Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Najiuliza maswali mpaka sasa na bado sipati majibu! Januari Mkamba ndani ya 5 bora kwa kigezo gani? Amekuwa Naibu waziri kwa Muhula mmoja tu, amekuwa Mbunge kwa Mihula miwili tu, sasa ni kipi kilichomfanya hata ateuliwe?
Ni muhula mmoja tu mkuu
 
Swali ni je Lowasa atakuwa mkomavu wa kisiasa na kukubali yaishe?

Au ataamua "ukimwaga ugali namwaga mboga"??
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Nina kila sababu kumshukuru Mungu Rabuka, kwa kusikiliza kilio chetu. Hakika mimi pamoja na wadau wengine humu tulianzisha mapambano ambayo kwa hakika yalikuwa magumu sana kwetu. Uzalendo wetu ndio ulituunganisha humu. Tulishikamana na tulitiana moyo ijapokuwa tulijua kuwa tuna kazi kubwa mbele yetu. Wapo waliotubeza humu kuwa tunapoteza muda bure kupambana na mtu mwenye pesa na mamlaka. Wapo waliosema kuwa tunatumika na baadhi ya wagombea. Wapo pia waliosema kuwa hakuna anayetusikiliza humu. Wapo pia waliobeza yale tuliyokuwa tunaandika huku wakituambia kuwa sisi ni wazushi. Hakika tulikumbana na misukisuko mikubwa sana. Wengi tumepigwa ban mpaka za mwezi lakini baada ya kifungo tuliendelea na mapambano hadi kimeeleweka.

Wadau, unapomuua nyani hutakiwi kumuangalia usoni. Ndivyo nilivyofanya pamoja na wadau wengine kama akina Simiyu Yetu, TataMadiba, Emma, kanone, Weston Songoro, Chabruma nk. Hatukumuangalia usoni Lowasa pale tulipobainisha mipango yake ovu. Tuliweka bayana pale alipogawa fedha kwa viongozi wa dini ili aungwe mkono. Tulieleza waziwazi jitihada za Apson Mwang'onda kuhakikisha kuwa fisadi Lowasa anaenda Ikulu. Mipango yake ovu hiyo ilibainishwa huku tukipata kwa urahisi taarifa ovu za Team Lowasa.

Wengi wetu humu hatukuwa na uhakika kama Lowasa atakatwa. Hii ni kwa sababu jamaa ana fedha nyingi na alijaribu kuhonga kila mtu aliyoeona kuwa ana maslahi kwake. Ila ameshindwa kutuhonga humu kutokana na utaratibu mzuri wa JF wa kulinda watoa habari. Lowasa hakuwa na namna ya kutufikia members humu. Alikuwa na mamlaka tu ya kuagiza mods watupige ban. Ila hiyo haikutukatisha tamaa. Pale tulipoanguka tulisimama tena na kuendelea na safari na sasa tumefika kileleni kwa furaha kubwa sana. Fisadi kakatwa. Jeuri ya fedha haijamsaidia. Mataikun waliomzunguka hawajamsaidia. Watu vichwa maji waliomzumguka hawajamsaidia.

Baada ya kuhakikisha kuwa CCM hakihodhiwi na mafisadi, sasa ni muhimu wana CCM tukashikamana kwani Umoja ni Ushindi. Kwa kitambo kidogo tuliwaweka pembeni mahasimu wetu, UKAWA. Tunarejea kwa kishindo. UKAWA kaeni chonjo. Mapigo yale yaliyowasambaratisha akina Slaa yanakuja tena kwa kasi ya hali ya juu. Naamini kuwa watu tuliofarakana kimawazo kama Ritz, MUSSA ALLAN, Minyoo, Funza, Ocampo four, Pasco nk tutakuwa pamoja tena katika mapambano dhidi ya adui yetu mkuu.

Mwisho niwaombe radhi wale niliowakwaza kwa namna moja ama nyingine. Mkumbuke kuwa si makusudi yangu kuwakwaza bali ni katika jitihada za kupambana na mafisadi. Baada ya ushindi huu, Naamini kuwa tutaendelea kuwa pamoja ili kuhakikisha kuwa CCM inashinda kwa kishindo ifikapo Oktoba.
 
Ni shangwe na nderemo kwa wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mjini Dodoma yalipo makao makuu na Tanzania kwa ujumla baada ya Kufanyika mchujo wa Tano bora.

Ulikuwa ni mmpambano uliovuta wengi ni nani na nani watakaoingia kwenye ngwe hii ya Lala salama.

Hatimaye majina matano yametitokeza ya watia nia

1 . JANUARY MAKAMBA
2. JOHN POMBE MAGUFULI
3.BALOZI AMINA SALIM ALLY
4.ASHA ROSE MIGIRO
5.BENARD MEMBE

Kutokea kwa Jina la JANUARY MAKAMBA kumepokelewa kwa Furaha na Shangwe.

Umakini wake katika kujenga hoja na uwezo wake katika utendaji wa kazi unafahamika kwa watu wote.

