Yaliyojili jioni hii mahakamani kati ya Mnyika vs Hawa Ngh'umbi

Lua

JF-Expert Member
May 19, 2011
704
305
YALIOJILI KATIKA KESI YA MH: JOHN MNYIKA VS HAWA NG’HUMBI
DAI LA KURA HEWA ELFU 15.
SHAHIDI WA HAWA NG’HUMBI.
Wakili; katika chumba cha majumlisho ya jumla, baada ya kumaliza kujumlisha kura vyama shiriki vinapata nakala?
Shahidi: Ndio wanapata.
Wakili: uchaguzi 2010 je vyama vilipata nakala?
Shahidi: ndio, na ni kwa chama changu.
Wakili: je nakala ulizotoa ni sahihi?
Shahidi: ndio, ni sehemu ya nakala
Wakili:huwa mnapewa copy au 0riginal?
Shahidi: tunapewa copy
Wakili: kwanini sasa hapa mahakamani umeleta photocopy badala ya copy ya original?
Shahidi: mi sijui labda umuulize wakili wangu.
Wakili: je kwy fomu ilizoleta mahakamni kuna wakala wa ccm?
Shahidi: ndio
Wakili:je una wasiwasi na wakala wa ccm?
Shahidi:sina wasiwasi
Wakili: anaonyesha fomu ambayo wakala wa ccm katika kituo amesaini. Je aliyesaini ni wa chama gani?
Shahidi: mi sijui sababu sikuwepo.
Wakili: ok
Wakili:je unaudhibitisho juu ya laptop unazodai mnyika amezingiza kwa ajili ya kuhesabia?
Shahidi:sina udhibitisho.
WAKILI WA MLALAMIKIWA.
Wakili: fomu ya matokeo inaonyesha wewe ukusaini, je unaidhibitishia vipi mahakama kama ulikuwepo siku ya majumrisho?
Shahidi: nilikuwepo na mimi nilipewa nakala.
Wakili: bado hujajibu swali, kwa maana hiyo hukuwepo na hayo maneno umeyatunga.
Shahidi; nilikuwepo na hata chama changu kinajua.
Wakili: ulisema mnyika aliingia na wafuasi wake zaidi ya nane, na uliwataja wanne tu, kama ulikuwepo taja na wengine waliobaki?
shahidi: wanatosha hao niliowataja.
Wakili: ulisema mnyika aliingia na wafuasi wake, je kati ya wewe na mnyika nani alianza kuingia ktk chumba cha majumuisho.
Shahidi: mnyika alianza.
Wakili:sasa ulionaje kama mnyika aliingia na wafuasi wake?
Shahidi: kuna baadhi walikuja baada na wengine ni kabla.
Wakili: ulisema wale waliongia walikua wanawazonga wasimamizi, je watu wa usalama hawakuwepo?
Shahidi: ndio walikuwepo.
Wakili: je ulikwenda kuwalalamikia kwa watu wa usalama?
Shahidi: sio jukumu langu.
Wakili: ni jukumu la nani?
Shahidi; msimamizi wa uchaguzi.
Wakili: mlipata bahati ya kuwepo kwa mkurugenzi wa uchaguzi [kiravu] kwa nchi nzima, je naye ulimlalamikia?
Shahidi: nilimlalamikia
Wakili: alikujibu nini?
Shahidi: hakunijibu
Wakili:je wale wafuasi wa mnyika walikua na shughuri gani?
Shahidi: kuwazonga wasimamizi
Wakili: je watu wa usalama hawakuwazuia?
Shahidi: ndio hawakuwazuia
Jaji: umeathiri vp matokeo?
Shahidi: kupatikana kwa kura hewa hizo elfu 15
Wakili: wakati wa kampeni ulisema ratiba ya tume ilikua haifuatwi, je ni kwa chama chako tu au na vingine?
Shahidi; vyama vyote
Wakili: unaushahidi gani kama vyama vingine havifuati?
Shahidi: ilishawahi kutokea kwa mgongano wa kuingiliana kwa mkutano maeneo ya mbezi kati ya ccm naa cdm
Wakili: nani siku hiyo alikua na ratiba ya mkutano kwa mujibu wa ratiba ya tume?
Shahidi; cdm
Wakili: je unajua idadi ya fomu ulizoleta hapa mahakamani unazolalamikia.
Shahidi: sio dai langu.
Jaji: aliingia jaji na kusema unapaswa kujibu sababu umeleta hapa mahakamani ni lalamiko.
Shahidi: sijui.
Wakili: moja kati ya kazi ya wakala wa ndani wa majumuisho ni kurekebisha kasoro zilizojitokeza kwenye vituo, ni kweli?
Shahidi: sio
Wakili: wakili akampa fomu asome sehemu ambayo inaelezea moja ya kazi ya wakala na hiyo aliyoisema wakili ipo.
Shahidi: mimi sijui hicho.
Wakili: je unajua tofauti ya kura kati ya mnyika na hawa ng’humbi?
Shahidi: sijui
Wakili: sasa uliwakilisha nini kama hujui?
Shahidi: na ndio maana sikusaini baada ya kuona madudu niliacha.
Wakili: je baada ya kuona kuna kasoro je ulijaza fomu za malalamiko?
Shahidi: hapana
Wakili: kuhusu mnyika kuingiza laptop zake na kuzitumia kwa ajili ya majumuisho, je zilikua ngapi?
Shahidi: tano
Wakili: je alizibeba mwenyewe?
Shahidi: ndio alibeba mwenyewe zote tano.
Wakili: je wakati mnyika anaingiza hizo je za tume zilikua mbovu?
Shahidi: hazikua mbovu, bali zilikua slow.
Wakili: wakati unajielezea mwisho ulisema matokeo yabatilishwe na uchaguzi urudiwe ni kweli?
Shahidi: ndio
Wakili: kwanini uchaguzi urudiwe na si kuhesabiwa tena kura za kwenye mabox, ambazo bado yapo hadi leo yameifadhiwa na tume na utaratibu huu upo?
Shahidi: siwezi kusema kura zihesabiwe wakati nilishasema uchaguzi urudiwe.
Jaji: jaji aliingilia kati na kumwambia shahidi ajibu swali na si maelezo.
Shahidi: sikujua kama utaratibu huo upo.
Wakili: sasa ushajua utaratibu huo upo wa kuhesabiwa kura tena kama kuna utata, je uko tayari?
Shahidi: nipo tayari.
Wakili: ok mh jaji mi nimemaliza.
Jaji: kuna shahidi mwingine
Wakili wa mshitaka: alipaswa kufika lakini hajafika hadi muda huu na hiyo ni kutokana na kuchelewa kupewa ruhusa.
Jaji: je kesho mna uhakika atakuja?
Wakili: ndio mh jaji. Mara wakili aliongea na mgombea [mlalamikaji] na kumpa taarifa wakili kuwa shahi wan ne hawezi kuja amekataa.
Wakili: akatoa taarifa kwa jaji
Jaji: je zaidi ya huyo kuna shahidi mwingine.
Wakili: hakuna, kwa maana hiyo tumefunga mashahidi kwa upande wetu. [mlalamikaji]
Kesi imehairishwa hadi tarehe 29/03/2012 saa tatu asubuhi, mahakama ya kazi iliyopo [akiba].
 
