Yaliyojili jioni hii mahakamani kati ya Mnyika vs Hawa Ngh'umbi

Huyu Hawa Ng'umbi awe mbunge wa nani alhali nilimkuta MSAKUZI akigawa rushwa nikamwambia hata kwa mawe na marungu huwezi kuwa MBUNGE. Hatuhitaji wabunge wa magamba UBUNGO akafie mbali na rushwa zake. Asubiri UKUU wa WILAYA maana msela atam-consider tu katika wilaya zake mpya za mikoa minne. KAFIE MBALI HAWA NG'OMBE

Hata hivyo si alikuwa ni mkuu wa wilaya wakati ule???
Mama huyu kuna wakati ililipotiwa kuwa ana hali mbaya kiafya na alipelekwa India, hivi alishapona??
 
Jamaa wa tume pia hawako makini. Inakuwaje matokeo ya uchaguzi yajumlishwe kwa wagombea wawili tu na wengine matokeo yao yasionyeshwe. Yaani ukifuatilia hata si kwa umakini sana utatambua kuwa this case is on the favour of CDM.
 
Hata hivyo si alikuwa ni mkuu wa wilaya wakati ule???
Mama huyu kuna wakati ililipotiwa kuwa ana hali mbaya kiafya na alipelekwa India, hivi alishapona??

Hawa Ng'humbi alishawahi kuwa Mkuu wa Wilaya. Pia kuna mama mwingine anaitwa Hawa Ngulume nae aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya na ndiye aliyekuwa mgonjwa kipindi fulani mpaka magazeti yakaandika habari zake. Hawa Ngulume nae ni "wale wale" ambao kiingereza ni cha kuokoteza kama cha Hawa Ng'humbi. Ngulume alipewa zawadi ya u-DC zama za Ben Mkapa, usichimbe sana CV yake maana unaweza kukata tamaa na kujiuliza kama kuna haja ya kuwa na ma-DC.

Kwa hiyo nahisi umechanganya ma-file. Huyu Mama mwenye kesi ni wale wajanja wajanja wa kutumia mgongo wa UWT na ndiko alikotuhumiwa ufisadi na ndiko alikopatia mihela ya kuhonga wakati wa kura za maoni. Kwenye kura za maoni alikuwa anamwaga njuluku kama hazina mwenyewe na ndio maana alimpiga dafrao Shamsa Mwangunga pamoja na u-Waziri wake. Kwa hiyo kwa kipindi kifupi sana asingekuwa choka mbaya kiasi hicho cha kukosa hela hata za kwenda Muhimbili kutibiwa.

Ndio maana wakati mwingine huwa nashindwa kuelewa, maana nikilinganisha upeo wa huyu mama na upeo wa Nape Nnauye na Mwangunga, nashindwa kujua ilikuwaje akawashinda kwenye kura za maoni? Siri ni kale ka-mchezo ka chama chetu makini ka kutumia njuluku kununua uongozi!
 
Jamaa wa tume pia hawako makini. Inakuwaje matokeo ya uchaguzi yajumlishwe kwa wagombea wawili tu na wengine matokeo yao yasionyeshwe. Yaani ukifuatilia hata si kwa umakini sana utatambua kuwa this case is on the favour of CDM.

Wakati mwingine Tume ya Uchaguzi huwa inaweza kuvuruga taratibu kwa makusudi na hasa kama wamekosa namna ya kuokoa jahazi ili kutoa mwanya wa kufungua kesi.

Kitu kama hiki kiliwahi kutokea kwenye uchaguzi wa 2005 jimboni Karatu. Dr. Slaa alishinda uchaguzi, then CCM wakafungua kesi ili kupinga matokeo, lakini washitakiwa walikuwa 2, Mwanasheria Mkuu na Msimamizi wa Uchaguzi. Lengo ikiwa ni kupeleka ushahidi hafifu ili matokeo yatenguliwe then uchaguzi uitishwe upya.

Dr. Slaa alipoona hilo changa la macho aliamua kuiomba Mahakama na yeye aunganishwe kwenye kesi kwa kuwa ana maslahi na kesi hiyo. So, na yeye akawa mlalamikiwa wa tatu. Kama Dr. Slaa asingeunganishwa basi ingekuwa imekula kwake na matokeo yangetenguliwa kilaini sana na uchaguzi ungerudiwa.
 
