Drjacka92
JF-Expert Member
- Jul 20, 2016
- 445
- 522
Salaam!!.
Kiukweli Chumvi ni bidhaa ambayo inatumika kwakiasi kikubwa karibu kila siku Katika vyakula vyetu binadamu.
Lakini watu wengi wanafahamu tofauti nauhalisia na jinsi inavyotengenezwa. Wengi wanajua eti kwamba chumvi inachimbwa ardhini kama yanavyochimbwa madini mengine lakini ukweli haupo hivyo.
Ajabu nikwamba Chumvi hutengenezwa kwakutumia Maji ya Bahari tu hayaongezwi kitu kingine chochote. Madini joto katika chumvi huwekwa kipindi ambacho chumvi imeshakamilika kutengenezwa.
Maji huvutwa kutoka baharini nakuanikwa Katika makalo maalumu yaliyoandaliwa, maji huwekwa Katika makalo hayo kwamuda usiopungua mwezi mmoja, nahiyo hufanyika msimu wa jua Kali, kadri maji yanavyopigwa na jua huongezeka kiasi chaukali wa chumvi Katika maji Yale ya bahari, (kitendo hicho huitwa kuongezeka Point Katika maji) hivyo kila siku maji hayo hupimwa kwakutumia Hydrometer, kadri point zinavyoongezeka Yale maji yanaganda nakuwa chumvi.
Chumvi huvunwa baada yakukomaa, nahapo hufuata zoezi lakuiosha chumvi. Chumvi huoshwa kwa maji makali yenye kiasi kikubwa cha point ya chumvi, ikioshewa maji mazuri yasiyo nachumvi huyeyuka kabisa.
Chumvi ya unga unaweza kuipata shambani kipindi chumvi haijakomaa nakuwa kama jiwe, lakini pia husagwa kiwandani baada ile ya mawe kutoka shambani.
Kilimo cha chumvi hutegemea sana Jua, kipindi cha mvua chumvi haizalishwi nahuwa adimu sana, kwawauzaji wa chumvi wanatambua uadimu wake kipindi cha mvua.
Hayo ni machache tu, kama unaswali lolote kuhusu Chumvi niulize, kama unataka ufanye biashara ya chumvi nitakueleza pia, au kama unataka uanzishe shamba la chumvi nitakupa maelekezo zaidi.
Kazi njema.