kweli ccm imeishiwa maana watu wenye akili nzuri wa kuitetea hawapo mpaka wanaokoteza hadi walevi
mashahidi wawili muhimu wa upande wa mlalamikaji hawa ngumbi wamegoma kuja mahakamani kutoa ushahidi hali iliyomfanya mlalamikaji kufunga ghafla ushahidi wake hapo jana. Wakili wa mlalamikaji issa mayige awali alisema kwamba wangeleta mashahidi wengine wawili hata hivyo muda wa mashahidi hao ulipofika alieza kuwa shahidi kutoka itv ameshindwa kupata ruhusu ya mwajiri wake. Kutokana na hali hiyo jaji upendo msuya alimtaka wakili wa mlalamikaji kufanya mawasiliano na mashahidi wake kupata uhakika iwapo watakuja mahakamani. Mlalamikaji hawa ngumbi na wakili wake walipiga simu kwa mashahidi hao na kurejea mahakamani na kueleza kuwa mashahidi hao hawawezi kuja mahakamani hivyo wameamua kufunga ushahidi. Kesi hiyo itaendelea tarehe 29 machi 2012 ambapo upande wa walalamikiwa utaanza kutoa ushahidi wake. Mlalamikiwa namba moja na namba mbili ambao ni ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali na tume ya uchaguzi wataanza kutoa ushahidi.
ni kitu gani hawa ng'umbi analalamikia katika hii kesi?
kwani JK hajampa madaraka huyu mama kama ukuu wa mkoa au hata wilaya au ubarozi??
alafu tukumbuke huyu mama alishapewa jukumu la ukuu wa wilaya ili asimamie sheria sasa unajiuliza hayo mazingira ya kazi huko alikokuwa yalikuwaje!!!hawa ng'umbi ni ************