Ufafanuzi:
Wakili J- Wakili Mbogolo, wakili mtetezi kwa John John Mnyika
Wakili H- Wakili Maige, wakili wa mshati, Hawa Nghumbi
Wakili G- Wakili Mulokozi, Wakili mtetezi kwa serikali

Wakili J: Ieleze mahakama wewe ni nani?
Mnyika: John John Mnyika, miaka 31, mkristu, mkazi wa Sinza

Wakili J: Unafanya shughuli gani?
Mnyika: Ni mbunge, Mkurugenzi wa chama idara ya habari na uenezi Makao Makuu ya CHADEMA, Mwenyekiti CHADEMA kanda Kinondoni, DSM.

Wakili J: Ulishiriki vipi uchaguzi Mkuu 2010?
Mnyika: Nilikuwa mgombea niliyependekezwa na CHADEMA, na kuteuliwa. Nilishiriki katika kampeni kama mgombea lakini vile vile wakati wa kampeni nilikuwa Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA Taifa. Pia nililikuwa Katibu wa Timu ya Taifa ya kampeni ya CHADEMA. Nilikuwa mjumbe wa Kamati ya kampeni ya CHADEMA jimbo la Ubungo.

Wakili J: Wagombea walikuwa wangapi?
Mnyika: walikuwa 16

Wakili J: Matokeo?
Mnyika: Nilitangazwa mshindi

Wakili J: Lini na nani alikutangaza?
Mnyika: Nilitangazwa tarehe 02/11/2010 na Msimamizi wa Uchaguzi, Bwana Nduguru

Wakili J: Mlalamikaji anapinga ushindi na ametoa sababu tano. Tuanze, je kampeni zilikuwa zinaongozwa vipi na kuratibiwa?
Mnyika: Zilikuwa zinaongozwa na nyaraka mbalimbali. 1. Ratiba ya kampeni-ambayo ilikuwa inaonyesha nani anakuwepo wapi 2. Sheria- mbalimbali kama sheria katika uchaguzi 3. Maadili ya uchaguzi-ambayo nilisaini kama mgombea na yalikuwa yanatuongoza. 4. Maelekezo ambayo tume ilitupa wagombea na pia kutoa nakala kwa vyama vya siasa.

Wakili J: Ratiba ya kamepni iliandaliwa na nani?
Mnyika: Katika ndani ya ngazi ya chama kamati ya kampeni tuliandaa mapendekezo ya ratiba kasha tukawasilisha kwa msimamizi wa uchaguzi kwa maandishi. Msimamizi wa uchaguzi akaitisha kikao cha vyama vya siasa. Na baada ya kikao hicho Msimamizi akaleta kwa barua nakala ya ratiba ya kampeni. Ambayo mimi kama mgombea nilipewa nakala na chama vilevile.

Wakili J: Angalia nayaraka hii
Jaji: Ni nini?
Mnyika: Ratiba ya kampeni za uchaguzi manispaa ya Kinondoni.

Wakili J: Mwezi gani?
Mnyika: Septemba, 2010

Wakili J: Unakumbuka mratibu wa kampeni zako?
Mnyika: Ndiyo. Nilikuwa na waratibu wawili. Mratibu Mkuu ambaye tulikuwa tunamwita pia Mwenyekiti, anaitwa Eric Ongara na mwingine Ally Makwilo.

Wakili J: Shahidi alisema mlikuwa wapi Septemba 11, 2010?
Mnyika: Alisema nilikuwa na mkutano eneo la Riverside siku hiyo Septemba 11, 2010 jumapili

Wakili J: Ulitoa matamshi gani?
Mnyika: Nimesikia madai kuwa nilitoa matamshi kuwa yeye ni fisadi
Jaji: yeye nani?
Mnyika: yeye mlalamikaji Hawa Nghumbi ni fisadi kwa kuwa ana tuhuma za kuuza nyumba za UWT

Wakili J: alisema katika mkutano alikuwepo?
Mnyika: alisema hakuwepo ila aliambiwa

Wakili J: Aliambiwa na nani?
Mnyika: alisema aliambiwa na mwanachama wake ambaye alitaja jina hapa mahakamani Mheshimiwa Jaji.

Jaji: alitaja jina gani?
Mnyika: Sikumbuki ila alikuja kutoa ushahidi kama shahidi namba 2 Mheshimiwa Jaji

Wakili J: Unaiambia nini mahakama juu ya hayo?
Mnyika: Aliyosema si ya kweli. Tarehe 11/09/2010 sikuwepo Riverside. Nilikuwa katika mkutano mwingine ya hadhara; asubuhi Ubungo eneo la Msewe-Msikitini. Mchana mpaka jioni; nilihamia kata ya Saranga eneo la Stop-over. Na siku hiyo kwa kumbukumbu zangu ni siku ya jumapili na si jumamosi kama ilivyodaiwa hapa mahakamani mheshimiwa Jaji.

