Yaliyojiri bungeni Dodoma: Jumapili, 5 Julai 2015

Yaliyojiri bungeni Dodoma: Jumapili, 5 Julai 2015

Wakuu tupeni update mi niko kwenye foleni ya bvr mtu wa 30
Na natamani nijue kinachojiri huko domu

Mkuu tukupe nini hawajamaa badala ya kuchambuwa muswada na kuboresha wanaimba taarabu na mipasho.

Sasa ameingia Rage. Nayeye niyaleyale

Huyu msomari nishiida.
 
Wakuu tupeni update mi niko kwenye foleni ya bvr mtu wa 30
Na natamani nijue kinachojiri huko domu

Mkuu huko hakuna kitu cha maana endelea na shughurizako kaka.Muda huu anaongea Rage,kuna cha maana hapo unategemea?
 
Rage hajaanza bado kuchangia muswaada husika.
 
msiwe mnakurupuka kuanzisha uzi, hili jambo hata mimi tu nilikuwa nalifahamu, jana sheria ilitenguliwa ili iwaruhusu kufanya kazi jumapili na saba saba..... wewe labda ndo umepigwa hiyo chenga maana ulikuwa hujui
 
Hili bunge halina mvuto, huu uchangiaji unaonyesha ni maelekezo maalum
 
Wakuu tupeni update mi niko kwenye foleni ya bvr mtu wa 30
Na natamani nijue kinachojiri huko domu

yaani mkuu umeacha meza yako pale tanganyika stand kupoteza mda kujiandikisha?
 
Uk-4.
Waziri wa fedha kupewa mamlaka.

Teyari tunasheria je ile hatafanyakazi tena?
 
Mama spika ameendelea kuwa ngangari hata leo baada ya kuukataa muongozo uliombwa na Selasini na Halifa ambao wamesema hawakujutia makosa kama ilivyotamkwa jana. Na kwamba wamezalilishwa kwa kauli hiyo ya kamati. Selasin ameamua kutoka. My take; Makinda kajiandaa kuwamaliza wote mle ndani anatumia rungu la spika na amekuwa mbogo. Hata wapinzani wasiosimamishwa kama wataingia bungeni labda wachangie kikawaida wakitumia miongozo atawatoa nje.

Makinda anatekeleza matakwa ya waliomuweka hapo.
 
Huyu Rage mbona haelewiki mambo ya airtel tena!!!!
 
mleta mada ufahamu wake ni mdogo sana,suala la bunge kufanyika leo lilijulikana mbona,sheria ilitenguliwa na kuruhusu mjadala ufanyike,rudi kajipange upya,
 
msiwe mnakurupuka kuanzisha uzi, hili jambo hata mimi tu nilikuwa nalifahamu, jana sheria ilitenguliwa ili iwaruhusu kufanya kazi jumapili na saba saba..... wewe labda ndo umepigwa hiyo chenga maana ulikuwa hujui

Achana naye huyo mkuu,nafikiri atakuwa anatafuta KICK
 
nahisi wabunge wengi wa upinzani hawapo ndio maana kamera ni kwa ruge na mwigulu tu.
 
Watz tujilaumu wenyewe kufikiri siasa ni kama ushabiki wa Yanga na Simba. Watz sasa wajue kutokuwa na balanced bunge kwa maana ya chama tawala na upinzani ni kujiumiza wenyewe!
 
nashukuru sana mkuu kwa taarifa nilikuwa sijui kabisa kama kulikuwa na bunge leo.
 
Ngoja nikafanye shughuli zangu badala yakuangalia matutusa haya.

Aibuuuuuu.
 
Dianna Chilolo: Hakuna hata mbunge mmoja wa UKAWA aliyewahi kukaa bugeni kama Anna Makinda

Wanawake wakatae UKAWA kwasababu Spika Makinda amedharalilishwa kama mwanamke kwa kumuona hafai. wanawake wawasome namba UKAWA wawakatae.

Misaada imeletwa kwa hati ya dhararu, haina maana imekuja kwa ajali. Hati ya dhararu maana yake imepewa kipaumbele.

Wanataka wawekee uataratibu wazawa na wageni katika kuwekeza katika mafuta na gesi asilia. Miswaada 3 ni mizuri, ni mizito na ina masilahi kwa watanzania. Ameunga mkono hoja.

Ismail Aden Rage: UKAWA ni watoto wadogo Spika awasamehe Mungu atawaadhibu.

Wabunge walipelekwa kujifunza utaratibu wa mabunge ya commonwealth. UKAWA ni wepesi kushiriki mafunzo ya nje.

Nimesoma taarifa ya Law Tanganyika society. Miswaada ni mizuri imekuja wakati muafaka ipitishwe ili kuongeza uwajibikaji.

Nilimuhoji CE wa TPDC kwanini hataki kutoa mikataba gesi na mafuta. Kwasababu TPDC wanalinda interest za wawekezaji. Miswaada hii inaleta huo uwazi.

Airtel tangu imeanzishwa serikali haijapata gawiwo hata kidogo. Makampuni yatakayokuja yajisajiri kwenye soka la hisa la DSE. Ameunga mkono miswaada yote mitatu.
 
Back
Top Bottom