Yahusu wafufuao wafu na misukule

Yahusu wafufuao wafu na misukule

Serikali sikivu imekaa kimyaa....huu ni Utapeli kabisa! mama lwakatale alishatapeli kufufua wafu,serikali kimyaaaa
 
turashashe jr;
"... Siamini ka ingekuwa ni jengo tu la ile dini nyingine ya majambia limetajwa tu humu hii thread ingekuwa ina endelea"

Hebu tufafanulie ni dini ipi hiyo ya majambia, nyambafu wewe!!

Dogo 1;
Sina haja ya kukufafanulia ni ipi kwani tayari wameshaanza hao hao kina Dogo kurusha mapovu. Sikuitaja tayari weshajishuku. Ndo maana nkamwambia turashashe kuwa ingelikuwa ndo dini hiyo kaitukana kihivyo cha moto angeshakiona. Sijaitaja tayari matusi mwaaa ningeliitaja. Aksanteni kwa kujilinda kwa mijitusi ka hiyo yako
 
Mna MIUNGU wangapia YAKHE?

Naona yakhe umerukia mada nyingine !
Hii lugha imetumika mpaka ndani ya Biblia.
Soma kitabu cha 'Mwanzo' utakuta lugha kama: .......na tuumbe mtu kwa mfano wetu.
Yakheee upo ?
 
Hili jambo miaka mitatu nyuma lilikuwa maarufu sana, yaliibuka makanisa ya mitume na manabii kwa kasi ya ajabu yaliyokuwa kila wakati yakituonyesha picha za wafu waliokufa kimazingara na baadae kufufuliwa nao.

Karata hii isiyo na chembe ya haya wala soni ya udanganyifu ikawapatia waumini wengi na umaarufu mkubwa.

Gwajima bingwa wa haya mazingaombwe kwa kujiamini kabisa aliutangazia uma wa waumini wake kuwa angemfufua Marehemu Amina Chifupa RIP, watu wakausubiri kwa hamu muujiza huu, Chifupa mpaka leo hajafufuka.

Maumivu yalibaki kwa mtoto wake na ndugu zake ambao jina la ndugu yao lilitumika kwa malengo binafsi huku magazeti ya udaku yakiwa kichocheo kikuu

Watu wote tuliowaona wakifufuliwa hatujawahi kuonyeshwa ndugu zao na historia zao, sijawahi kuona mtu wa Dar akifufuliwa au mtu ninayemfahamu, bali mtu wa dar alifufukia Arusha, wa mwanza alifufukia dar nk.

Upofu wa imani ukawafanya wengi wakimbilie kwenye haya makanisa, lakini sasa mambo yamebadilika na uongo wao umejulikana! Siku hizi kufufua misukule sio dili tena, kilichopo ambacho nacho kinakufa ni kutoa mapepo! Hivi mapepo yanakaa kwa akina mama tuuu!?

Imani ni kitu kizuri pale tu unapojitambua kuwa unaamini nini na kwa nini! Hawa manabii na mitume wa uongo wamechuma Mali nyingi kwa waumini wapumbavu! Serikali iliangalie hili kwa makini yasije kutokea yaliyotokea Uganda, Kenya na ulaya kule watu waliojiuwa kwa maelfu kwa maagizo ya viongozi wao wakiamini kwa kufanya hivyo watakwenda peponi.
Hatari sana
 
Wakinamama wanatia aibu fuatilia kwa makini ndoa nyingi zimevurugika kisa mambo hayo mama anaacha familia anaenda kulala kanisani mambo gani hayo ni shidaaaa
 
Wamekosa msingi na malezi mazuri ya kidini! Hawa ni wavivu wa kusoma neno na kulitafakari hawa ni wale wanao subiri kufanyiwa kila kitu wakichukua shortcut ya miujiza na baraka za kunjunga
 
Hili jambo miaka mitatu nyuma lilikuwa maarufu sana, yaliibuka makanisa ya mitume na manabii kwa kasi ya ajabu yaliyokuwa kila wakati yakituonyesha picha za wafu waliokufa kimazingara na baadae kufufuliwa nao.

Karata hii isiyo na chembe ya haya wala soni ya udanganyifu ikawapatia waumini wengi na umaarufu mkubwa.

Gwajima bingwa wa haya mazingaombwe kwa kujiamini kabisa aliutangazia uma wa waumini wake kuwa angemfufua Marehemu Amina Chifupa RIP, watu wakausubiri kwa hamu muujiza huu, Chifupa mpaka leo hajafufuka.

Maumivu yalibaki kwa mtoto wake na ndugu zake ambao jina la ndugu yao lilitumika kwa malengo binafsi huku magazeti ya udaku yakiwa kichocheo kikuu

Watu wote tuliowaona wakifufuliwa hatujawahi kuonyeshwa ndugu zao na historia zao, sijawahi kuona mtu wa Dar akifufuliwa au mtu ninayemfahamu, bali mtu wa dar alifufukia Arusha, wa mwanza alifufukia dar nk.

Upofu wa imani ukawafanya wengi wakimbilie kwenye haya makanisa, lakini sasa mambo yamebadilika na uongo wao umejulikana! Siku hizi kufufua misukule sio dili tena, kilichopo ambacho nacho kinakufa ni kutoa mapepo! Hivi mapepo yanakaa kwa akina mama tuuu!?

Imani ni kitu kizuri pale tu unapojitambua kuwa unaamini nini na kwa nini! Hawa manabii na mitume wa uongo wamechuma Mali nyingi kwa waumini wapumbavu! Serikali iliangalie hili kwa makini yasije kutokea yaliyotokea Uganda, Kenya na ulaya kule watu waliojiuwa kwa maelfu kwa maagizo ya viongozi wao wakiamini kwa kufanya hivyo watakwenda peponi.

katika maisha haya , kuna rundo la binaadam wenzetu ni kama mizigo nchini. hata wao wanajijua kwamba ni mizigo. mshana jr sijui kama unajijua kwamba wewe ni kati ya mizigo, tena mizigo kwelikweli.

