fredmlay
JF-Expert Member
- Apr 30, 2008
- 1,849
- 388
ritz kikao kilikuwa na mambo mengi ya kujadili. Kuna ile ahadi aliyotupa Dr. Slaa hapa kwamba kamati zitaketi na kutuambia ni nini waliongea na Rais baada ya mikutano yao miwili. Hii taarifa haijawahi kutoka na ni matumaini yangu kuwa sasa itatolewa. Pili tukiambiwa kuna Kamati inachambua wajumbe wa Tume ya katiba na CDM itatoa taarifa; nadhani hili nalo litatolewa taarifa kwa umma. Na sasa hili la uwajibikaji wa serikali ambalo naona Zitto amejinyakulia nukta nyingi na kuna watu walitamani liwe la kichama zaidi na liwakilishwe na KUB lakini naibu KUB si kwa hicho cheo bali kama mbunge akatumia Ubunge wake kulisimamia. Hili limempandisha Zitto kwenye chati givyo itabidi na wengine waje na single zao. Kumbuka Zitto alipokuja na hoja ya posho mwingine akaja na hoja ya kukataa gari la KUB. Timing tu hapa.
Ukweli ni kwamba hapa jamvini Zitto kapanda chati zaidi lakini kwa umma wa watanzania walio wengi wanakipongeza CDM, wanajua kila mbunge hufanya kazi ya chama ya kusafisha uozo, kukemea serikali, kufichua uozo nk.
Kwa viongozi, wananchi wanaangalia ujasiri wa mmoja mmoja wakiamini kwamba pamoja na malengo ya chama, mengine yanataka ujasiri kuyatekeleza maana katika utekelezaji kuna kuumizwa na vyombo ya utawala wa serikali yetu dhalimu, ila bungeni hilo halipo hivyo inakuwa rahisi kutekeza malengo ya chama bila woga wowote.
Last edited by a moderator: