Yale maji ndani ya nazi nani kayaweka?

Yale maji ndani ya nazi nani kayaweka?

Yanawekwa na mnazi wenyewe, ambao ni moja ya mimea yenye kutunza maji mengi toka ardhini. Hayo ndiyo msaaada mkubwa wa kukua mche baadaye.

Mnazi unasambaza maji na ndiyo maana sehemu ile ya kubebea nazi, wagemaji wanakata na kufunga kopo. Wanakinga majimaji ya mnazi hayohayo.

Tena wakija kuyatoa kwenye kopo yana harufu ila ladha kama maji ya dafu tu. Shida yakilala tu baada ya kushushwa ni pombe

Maji hayohayo yanayokuwa kwenye nazi ni kitu muhimu sana katika uotaji wa mche mpya. Kama ilivyozoeleka mbegu zingine huwa zinafukiwa zioze ndiyo ziote. Nazi huwa huwa haifukiwi huweka juu kwenye udongo ikiwa haijaondolewa maganda. Unaichanja kidogo karibu na eneo ambalo huwa na kikonyo sehemu ambayo itakuwa juu.

Kupitia maji yake itatoa mzizi ambao utakita kwenye ardhi na mche ambao utatoka na kuja juu. Ndiyo mnazi mpya huo.
 
Back
Top Bottom