Wakili J: Shahidi #2 alisema ulianza kwa kufanya nini?
Mnyika: Kadiri ya maelezo yake nilianza kwa kutangaza nia ya kugombea ubunge. Na baadae nikaelezea sababu ya kugombea. Baadae akaendelea kutoa maelezo mgombea wa CCM asichaguliwe kwa sababu ni fisadi kutokana na tuhuma kushiriki kuuza nyumba UWT.

Wakili J: Unaielezaje mahakama juu ya hayo?
Mnyika: Maelezo yaliyotolewa na shahidi juu ya mimi kutangaza nia. Maelezo hayo yanadhihirisha kuwa shahidi husika hakuwa akihudhuria mikutano yangu ya kampeni toka kanpeni zilivyoanza rasmi. Kwa sababu mimi nilitangaza nia ya kugombea ubunge mwezi Machi, 2010. Nilitangaza kupitia vyombo vya habari, mkutano ya hadhara na taarifa hiyo nilisambaza katika mitandao ya kijamii kwa maana ya kupitia internet. Rekodi hizi zipo. Hivyo, sikuwa na sababu mwezi wa Septemba baada ya kuwa nimeshapendekezwa na chama na nimeshakwisha kuteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi na nipo katikati ya kampeni kutangazia wananchi nina nia ya kugombea ubunge ambao nilikuwa nagombea tayari.

Wakili J: mlalamikaji anasema kutokana na kauli hiyo ilipelekea kushindwa
Mnyika: Kwanza sijazitoa kauli hizo. Sikuwepo. Pili, iingie kwenye kumbukumbu ya mahakama yako tukufu Mheshimiwa Jaji mwaka 2010 nilikuwa nagombea kwa mara ya pili. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2005 ambapo kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na tume nilipata kura zaidi ya elfu 45. Pia iingie katika kumbukumbu jimbo la Ubungo ndilo jimbo lenye wapiga kura wengi kuliko jimbo jingine lolote Tanzania, wapiga kuwa laki nne na hamsini elfu.

Wakili J: Mahakama ielewe nini wapigakura lakinne na hamsini elfu.
Mnyika: Ielewe kuwa katika kampeni zenye siku 90, zenye kufanywa kwa mikutano katika mitaa mingi ndani ya kata zilizopo kwenye jimbo, mkutano mmoja ieleweke si rahisi kuathiri matokeo.

Wakili J: Hii tuhuma ya kuuza nyumba za UWT ulipata kuisikia?
Mnyika: Ndani ya kumbukumbu zangu Mheshimiwa Jaji, nilipata kuisikia. Mosi, kabla ya kampeni wakati wa kura za ndani za CCM, walikuwa wanatuhumiana wao kwa wao. Na iliandikwa na moja ya vyombo vya habari. Pili, nilisikia moja kwa moja Agosti 28, 2010 wakati mimi na mlalamikaji tukiwa katika kipindi cha mchakato majimboni kilichokuwa kinarushwa moja kwa moja na TBC1, mmoja wa wananchi waliohudhuria alimuuliza swali mlalamikaji Hawa Nghumbi, alimuuliza swali kuhusiana na tuhuma hiyo. Nikawa nimeisikia tena kwa mara nyingine. Na …

Wakili J: Unakumbuka nini?
Mnyika: Nakumbuka aliahidi kwa kurudia mara mbili kwamba atamshtaki aliyetoa tuhuma.

Wakili J: Hapa mahakamani una kumbuka nini juu ya madai hayo alisema?
Mnyika: Hapa mahakamani alisema, hakumshtaki mpaka sasa kwa kuwa alisema madai si ya kweli hivyo akayapuuza.

Wakili J: Mahakama ielewe vipi kuhusiana na tuhuma hizo?
Mnyika: Ningependa mahakama irejee kwenye ukweli kwamba madai yake mimi nilikuwa tarehe 11 Septemba, 2010 siku ya jumapili nilikuwa Riverside nikatoa tuhuma. Na ukweli nilioeleza sikuwapo Septemba 11, 2010 Riverside. Na pia haikuwa siku ya Jumapili kama ilivyodaiwa hapa mahakamani Mheshimiwa Jaji na mlalamikaji na ukweli tuhuma zote hizo zilisemwa kabla ya tarehe hiyo na hakuchukua hatua zozote kuhusiana na hizo tuhuma. Na kwamba kama angekuwa na malalamiko dhidi yangu katika kampeni, wote tulisaini maadili ya uchaguzi. Na maadili hayo yalimpa fursa ya kuwasilisha malalamiko. Nasikumbuki kupewa malalamiko. Hivyo hakutumia fursa hiyo. Pia mkutano mmoja hauwezi kuathiri matokeo kwani kampeni zilifanyika kuanzia Agosti mpaka ukomo wake Oktoba.

