Yaliyojiri katika Ziara ya Rais Samia Mkoani Morogoro

Aidha Mkuu wa mkoa wa Morogoro Bw. Martin Shighela alisema ziara hiyo ya Samia Suluhu Hassan atakutana na Wananchi na hivyo akatoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kumlaki Rais wao.
Hajasema tuje na mabango ya aina gani?
 
Kwa kweli mkoa wa Morogoro unapaswa kumegwa.
Ni mkoa wenye eneo kuuubwa lakini cha ajabu huwenda huo mkoa unawanyama wengi na maeneo ya mbuga za wanyama kuubwa kuliko hata watu na maeneo ya watu kuishi
 
Mwache Mama aendelee kupiga kazi. Endelea kutatua shida za wananchi.


Asante Mama Samia bodi ya mikopo wamenionfolea dhulma yao ( waliyoita VRF na Faini) Karibu mil. 5 +
Mungu akubariki
 
Hahahahaaaa.. hata huku USA, George Bush, Clinton, Obama, Trump ...bado wanaendelea kukagua miradi ya maendeleo...kazi iendelee.
Acha kueneza uongo, Trump ana keshaondolewa huyo atakagua mradi gani?

Mzee wa msoga ni mwizi na hashitakiwi, halafu wewe unafananisha USA na bongo
 
Mnapopata bahati ya kuongea na Rais, muwe mnafikisha kero zinazoikabili jamii husika.

Mfano hapo Morogoro JPM alifanya ubabe kwa mwekezaji wa kile Kiwanda cha Tumbaku (TTPL) hadi wakasusa wakafunga kiwanda. Hivyo zaidi ya wakazi 10,000 wakajikuta wanakosa ajira sasahivi wapo mtaani.

Hivyo tumieni fursa hiyo mwambieni Mama amrudishe huyo mwekezaji.
Mkuu GEMBESON ,umeandika jambo la msingi sana. Kongole.
Kufungwa kwa TTPL kwa kweli kuliniumiza sana sana. Watanzania waliokosa ajira ni wengi na kwa kweli imerudisha nyuma uchumi wa Moro kwa kupungua kwa mzunguko wa pesa mitaani.
Mh. Rais Samia S.H inabidi alivalie njuga sana hili swala ili hawa wawekezaji waweze kurejea haraka iwezekanavyo.
 
Back
Top Bottom