Kwakuwa;
Rais ndiye kiongozi mkuu wa Nchi, na ndiye mwenye maamuzi yote muhimu ya juu ya Taifa, kwa Nafasi hii ya hadhi dhahiri ni kwa kiongozi huyu kijana na Mwadilifu mwenye mikono safi.

Kamati kuu ya Chama cha cha Mapinduzi iliyoketi jana kuanzia saa kumi alasiri ikiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho.

Ilionyesha juu ya Uasisi wa jambo jema hutoka kwa Mungu.

Japokuwa kulikuwa na Tabiri nyingi za majina yalikuwa yamepenya ndani ya chama , kamati hii ilifanya kazi kwa usiri mkubwa sana.

Kazi ya kupiga kura kwa wajumbe wa Mkutano mkuu haitokuwa Ngumu kutokana na sifa zilizo wazi kwa majina matano yaliyo teuliwa.

Kijana huyu muadilifu mwenye sera zenye kitu kipya ndani ya Tanzania na uwezo anuai wa kusimamia mawazo ya jumla na ufanisi wa kuandaa mipango.

Amewashangaza watu waliokuwa wakifikiria wakati wake sio sasa ni Bado hivyo Asubirie.

Kuwaachia wenye jana nyingi na kesho chache, hakuna Daktari asiyekuwa na uwezo wa kutibu Tatizo bila kulijua lazima Daktari afahamu chanzo cha Tatizo ndipo ajue dawa yake ni nini.

Kwa Tanzania tunaweza kupata Daktari mzuri kama wajumbe wa NEC wa chama cha mapinduzi watafanya uchaguzi kwa umakini, na kutimiza mpango huu wa Mungu.

Imeandikwa na,
KIOGO MPINA,
DODOMA LEO.
 
Mimi Lowasa nime kukatia rufaaa
ushahidi ninakuja nao
huko huko
tupambane
unnamed%2B%25287%2529.jpg
 
Last edited by a moderator:
Naona scenarios mbili.
1. Benard Membe anaingia 3 bora pamoja na Magufuli, lakini Magufuli anashinda kwa kupata support ya TeamLowassa
2. Magufuli anakatwa mapema, asha Rose Migiro anashinda kwa support ya TeamLowassa.
Benard Membe ana wakati mgumu sana... Wajipange vizuri.
Lakini TeamLowassa wajue kwamba hata wakipiga kura za huruma au hasira, hao watatu watakaopatikana wana baraka za Kikwete.
 
Mwaka 2010 CCM Mkoa wa Mbeya walifanya Makosa Kwenye Nafasi ya Mgombea Ubunge Mbeya Mjini hatima yake Bw Joseph Mbilinyi SUGU akawapiga kwa Ticket ya Chadema, Mwaka huo huo Jimbo la Iringa Mjini CCM walifanya Makosa wakamkata Frediriki Mwakalebela kipenzi cha watu Wakamweka Monica Mbega hasira ya wananchi wakamchagua Peter Msigwa.

Mwaka huo huo 2010 Jimbo la Arusha Mjini CCM ilifanya Makosa wakamweka Batilda Buriani ambaye alikuwa hakubaliki na wananchi hasira ya wananchi wakamchagua Godbless Lema. CCM haitaki kujifunza kutokana na Makosa sasa wamecheza karata Dume kwa Nafasi ya Uraisi Hasira ya Wananchi wataiweka UKAWA madarakani lets wait and see.

Watanzania wa leo sio wale wa miaka 15 ilopita kuwa kila mgombea anayewekwa kuwania urais kwa ticket ya CCM anashinda uchaguzi.
 
Naona scenarios mbili.
1. Benard Membe anaingia 3 bora pamoja na Magufuli, lakini Magufuli anashinda kwa kupata support ya TeamLowassa
2. Magufuli anakatwa mapema, asha Rose Migiro anashinda kwa support ya TeamLowassa.
Benard Membe ana wakati mgumu sana... Wajipange vizuri.
Hakika Mkuu. Benard Membe ndiye yupo kwenye wakati mgumu zaidi. Sitegemei pro Lowasa wampigie kura Membe. Magufuli ndo chaguo sahihi kwa wana CCM ikiwa tunataka kushinda kwa kishindo
 
Hijawahi kutokea, mbwembwe zoote, pesa zoote na nguvu zoote alizotumia mh Edward lowasa na sasa ametolewa nje!

Janja ya lowasa ilionekana toka zamani alijifanya kuwa na upendo kwa makundi mengi ya kijamii ilhali akijulikana dhahiri kuwa hafai ktk urais.

Nimefurahi sana anguko la ufalme huu wa Giza CCM!
Katika mila za kiafrika sio jambo la kawaida kushangilia mtu anapopata msiba. Hebu kuweni na huruma hata kidogo tumetumia gharama kubwa jamani. Tunaomba faraja zenu wakati huu badala ya kejeli
 
Back
Top Bottom