Jaji: kuna shahidi mwingine
Wakili wa mshitaka: alipaswa kufika lakini hajafika hadi muda huu na hiyo ni kutokana na kuchelewa kupewa ruhusa.
Jaji: je kesho mna uhakika atakuja?
Wakili: ndio mh jaji. Mara wakili aliongea na mgombea [mlalamikaji] na kumpa taarifa wakili kuwa shahi wan ne hawezi kuja amekataa.

Mpaka shahidi ameona kesi haina dili.
 
Wakili: kwanini uchaguzi urudiwe na si kuhesabiwa tena kura za kwenye mabox, ambazo bado yapo hadi leo yameifadhiwa na tume na utaratibu huu upo?
Shahidi: siwezi kusema kura zihesabiwe wakati nilishasema uchaguzi urudiwe.
Jaji: jaji aliingilia kati na kumwambia shahidi ajibu swali na si maelezo.
Shahidi: sikujua kama utaratibu huo upo.
Wakili: sasa ushajua utaratibu huo upo wa kuhesabiwa kura tena kama kuna utata, je uko tayari?
Shahidi: nipo tayari.
.
hapa ndo patamu....kesi kwisha, Ruling: ombi la mlalamikaji halifuati utaratibu wa kisheria wa tume
 
kwa ushaidi huo anaoutoa inaonyesha shaidi ajiamini vilevile ni aibu sana kwa shaidi wa nne kukataa kutoa ushaid inaonyesha jinsi mshitaki alivyokuwa anatafutiza mashaidi mwisho wa siku wamemtolea nje,na kuamua kufunga kesi.
 
kweli ccm imeishiwa maana watu wenye akili nzuri wa kuitetea hawapo mpaka wanaokoteza hadi walevi
 
Back
Top Bottom