Wakili J: Juu ya Majumuisho ya kura. Majumuisho yalifanyika lini?
Mnyika: Tulianza mchakato wa majumuisho Oktoba 31, 2010. Na nasisitiza neno tulianza "mchakato". Usiku wa tarehe 31 saa sita kasoro mimi na wakala wangu tulienda Loyola baada ya kupewa barua. Tulipofika, tuliambiwa tunaanza kupokea matokeo na masanduku.

Jaji: Ulienda na mawakala wako?wangapi? nani?
Mnyika: Mmoja, Bwana Eric Ongara

Mnyika: Nilifika tukakuta eneo la kukaa mawakala. Nikakuta mawakala wengine. Tukaelezwa zoezi la kuhesabu litaendelea, tusubiri kuendelea kupokea vifaa na tukawepo pale usiku mpaka usiku wa manane. Baadae nikatoka na kumwacha wakala wangu.
Jaji: Kwa hiyo ulikuwepo kushuhudia kupokea vifaa?
Mnyika: Ndiyo mheshimiwa Jaji. Na nikatoka baadae nikamwambia wakala wangu anijulishe zikibaki kata chache ili nirudi.
Jaji: asubuhi saa ngapi?
Mnyika: 01/11/2010 around saa nne nikaambiwa nirudi. Nikapokea fomu chache zilizobakia.

Wakili J: Majumuisgho yalianza saa ngapi?
Mnyika: Saa tano asubuhi ndipo majumuisho yalianza Mheshimiwa Jaji.

Wakili J: Ulikuwepo?
Mnyika: Mimi nilikuwepo Mheshimiwa Jaji.

Wakili J: Ulifika na nani?
Mnyika: Mimi nilifika nikiwa mikono mitupu. Na wakala wangu alikuwa tayari ndani.

Wakili J: Umemsikia shahidi yeye alifika saa ngapi?
Mnyika: saa 3 usiku siku ya 01/11/2010

Wakili J: Kati ya wewe na yeye nani alimtangulia mwenzake?
Mnyika: Mara zote yaani 31/10/2010 na 01/11/2010 mimi niliwahi kumtangulia.

Wakili J: Ametoa tuhuma nzito sana, unakumbuka ulisema nini?
Mnyika: Nilikuja na wafuasi nane. Nikiwa nimebeba laptop 5 nimezibeba kwa kuzikumbatia.

Wakili J: laptop?
Mnyika: Madai hayo si kweli mheshimiwa Jaji. Haiwezekani mtu niliyeingia kabla yake awe aliniona nimeingia na laptop. Lakini ukweli wakala wangu Eric Ongara alikuwa na laptop. Huu ni ukweli.

Jaji: Alikuwa na laptop ngapi?
Mnyika: alikuwa na laptop moja mheshimiwa Jaji.

Wakili J: Vipi kuhusu mawakala wengine?
Mnyika: Nilikuta mawakala wengine. Hao walikuwa na laptop. Alex Mayunga wa AFP, alikuwa na laptop na laptop ya wakala wa CHAUSTA anayeitwa Michael John. Nazikumbuka laptop hizo. Tulipoketi, kulikuwa na waangalizi toka kituo cha Haki za Binadamu (LHRC), simkumbuki jina. Kulikuwa na mwangalizi wa Tanganyika Law Society (TLS), John Seka. Hawa waangalizi walikuwa na laptop wanatumia.

Wakili J: Laptop zilikuwa zinatumikaje?
Mnyika: Ni zungumzie mimi na wakala wangu namna alivyokuwa anatumia. Kura zilipigwa kwenye vituo, matokeo yakatangazwa kwenye vituo. Mawakala katika vituo wakapewa nakala ya fomu za matokeo vituo 1013. Sisi kwenye kamati yetu ya kampeni.

