Yaliyojiri kesi inayomkabili Mbowe na wenzake leo Februari 4, 2022. Kesi imeahirishwa. Shahidi wa 13 kuendelea kutoa ushahidi Februari 7, 2022

Hizi siku mbili zilikuwa ngumu sana kwangu. Mawakili wa serikali walitukatili sana kutoleta mashahidi. Kufuatilia hii kesi inanikumbusha uhondo niliokuwa naupata enzi nikisoma novel za Willy Gamba.

Naweka kambi hapa kufuatilia michongo.

Mungu ibariki JF na mleta mchongo kwa updates zako zilizotukuka
kama mimi yaani
 
Najiuliza: Kwa nini wanaleta mashahidi kama huyu? Alisema chochote kinachoweza kuthibitisha mashtaki? Nje ya kwamba aliambiwa Mbowe aliandaa Ugaidi?
Toka mashahidi waanze kutoa ushahidi wao wanaongelea ukamataji, uwekaji mahabusu, kuandika maelezo, kusafrisha washitakiwa, kuharibika kwa gari njiani, detention register,miala ya simu shs 500,000/- Kama fidia ya nauli n.k. Hakuna ushahidi unaotolewa unaoonyesha mwelekeo wa ugaidi, hata mashahidi muhimu kina Kingai, Mahita,Urio na huyu anayeendele hawaonyeshi. Sasa ugaidi utaelezwa lini na nani?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Shahidi wa jana ilibidi aombe awe anatoka toka kwenda kwa short call na kuna wakati inaonesha aliomba tu ruhusa kabla Mh. Jaji hajamalizia kumjibu akawa ametoka mkuku!

Huyu n yule wa wakati ule hivi watakuwa na maradhi gani yanayowafanya wasiweze kustahimili kubana mkojo kizimbani mpaka wamalize. Wameshindwa kuiga mfano wa MaWakili ambao wao wakianza examination ni mpaka wanamaliza hamna kuomba ruhusa?

Lakini hata hivyo Acha ikae hivyo hivyo!
UTI na tezi dume.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom