Yahusu wafufuao wafu na misukule

Yahusu wafufuao wafu na misukule

Kuna makanisa ya Kweli na ya uongo sio kwamba yote matapeli and the Word is widely straight-out unabii unatimia wa nyakati za mwisho.
 
Kuna makanisa ya Kweli na ya uongo sio kwamba yote matapeli and the Word is widely straight-out unabii unatimia wa nyakati za mwisho.

Up sahihi chongchung na post hii imelenga hayo ya uongo
 
Last edited by a moderator:
Nendeni mkasali huko kwenye hayo makanisa msichunguzechunguze. La sivyo kuweni waislamu....
 
Naona yakhe umerukia mada nyingine !
Hii lugha imetumika mpaka ndani ya Biblia.
Soma kitabu cha 'Mwanzo' utakuta lugha kama: .......na tuumbe mtu kwa mfano wetu.
Yakheee upo ?

Asante kwa kusadiki katika Utatu Mtakatifu. Mungu Baba Mungu Mwana Mungu Roho Mtakatifu. Mungu akubariki. Kila ulumi utamkiri Bwana...
 
Na manabii na mitume wenyewe ni wajanja wanapeleka makanisa yao kwenye mzunguuko wa hela kama Dar,Mwanza na Arusha

Me nawasubiri walete hukuuu mtwara kama hawata kuwa ombaombaa au iringa kwetu uwiiiiii
 
Una ushaaid kuhusu mh gwajima?au uwezo wa kufikiri umegota?nataka kujau ukweli tuh
 
Hiyo yakutuma sadaka niliona Kenya, nilikwenda kumuona rafiki yangu Nairobi akanambia wao wanatuma hela kwa njia ya simu halafu wanaambiwa kutakua na maombi saa kadha ukamate TV ufungemacho uombewe,nilishangaaa sana lakini sikutaka kumkera sababu alikua serious na wanamuamini sana huyu mchungaji,nikaishia kujiuliza maswali mwenyewe nikajijibu mwenyewe..

Ningekuwa mimi hera sitowi na nashika TV nioneee....
 
Una ushaaid kuhusu mh gwajima?au uwezo wa kufikiri umegota?nataka kujau ukweli tuh

Jichagulie Jibu kama wewe ni mfuasi wake na pia Jichagulie jibu Kama wewe si mfuasi wake
 
It is you who don't read the Bible, but people who are informed are doing it. Hereunder is the impeccable proof.

Matthew 10:8 Heal the sick, raise the dead, cleanse those who have leprosy, drive out demons. Freely you have received; freely give.

You use verses on your favour. But what i know pastors use witchcraft to get deciples.
 
Hili jambo miaka mitatu nyuma lilikuwa maarufu sana, yaliibuka makanisa ya mitume na manabii kwa kasi ya ajabu yaliyokuwa kila wakati yakituonyesha picha za wafu waliokufa kimazingara na baadae kufufuliwa nao.

Karata hii isiyo na chembe ya haya wala soni ya udanganyifu ikawapatia waumini wengi na umaarufu mkubwa.

Gwajima bingwa wa haya mazingaombwe kwa kujiamini kabisa aliutangazia uma wa waumini wake kuwa angemfufua Marehemu Amina Chifupa RIP, watu wakausubiri kwa hamu muujiza huu, Chifupa mpaka leo hajafufuka.

Maumivu yalibaki kwa mtoto wake na ndugu zake ambao jina la ndugu yao lilitumika kwa malengo binafsi huku magazeti ya udaku yakiwa kichocheo kikuu

Watu wote tuliowaona wakifufuliwa hatujawahi kuonyeshwa ndugu zao na historia zao, sijawahi kuona mtu wa Dar akifufuliwa au mtu ninayemfahamu, bali mtu wa dar alifufukia Arusha, wa mwanza alifufukia dar nk.

Upofu wa imani ukawafanya wengi wakimbilie kwenye haya makanisa, lakini sasa mambo yamebadilika na uongo wao umejulikana! Siku hizi kufufua misukule sio dili tena, kilichopo ambacho nacho kinakufa ni kutoa mapepo! Hivi mapepo yanakaa kwa akina mama tuuu!?

Imani ni kitu kizuri pale tu unapojitambua kuwa unaamini nini na kwa nini! Hawa manabii na mitume wa uongo wamechuma Mali nyingi kwa waumini wapumbavu! Serikali iliangalie hili kwa makini yasije kutokea yaliyotokea Uganda, Kenya na ulaya kule watu waliojiuwa kwa maelfu kwa maagizo ya viongozi wao wakiamini kwa kufanya hivyo watakwenda peponi.

Wewe kama hiwaamini mitume na manabii ni uamuzi wako, lakini maandiko ya Biblia yanaonesha watakuepo mpaka Yesu arudi, swala la kufufua wafu na kurudisha misukule unayo haki ya kutoamini lakini biblia inasema kufufua wafu ni moja ya ilani ya Yesu, hivyo anapotokea anayeamini anaitekeleza, hivyo mimi sioni ajabu mtu kufufua wafu si kwa sababu ya miujiza yenyewe bali kwa kuwa ahadi hiyo ilishatolewa miaka 2000 iliyopita
 
Back
Top Bottom