Yako wapo mapenzi?

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,835
2,659
Nimekaa nikawaza kidogo na kujiuliza hili swali. Yawezekana yaliyonisababishia kuwaza haya nimeyapitia jana, juzi, miezi kadhaa, ama miaka kadhaa nyuma.

mapenzi ya wawili waliokutana kwa bahati. Waliotafutana kwa mikiki na visiki vingi hadi wakawa pamoja. Nazungumzia yale mapenzi yaliyokuwa machanga enzi hizo. Yapo? Yako wapi sasa? Yale mapenzi ya kulishana kama njiwa. Ya kuwaziana mema mwanzo mwisho. Ya kuhofia kuachana. Ya kugandana kama kumbikumbi.

Hivi huyo uliye naye ndiye yule aliyekufanya kukosana na wazazi wakati fulani?
Ndiye yule aliyekufanya roho ipae ukimwona?
Ndiye yule aliyekufanya roho ipasuke ukisikia jina lake?
Ndiye yule aliyekusababishia kuwa mnadhifu wakati wote?
Ndiye yule aliyekujazia tabasamu usoni na moyoni wakati wote?
Ndiye yule aliyekupa ganzi ya hisia usisikie wala kuona?
Ndiye yule ambaye harufu ya manukato yake ilikutikisa kwa mahaba?
Ndiye yule miezi/miaka michache nyuma mlipeana ahadi zisizotekelezeka?
Ndiye yule ambaye mlikaa enzi hizo mkapanga familia yenu iweje? Imekuwa?

Ndiye yule? kama ndiye yule una kheri. Kama siye, kabadilika nini? Nini kimembadili? Wakati fulani tunatamani kurudisha wakati nyuma japo tuonje tone la yale tuliyopitia katika ulimwengu wa mapenzi. Inashindikana. Kwa nini inashindikana? Chanzo cha kushindikana ni nani? Kuna jambo au mambo yaliyochangia nyie kufikia hali mliyo nayo (kuachana ama kuwa na uhusiano wa mashaka). Pengine unajua sababu. Pengine mnashangaa kwa nini mmefika hapo.

Ulishawahi kumuuliza, 'hivi kwa nini tumefika hapa, mpenzi wangu?' Kwa nini hili litufikishe hapa? Nimebadilika nini? Sikuvutii tena? Siamshi hisia zako kama awali? Nini kimesababisha tufikie hapa? Ni watoto? Ni ndugu? Ni ukapa? Kuna msaidizi wangu huko nje? Ni nini basi? Yako wapi yale mapenzi? au ni utu uzima?

Kwa nini tuishi kwa mazoea?
Kwa nini faraja yangu iwe watoto pekee? Kwa nini isiwe wewe tena?
Kwa nini faraja yangu iwe marafiki zangu?
Kwa nini faraja yangu iwe pombe?
Kwa nini faraja yangu iwe ni kuchelewa kurudi nyumbani?
Kwa nini faraja yangu iwe hawara?
Kwa nini faraja yangu isiwe wewe tena?

Najua mpo mnaokumbana na haya. Hitimisho la simulizi hii ni wewe kuchukua hatua kwa kadiri inavyostahili, ukiakisi katika wakati uliopita. Kipidi kile mnakesha kwenye mbalamwezi mkiimbiana mashairi mazuri na kulisha ndimi. Leo zimekuwa chungu? Muulize, je, unakumbuka?
 
Daahhh
maswali ni mengi
Hayo..

Nway yule
alienifanya niruke
dirisha usiku hayuko na mimi
Sasa..Naamini mapenzi ya
kipindi kile ni tofauti sana na ya sasa.

Na inasababishwa
na sababu mbalimbali
za maisha ..

Saa nyingin e mie naona ni
Borea ku move on na maisha kuliko
kuwaza je ningekuwa na fulani ingekuwaje
Sasa.. shukuru kwa uliye naye na kama huna omba
na tafuta kwa juhudi utapata..
 
Watu wanabadilika pia sababu mbalimbali za kimaisha ndio maana kuna SUMMER, WINTER, SPRING na AUTUMN
 
raia fulani, ulichoandika kimeugusa moyo ,asante ni thread nzuri.
ni vizuri sana ikiwa wapenzi/wanandoa mna kawaida ya kujitafakari kila mara kwa maswali haya na kuyapatia ufumbuzi basi nina hakika mahusiano hayawezi kufa hata siku moja ,japo mawimbi na upepo havikosekani kwenye mahusiano.
 
raia fulani, ulichoandika kimeugusa moyo ,asante ni thread nzuri.
ni vizuri sana ikiwa wapenzi/wanandoa mna kawaida ya kujitafakari kila mara kwa maswali haya na kuyapatia ufumbuzi basi nina hakika mahusiano hayawezi kufa hata siku moja ,japo mawimbi na upepo havikosekani kwenye mahusiano.
 
Daahhh
maswali ni mengi
Hayo..

Nway yule
alienifanya niruke
dirisha usiku hayuko na mimi
Sasa..Naamini mapenzi ya
kipindi kile ni tofauti sana na ya sasa.

Na inasababishwa
na sababu mbalimbali
za maisha ..

Saa nyingin e mie naona ni
Borea ku move on na maisha kuliko
kuwaza je ningekuwa na fulani ingekuwaje
Sasa.. shukuru kwa uliye naye na kama huna omba
na tafuta kwa juhudi utapata..
Ubarikiwe Sana
 
Nadhani sasa imefika wakati tubadilishe vyeti vya ndoa na kuweka mambo kazaaa hazarani ukijua ukikiuka tutaenda kwa talaka. disclaimer agreement hivi kila upande ujue hivi manake hii karne ya sayansi na tekinologia inaleta changamoto nyingi sasa hasa hasa na visimu vya mikononi jamani sms ni raisi sana kupata mtu wa kukuokoa schoolmate,rafiki, mnaofanyakazi nao na usiache visemina. Ukikosewa tu na sms na moyo unapona
 
raia fulani, ulichoandika kimeugusa moyo ,asante ni thread nzuri.
ni vizuri sana ikiwa wapenzi/wanandoa mna kawaida ya kujitafakari kila mara kwa maswali haya na kuyapatia ufumbuzi basi nina hakika mahusiano hayawezi kufa hata siku moja ,japo mawimbi na upepo havikosekani kwenye mahusiano
kuna mawimbi mengine makali usipokuwa makini yanazamisha meli

 
Daahhh
maswali ni mengi
Hayo..

Nway yule
alienifanya niruke
dirisha usiku hayuko na mimi
Sasa..Naamini mapenzi ya
kipindi kile ni tofauti sana na ya sasa.

Na inasababishwa
na sababu mbalimbali
za maisha ..

Saa nyingin e mie naona ni
Borea ku move on na maisha kuliko
kuwaza je ningekuwa na fulani ingekuwaje
Sasa.. shukuru kwa uliye naye na kama huna omba
na tafuta kwa juhudi utapata..
lakini bado ukireflekt bak kuna mengi ambayo unayakosa. Mwisho wa siku life must go on responsibly
 
lakini bado ukireflekt bak kuna mengi ambayo unayakosa. Mwisho wa siku life must go on responsibly

Ni kweli
Kabisa mpendwa
cha kufanya sasa nikuchua
mazuri yote ya hapo zamani za kale
Na kujaribu kurekebisha kilicho
endas wrong..

Maana hatuwezi kurudi nyuma
kama mimi niliyempenda
kipindi kile anafamilia yake sasa..
nikumwombea mema..
Na ku move forward..
 
Back
Top Bottom