Yaliyo nikuta kwenye daladala

Yaliyo nikuta kwenye daladala

Mkuu tatizo wewe ulikomaa kumcheki mzee akiingia mmu badala ya kumtupia maneno mazuri ya kimahaba kwa mtoto ndo maana kachukia kiasi hicho. Kwanini usimsemeshe wakati yupo karibu yako? Ina maana hujatambua uzuri wake ndo maana kalipuka kama moto
 
Habari

Ipo hivi jana nilikuwa nimetoka zangu kinondoni narudi home kimara- suka nilipofika usalama nikaanza kutafuta daladala ya kwenda suka kama ww mwenyeji wa dar utakuwa unajua usafiri wa kwenda mbezi usiku unavosumbua sijazoea kugombania daladala lakini baada ya kukaa sa 1kituoni bila kupata gari ikabidi nikubaliane na hali halisi ya kugombania,ikaja daladala ambayo ilikuwa inaishia suka ndipo nilipo amua kuingia hvyo hvyo bila kujali.

Kiukweli tulikuwa tumebanana sana hakkuwa na namna sababu ilikuwa kama sa 2 usiku inaenda sa 3 nilisimama usawa wa kiti ambacho dada mmoja mweupe alikuwa kakaa hapo kwa jinsi tulivyo banana niliamua kugeukia kutazama dirisha sasa mkono mmoja ulipita juu ya kichwa cha yule dada na nikashika nguzo ya dirisha mkono wa kulia ukashika kiti kilicho kuwa mbele ya yule dada na hata gari ingedunda vipi nisingeweza kumgusa.

Nilizubaa mbele kumuangalia mzee mmoja ambae alikuwa na smartphone huawei kilicho fanya nizubae kuangalia ile simu ni kuwa yule mzee alikuwa kama wa miaka 55 hadi 60 hivi lakini nilishangaa kuona aki click JF application na kufika hadi kwenye jukwaa la MMU na kufungua.

Lakini nilishindwa kuona ni uzi gani aliufungua kwani nilishutuliwa na vibao viwili vya mkononi kutoka kwa yule dada na akanza kuongea we kaka vipi unataka kunitoboa macho utanizaa ukinifanya nikiwa kipofu alinifokea sana bila kuelewa kosa langu ni lipi na akanivyonza sana hata mama angu mzazi hajawahi nifokea vile abiria wote walishikwa na butwaa kuona yule dada alivyo kuwa akinifokea na kuongea maneno yasiyo na hekima nilipandwa sana na hasira nikashindwa kuongea hata sikumjibu kitu nilimwangalia usoni kama dakika 1 hivi nikajisema moyoni malipo ni hapa hapa duniani.

Ndipo abiria wakanza kumsema yule dada na kumuonya kuacha hiyo tabia

Yule mzee wa MMU alikuwa mstari wa mbele sana kumsema yule dada sijui anatumia ID gani humu ningemtaja lakini bila shaka huu uzi anausoma na atakuwa shahidi wa kile kilicho tokea na kuja kushuhudia hapa nilipenda san alivyo mpa makavu yule dada lengo langu lilikuwa ni kufika manzese nishuke kwa hasira nilizo kuwa nazo lakini sikushuka kwa jinsi abiria walivyo mshambulia yule dada akiwepo mzee wetu wa humi MMU nilimsikia akisema ndo maana yeye kamua kumuozesha binti yake kwa laki 2 kwasababu ya tabia za ajabu za akina dada walizo nazo na kuhofia isije siku wakachana afu akashindwa kurudisha mahali.

Mzee najua unanisikia please njoo uwe shahidi wa haya bahati mbaya kimara mwisho yule mzee alishuka.

Inaniuma sana kwa alichonifanyia yule dada sitamsahau leo hadi kesho kwanini anifanyie vile mm binadamu mwenzake,mimi nilimkosea nini kama alikuwa hataki kubanwa kwanini alipanda daladala ni kujiona au nini inaniuma sana nyie akina dada sijui nani ali walaani.

Eeeh Mungu baba msamehe kwani halijui alitendalo

Mbona unalalamika kwa unyonge sana? We mwanaume bwana hayo mambo madogo
 
Pole sana mkuu ina maana mkono wako ulikuwa sawa na msumeno au misumari?