Jaji: Walipewa lini?
Mnyika: Wote walipewa 31/10/2010 ila mida ilikuwa imetofautiana. Ila ilipofika saa nne usiku. Tulikuwa na nakala za matokeo ya vituo. Tulipokwenda saa sita kasoro tulikwenda na fomu za matokeo. Wakala wetu aliweza kwenda na watu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi sambamba katika kuhakiki, sisi tulikuwa tunatumia laptop yetu ambayo haikuwa na programu kama yao. Kituo kikiingizwa katika majumuisho nasi tuliingiza katika laptop kujumlisha kadiri ya wakala na taarifa tulizokuwa nazo.

Wakili J: Hivyo hiyo ndiyo kazi ya laptop ilikuwa nayo?
Mnyika: Ndiyo

Wakili J: Mdai anasema ulipika matokeo hewa kwa matumizi ya laptop yako
Mnyika: Nimeeleza awali Mheshimiwa Jaji, matokeo awali yalitangazwa katika vituo. Huwezi kupika matokeo bila kuwa na fomu mbadala na ushahidi mbadala. La pili, laptop ya wakala wangu Mheshimiwa Jaji haikutumiwa na Tume. Hivyo isingeweza kupika matokeo

Wakili J: Sheria inataka wajumlishe kwa njia gani?
Mnyika: Kwa uzoefu wangu wa kisheria kwa kushiriki katika chaguzi na nyaraka za uchaguzi. Hakuna maelezo ya kifaa gani kitumike. Kinachoelezwa katika sheria na maelezo ya vyama kwa wagombea. Msimamizi wa Uchaguzi anapaswa kutaja kwa sauti kura ili wote waweze kujumlisha. Upande mmoja wa nukuu yaani Tume, pia wengine wenye uwezo wa kujumlisha ili waweze kuhakiki ujumlishaji wa matokeo kwa wagombea. Hatua hii ilifatwa pia Loyola.
 
Kama inavyosemwa hapa kila siku hapa JF, hakuna kesi hapa watu wameamua kuchezea fedha za umma ambazo zingeweza kuelekezwa katika kuboresha huduma za kijamii lakini wao wameamua kuzichezea.
 
Kama inavyosemwa hapa kila siku hapa JF, hakuna kesi hapa watu wameamua kuchezea fedha za umma ambazo zingeweza kuelekezwa katika kuboresha huduma za kijamii lakini wao wameamua kuzichezea.

hii inaonyesha ni jinsi gani CCM na wabunge wao pamoja na mahakama ambazo zipo chini ya CCM zinavyojivua na kujiweka uchi mbele ya watanzania walio wengi! Kweli hii ni misuse ya mipesa ya walal hoi!
 
...mwisho wa ubaya ni aibu...kila la kheri Myika na kumbuka kwamba..."PALIPO NA MWANGA GIZA HALIKAI"...
 
Mbowe aliwahi kusema akichangia kwenye hotuba ya budget ya Wizara ya mambo ya ndani 2010/2011 kwamba kuna wananchi wengi wanakosa haki zao kwakuwekwa mahabusu bila kufikishwa mahakamani kutokana na uhaba wa mahakimu na majaji lakini pia hawa majaji waliopo hawatumiki ipasavyo na hili ndo linajidhihirisha kwa uwazi kabisa.
 
Mbowe aliwahi kusema akichangia kwenye hotuba ya budget ya Wizara ya mambo ya ndani 2010/2011 kwamba kuna wananchi wengi wanakosa haki zao kwakuwekwa mahabusu bila kufikishwa mahakamani kutokana na uhaba wa mahakimu na majaji lakini pia hawa majaji waliopo hawatumiki ipasavyo na hili ndo linajidhihirisha kwa uwazi kabisa kwenye hii kesi yakubuni.
 
Duuuuh hawa Ng'umbi aibu hii utaificha wapi ndugu yangu!!!!!!!


Ona sera za CCM!!!!!!!!!
Nipigeeeeeeee Nisipigeeeeeeee????????????????????
Pigaaaaaaaaaaaa
Bendera ya CCM ina rangi ganiiiiiiiiiiiiii???????????????
Kijaniiiiiiiiiiiiii.
Ukipanda mahindi yanaota rangi ganiiiiiiiiiiiii???????????
Kijaniiiiiiiiiiiiii.
Ukipanda mpunga unaota rangi ganiiiiiiiiiiiiii???????????
Kijaniiiiiiiiiiiiiiii
Migomba yote ina rangi ganiiiiiiiiiii?????????????
Kijaniiiiiiiii.
Piga makofi na vigelegele kwa Chama cha Mapinduzi.
CCM Oyeeeeeeeee.
Oyeeeeeeeeee.
 
Back
Top Bottom