Yako wapi Maamuzi ya Kikao cha CHADEMA?

Wakuu kweli kabisa CDM imefanya kikao lakini hakuna hata chembe ya habari toka huko ndani? Sijui habari za Botilo lakini hili la kutaka taarifa ya jinsi wabunge walivyoisimamia serikali ili hali kuna mchakato wa kutaka kupeleka hoja ya kutokuwa na imani na PM kidogo nilishtuka.

mkuu kwani mbunge kila anachofanya bungeni lazima kiwe na baraka za chama.?kama ni hivyo mbona hata mwenyekiti mbowe alisain.? Lakini tusiongee sana labda ni uzushi tu kila kitu kiko sawa.!
 
we ni mpuuzi kuna uhusiano gani kati ya tittle ya thread yako na ulichoandika!!Mod imefika muda watu kama hawa tuwe tunawatukana tu na msitupige ban limtu linakurupuka tu sijui limevimbiwa makande afu linaanzisha thread kama hii kwakweli yanakera.
 
Ubishi hausaidihi CDM ni chama na kinaongozwa na watu na siku zote kujadiliana jambo na kutofautiana ndani ya vikao vya chama ni kawaida viongozi wa CDM si miungu kiasi kwamba wasitofautiane, inawezekana ikawa kweli msibishe tu jamani cha msingi ni kumuomba tu mungu hali hiyo isijetokea ikavuruga chama!
 
Ubishi hausaidihi CDM ni chama na kinaongozwa na watu na siku zote kujadiliana jambo na kutofautiana ndani ya vikao vya chama ni kawaida viongozi wa CDM si miungu kiasi kwamba wasitofautiane, inawezekana ikawa kweli msibishe tu jamani cha msingi ni kumuomba tu mungu hali hiyo isijetokea ikavuruga chama!
Good point.
 
Kazi ipo Tz!! Akina Botilo jitahidini sana kupunguza sukununu vichwani mwenu!!
"ukimuombea mabaya mwema unamuongezea rehema za Mwenyezi Mungu!!"
 
Hoja ya zito kumtk wzr mkuu kujiuzulu haikuwa na baraka za chama zito alkw anahoji mamlaka ya Slaa kudai hayo more updates soon kuna kichwa kule ndani ndo kimenibonyezea hii kwanza

Kama ilikuwa haina baraka ya chama,mbona mwenyekiti aliiunga mkono na kuitetea kwa nguvu pia wanachadema wote bungeni kusaini petition?
Hiyo habari yako ni grapevine.
 
Kama mi mwongo subirini na make kitako kusikia mtokoto uliotokea sijui mtakimbilia wapi mpasuko upo mkubwa tuu!tuache ushabiki hali si nzuri baada ya kikao kuvunjika
Kwa jinsi ulivyo, kama hili lingekuwa hivyo ungeshalianzishia thread badala ya kumjibu mwingine.
 
Kama ilikuwa haina baraka ya chama,mbona mwenyekiti aliiunga mkono na kuitetea kwa nguvu pia wanachadema wote bungeni kusaini petition?
Hiyo habari yako ni grapevine.

Mkuu wasingesaini wasingeeleweka mbele ya macho ya Watanzania. Hii kitu imempa umaarufu Zitto na kuna watu roho zinawanyongorota. Zitto aliwalia timing na kuweka hoja hadharani hivyo isingekuwa rahisi kuizuia hadharani. Katika siasa kuna wakati mnakuwa hamko pamoja lakini hadharani mnajifanya ni wamoja.
 
mwenye hizi data origino atupe tusikae kulumbana tu bali kujenga chama
 
Hoja ya zito kumtk wzr mkuu kujiuzulu haikuwa na baraka za chama zito alkw anahoji mamlaka ya Slaa kudai hayo more updates soon kuna kichwa kule ndani ndo kimenibonyezea hii kwanza

Intelijensia feki ya UWT na Lumumba
 
Acha walumbane, wagombane, wapigane na kutoana ngeo lakini mwisho wa siku Watanzania tunataka mabadiliko. Na mabadiliko yenyewe tumeshindwa kuyapata ndani ya CCM hivyo wakigawanyika na kuacha kuwa wamoja watakuwa wanaendelea kutuchelewesha.
Inshu kubwa ni "patient" people are not patient, they think its their right to say something and be followed without any justification to the oponents within their group. CDM are very potential now, sasa hii ya kutoelewana haina mashiko lazima kama kuna manung'uniko yawekwe sawa hata kwa kuvunja vikao na kupandishia hasira then mnarudi tena na kuelewana.
 
Kikao kimekosa maana mara baada ya CC ya CCM kutoa tamko la kusudio la JK la kufanya mabadiliko yenye TIJA kuwatosa mawaziri na watendaji serikalini waliofisadi mali za umma
 
Inamaana akina zitto hawaioni hii watujuze ata kidogo!

Ila inawezekana ata kikao kuvunjika kwani chadema sio malaika inawezekana kupishana ila uzuri wanabusara kwenye maamuzi.

Namjua Zitto anakiburi lakini hana msimamo. Hajawai ata kuoa anataka uraisi hujaongoza ata familia anataka nchi.
 
Kikao kimekosa maana mara baada ya CC ya CCM kutoa tamko la kusudio la JK la kufanya mabadiliko yenye TIJA kuwatosa mawaziri na watendaji serikalini waliofisadi mali za umma
Mafilili in action, actually stupid action!
 
Botilo ni kama mama shangingi. Umbea usiovumilika. Kwa taarifa yako mimi ni mjumbe wa kikao kile, hayo yako sijui umeyapata wapi? Labla unauliza. Sina mamlaka ya kutoa maazimio ya kikao kwenye media, ila mengi ni siri sidhani kama wahusika watatoa yote.
 
Tumaini Makene tuletee maamuzi ya kikao.

ritz kikao kilikuwa na mambo mengi ya kujadili. Kuna ile ahadi aliyotupa Dr. Slaa hapa kwamba kamati zitaketi na kutuambia ni nini waliongea na Rais baada ya mikutano yao miwili. Hii taarifa haijawahi kutoka na ni matumaini yangu kuwa sasa itatolewa. Pili tukiambiwa kuna Kamati inachambua wajumbe wa Tume ya katiba na CDM itatoa taarifa; nadhani hili nalo litatolewa taarifa kwa umma. Na sasa hili la uwajibikaji wa serikali ambalo naona Zitto amejinyakulia nukta nyingi na kuna watu walitamani liwe la kichama zaidi na liwakilishwe na KUB lakini naibu KUB si kwa hicho cheo bali kama mbunge akatumia Ubunge wake kulisimamia. Hili limempandisha Zitto kwenye chati givyo itabidi na wengine waje na single zao. Kumbuka Zitto alipokuja na hoja ya posho mwingine akaja na hoja ya kukataa gari la KUB. Timing tu hapa.
 
Last edited by a moderator:
acha unafiki hata kama unapewa posho na magamba! hali si nzuri labda kwenye familia yako ,mchumia tumbo ww.
 
Back
Top Bottom