Yaliyojiri Huku kwetu Kwamtogole

Yaliyojiri Huku kwetu Kwamtogole

Ni shost aliolewa amekaa kwenye ndoa na mume wake huu mwaka wa kumi na mbili mpaka wamefanikiwa kununua nyumba Kwamtogole. Ni nyumba ya vyumba sita baada ya kuikarabati bi shost anapewa taarifa na mume kuwa anakwenda kuoa mke wa pili.

Shost aliumia lakini alimwambia mume kaoe tu, baada ya ndoa tulicheza mdundiko kumkaribisha bi harusi mtaani, shost shurti kumtunza mwari. Tulikula pilau na soda za Azam juu.

Imepita miezi mume anakwambia bi mdogo hali yake si nzuri sana ki pesa hivyo wavumiliane . akiachiwa pesa ya mboga ni za budget ya dagaa maharage na mchicha au mlenda na dagaa.

Mume akiwa na zamu ya kulala kwa bishost anampa pesa ile ile aaliyomuachia ni mdogo lakini shost ni mtoto wa mjin, akiachiwa ile pesa anapika mchicha baadae anakata kitunguu saumu na viungo vya pilau akisha kaanga harufu ikikolea anaepua. Nyumba haina ceiling board, mke mdogo anaona haya makubwa kumbe akilala kwa mkewe anatoa pesa ya pilau.

Usiku bishost anatufuata kama kuna aliyenunua khanga au kitenge amtolee upya, basi atavaa khanga mpya kama mume amelala kwake.

Mwisho wa siku bi mdogo kuomba talaka mwenyewe alimwambia mume kama unampenda mke wako uliniolea nini, yeye ndiye wa kula pilau na kuvaa khanga mpya?

Si kila ulionalo ni la kweli chungu za kwanza.
Kumbe sisi majiran eh[emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12]

Samael
 
Mwenyewe aliachia ngazi aliona viti vinawenyewe hivi mimi sienei hapa

Ila mke mdogo akija kugundua ndio ameshaikosa bahati tena hiyo.

Ila my dada hii story inafundisha pia kwamba kukurupuka sio kuzuri kilicho bora ni kufanya uchunguzi kwanza.
 
Ila mke mdogo akija kugundua ndio ameshaikosa bahati tena hiyo.

Ila my dada hii story inafundisha pia kwamba kukurupuka sio kuzuri kilicho bora ni kufanya uchunguzi.
Kuolewa mke wa pili tena mkae nyumba moja inataka moyo sana.
 
Ni shost aliolewa amekaa kwenye ndoa na mume wake huu mwaka wa kumi na mbili mpaka wamefanikiwa kununua nyumba Kwamtogole. Ni nyumba ya vyumba sita baada ya kuikarabati bi shost anapewa taarifa na mume kuwa anakwenda kuoa mke wa pili.

Shost aliumia lakini alimwambia mume kaoe tu, baada ya ndoa tulicheza mdundiko kumkaribisha bi harusi mtaani, shost shurti kumtunza mwari. Tulikula pilau na soda za Azam juu.

Imepita miezi mume anakwambia bi mdogo hali yake si nzuri sana ki pesa hivyo wavumiliane . akiachiwa pesa ya mboga ni za budget ya dagaa maharage na mchicha au mlenda na dagaa.

Mume akiwa na zamu ya kulala kwa bishost anampa pesa ile ile aaliyomuachia ni mdogo lakini shost ni mtoto wa mjin, akiachiwa ile pesa anapika mchicha baadae anakata kitunguu saumu na viungo vya pilau akisha kaanga harufu ikikolea anaepua. Nyumba haina ceiling board, mke mdogo anaona haya makubwa kumbe akilala kwa mkewe anatoa pesa ya pilau.

Usiku bishost anatufuata kama kuna aliyenunua khanga au kitenge amtolee upya, basi atavaa khanga mpya kama mume amelala kwake.

Mwisho wa siku bi mdogo kuomba talaka mwenyewe alimwambia mume kama unampenda mke wako uliniolea nini, yeye ndiye wa kula pilau na kuvaa khanga mpya?

Si kila ulionalo ni la kweli chungu za kwanza.
Wewe dada nakugawa bure [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeonaeee. Vitu ambavyo kuna sehemu havifanyiki ila uswahilini linakuwa jambo la kawaida
Saw kabisa..ila uswahilini huwezi kuwa na stress aiseeh..sema sasa unadumaa kiakili hakuna kitu utawaza cha miaka 10 ijayo.kwa ufupi unakuwa na mawazo mgando.
 
Watu wanashindwa kuelewa Nyumba zinastiri wengi mjini. Unaweza ukakuta mtu ananyumba kubwaa ndani kwake wanakula mchicha wa chukuchuku.
 
Sky Eclat na wengine muishio Kwamtogole, mimi ni jirani yenu nachoma chips, mihogo, na vinasaidiwa na chachandu maridadi kabisa pamoja na kachumbari ya maana.

Hii kachumbari ina vikorombwezo vyote, hiliki kidogo, chumvi kwa mbali na pia huwa nahakikisha kabeji inalainika kwa kuichemsha kidogo kabla ya kuichanganya na nyanya na vitunguu kufanya kachumbari kamili.

Nina kibanda changu kidogo pembezoni mwa barabara yetu kubwa ya Sokoni, bidhaa zote Napata kutoka katika soko letu la Nataka.

Nipo karibu kabisa na Rosten Pub na ABG.

Halafu aisee ile pilau ya Idd ilikuwa kabambe, hongera sana kwa ukarimu wako.

😀😀
 
Back
Top Bottom