Taifa letu tunapiga mbiu ya kusonga mbele, kuna baadhi ya raia WENZETU ni mizigo, wanaifanya nchi yetu iwe nzito, wanapenyeza maujingajinga yao kwenye imani, siasa na uhuru wa mtu na mtu. bahati mbaya sana ni watu walio shindwa kimaisha, wako choka mbaya, hata akili zao zimechoka. WASAMEHEWE NA KUPUUZWA
 
Last edited by a moderator:
Hiyo yakutuma sadaka niliona Kenya, nilikwenda kumuona rafiki yangu Nairobi akanambia wao wanatuma hela kwa njia ya simu halafu wanaambiwa kutakua na maombi saa kadha ukamate TV ufungemacho uombewe,nilishangaaa sana lakini sikutaka kumkera sababu alikua serious na wanamuamini sana huyu mchungaji,nikaishia kujiuliza maswali mwenyewe nikajijibu mwenyewe..

Siku hizi watu wameanza kufahamu ukweli na kurudi kwenye makanisa yao ya mwanzo yasiyo na mbwembwe nyingi na yenye utaratibu thsbiti
 
katika maisha haya , kuna rundo la binaadam wenzetu ni kama mizigo nchini. hata wao wanajijua kwamba ni mizigo. mshana jr sijui kama unajijua kwamba wewe ni kati ya mizigo, tena mizigo kwelikweli.

Taifa letu tunapiga mbiu ya kusonga mbele, kuna baadhi ya raia WENZETU ni mizigo, wanaifanya nchi yetu iwe nzito, wanapenyeza maujingajinga yao kwenye imani, siasa na uhuru wa mtu na mtu. bahati mbaya sana ni watu walio shindwa kimaisha, wako choka mbaya, hata akili zao zimechoka. WASAMEHEWE NA KUPUUZWA

Hapa jiwe lililorushwa gizani lilitua penyewe. ..matokeo yake yakawa tamko la hamaki bila kuzingatia hoja na uhalisia
 
Last edited by a moderator:
Kuna kipindi niliona kama kanisa ni duka huru ambalo hudaiwi mapato serikalini na cha ajabu zaidi kumbe wengi wamejiegesha tuu wanafanya biashara ya kuuza unga usiopikiwa ugali wala uji, huu ni msiba mkubwa kwa ndugu zetu wasio na imani thabiti. Nakumbuka kipindi fulani nilienda Kwa tafiki yangu napiga hodi haitikii redio ndiyo inanguruma kipindi kikiwa ni cha maombi ambayo hurushwa na kituo kimoja cha redio kule arusha nikasema labda katoka kidogo nikachukua jukumu la kumsubiri nilishangaa kuona akitokea ndani baada ya kuisha Kwa kipindi nilipata masikitiko zaidi kuniambia samahani nilikuwa naomba pamoja na radio duh! Kumbe alipiga simu redioni akapewa maelekezo ya kutuma sadaka kiasi chochote atakacho kuwa nacho halafu ashike radio maombi yamuingie aloo! Nilijichokea nikajua huko Kwa mungu kutakuwa na maigizo siku ya kiama kwakweli shop church inalipa sana kuliko hata kununua Gari la biashara
 
Ugumu Wa maisha ndio unaleta yote hayo plus kuchanganyikiwa
 
Wakinamama wanatia aibu fuatilia kwa makini ndoa nyingi zimevurugika kisa mambo hayo mama anaacha familia anaenda kulala kanisani mambo gani hayo ni shidaaaa

Tatizo hili kwa akina mama halitaweza kuisha,hii ni kutokana na namna walivyoumbwa;wao ni wepesi sana wa kupokea mambo pasipo kufanyia tafiti za kina.
 
Umenikumbusha mchungaji mmoja mwaka 2010 alikuja kwa mzee Wangu apate dawa za mvuto na kuwa na nguvu ktk kanisa lake tena alikuja na wanasiasa 2 ni maalufu sana hapa mjini

basi mzee wangu akawambia kazi zao zote zinafanyika usiku maeneo ya makabulini kunduchi ilipofika usiku wa saa sita tukaenda wote nikiwemo na Mimi mwenyewe..

Basi kufika makaburini ikanyunyizwa dawa kwenye makaburi 2 ya dini yake yakasemwa maneno flani pale ya lugha maalum. Mara yakafunguka ukatoka moto mkubwa sana ukiambatana na radi nusra jamaa wakimbie, basi tukaona watu wanatoka mle na kuuliza kwa lugha ileile aliyoongea mzee wangu,

akawatajia Shida za wale jamaa wote watatu wakaambiwa wavue nguo pale pale wasogee, basi wakafanya kama walivyoelekezwa na wale watu wakaanza na yule mchungaji kwa nguvu alizokuwa anataka akapewa ila kwa makubaliano maalumu, na wale wengine ambao mmoja ni mbunge maarufu wa upinzani na mwingine sasa ni waziri wakafanyiwa vile walivyoomba, kazi ikawa imekwisha.

Mchungaji ana kanisa bagamoyo road linajaza huwa nawaonea huluma waumini mana wanaabudu wasichokijua na nikikutana nae nikumtania mana najua nguvu sio ya mungu yeye huniambia namshukulu malehemu mzee wako nisingekuwa tajiri kama sio yeye
Haka ni kauongo katamu.
 
Back
Top Bottom