Yaliyojiri Huku kwetu Kwamtogole

Yaliyojiri Huku kwetu Kwamtogole

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
Ni shost aliolewa amekaa kwenye ndoa na mume wake huu mwaka wa kumi na mbili mpaka wamefanikiwa kununua nyumba Kwamtogole. Ni nyumba ya vyumba sita baada ya kuikarabati bi shost anapewa taarifa na mume kuwa anakwenda kuoa mke wa pili.

Shost aliumia lakini alimwambia mume kaoe tu, baada ya ndoa tulicheza mdundiko kumkaribisha bi harusi mtaani, shost shurti kumtunza mwari. Tulikula pilau na soda za Azam juu.

Imepita miezi mume anakwambia bi mdogo hali yake si nzuri sana ki pesa hivyo wavumiliane . akiachiwa pesa ya mboga ni za budget ya dagaa maharage na mchicha au mlenda na dagaa.

Mume akiwa na zamu ya kulala kwa bishost anampa pesa ile ile aaliyomuachia bi mdogo lakini shost ni mtoto wa mjin, akiachiwa ile pesa anapika mchicha baadae anakata kitunguu saumu na viungo vya pilau akisha kaanga harufu ikikolea anaepua. Nyumba haina ceiling board, mke mdogo anaona haya makubwa kumbe akilala kwa mkewe anatoa pesa ya pilau.

Usiku bishost anatufuata kama kuna aliyenunua khanga au kitenge amtolee upya, basi atavaa khanga mpya kama mume amelala kwake.

Mwisho wa siku bi mdogo kuomba talaka mwenyewe alimwambia mume kama unampenda mke wako uliniolea nini, yeye ndiye wa kula pilau na kuvaa khanga mpya?

Si kila ulionalo ni la kweli chungu za kwanza.
 
Hahahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa kwa waswazi hiyo kawaida sana, tatizo wa Masaki Magorofani lazima lishangawe....
 
Back
Top Bottom