Kuna baadhi ya wanawake hawana adabu kabisa! Umetumia busara ya hali ya juu kumuacha na kunyamaza! Huo ndio uanaume!

Ingawa nilikuwa na hasira za kumpga hata kofi lakini niliamua nisijibu chochote hadi mwisho wa safari angu
 
Pole sana. Ila mbna unakaa mbali hvyo? Hamia makumbusho au kijitonyama. Huko utakutana na mikasa kila siku. Maana mm rafiki yangu aliamua kumkunja dada mmoja na kumpa vibao kabisa.

Alimkosea nini wana dharau sana wengi wao kumbe wote maisha magumu tuuu
 
Pole watu wapi kimwili tu akili zao zipo mbaaali sana! Pia hujaibiwa maana watu wajanja sana anakukoromea ukiwa washangaa kumbe pana mtu anakwibia hapo haha!

Nilipo ona daladala ni zakugombania walet na simu vyote niweka kwenye begi langu la mgongoni mfukoni sikuwa na kitu kma mpango wake ulikuwa huo alishindwa
 
Kumbe... Sasa sijui babu yupi huyo wa MMU aje tumpongeze
^^

Huwenda atakuja alikuwa alivamiaa jukwaa yeye ni wa katiba na siasa sijui lakini kwa maneno alio kuwa anampa yule dada anaonekana ni mwongeaji sanaaa
 
Mkuu tatizo wewe ulikomaa kumcheki mzee akiingia mmu badala ya kumtupia maneno mazuri ya kimahaba kwa mtoto ndo maana kachukia kiasi hicho. Kwanini usimsemeshe wakati yupo karibu yako? Ina maana hujatambua uzuri wake ndo maana kalipuka kama moto

Siwezi kbsa kumsemesha mtu tukiwa kwa gari tumejaa vileee sijui lakini yy alikuwa na mawazo ganii
 
ndio maana mimi huwa natembea na upup.u kwa ajili ya vizabizabina kama hao...

ukinichokoza tu kwenye daladala kama huyo mdada lazima nikupulizie wa mgongoni...
 
Alimkosea nini wana dharau sana wengi wao kumbe wote maisha magumu tuuu

Dada alisema kuwa jamaa anambambia kwenye makalio. Si unajua haya mambo ya kubanana . sasa dada akaanza kumletea noma gari zima anaongea yeye tu. Jamaa akamaindi akamkamata akamtia vibao.. Ikatokea tafrani pale tukaizima kiaina ila dada keshapokea vibao
 
Ingawa nilikuwa na hasira za kumpga hata kofi lakini niliamua nisijibu chochote hadi mwisho wa safari angu[/QUOTE
Usije kufanya kosa la kupiga ukifikiri ni suluhu hata siku moja! jifunze kupuuza wala watu kama hao hawatakusumbua! Maana unaweza kupiga na ukapata case ya mauaji kuna wengine wanatembea ni wagonjwa!
 
ungemtia dole la jicho kabisa,hapana kuharibiana mood kwa hisia tu...pole sana mkuu
 
kijana mimi nilijitahidi kukutetea kwenye daladala halafu unakuja kunizalilisha huku MMU? kumbuka tulipofika Tip Top nilijaribu kukupunguzia hasira juu ya huyo binti, uzuri nimekushika sura nitakukamata tu na utajuta kukaa Dar es saalam.
 
Habari

Ipo hivi jana nilikuwa nimetoka zangu kinondoni narudi home kimara- suka nilipofika usalama nikaanza kutafuta daladala ya kwenda suka ,ikaja daladala ambayo ilikuwa inaishia suka ndipo nilipo amua kuingia hvyo hvyo bila kujali.








nilipenda san alivyo mpa makavu yule dada lengo langu lilikuwa ni kufika manzese nishuke kwa hasira nilizo kuwa nazo lakini sikushuka kwa jinsi abiria walivyo mshambulia yule dada



Ulikua unaenda Suka??
Mbona lengo likawa kushukia manzese?
 
Back
Top Bottom