa wa Dar es salaam, hivyo ni mtu sahihi kuwepo hapo na kudokeza kwamba viongozi wengine wako kwenye harakati nyingine za kichama huko mikoani.
 

Attachments

  • ccm.png
    ccm.png
    66.1 KB · Views: 10,539
Back
Top Bottom