Yahusu Mabalozi wa kuhamasisha kodi

Yahusu Mabalozi wa kuhamasisha kodi

Nanyaro Ephata

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2011
Posts
1,237
Reaction score
1,828
Niliwahi kuandika kuhusu huyu Waziri wa Fedha anajiitaga mchumi wa daraja la kwanza! Huyu ni miongoni mwa mawaziri ambao ni mzigo kwa Watanzania!

Leo Bwana Mwigulu akiwa Bungeni amewatangaza watu watatu kuwa mabalozi wa kodi, Mobeto, Samata na Edo Kumwembe. Sasa twende taratibu, tatizo la kodi Tanzania ni tatizo la mfumo wa kodi wenyewe, tatizo ambalo waziri na timu yake walipaswa kulitatua kwanza!

Kodi haitalipika kwa HAMASA wala kuwa na MABALOZI bali kwa kuondoa kero kwa wafanyabiashara. Kodi italipika kwa kuongeza wigo wa walipa kodi. Kodi italipika kwa kuweka mazingira rafiki ya ulipaji kodi. Hapa lazima serikali itekeleze wajibu wake kimsingi Serikali imeacha wajibu wake wa kuongeza wigo wa walipa kodi badala yake hata wale wachache imeshindwa kuwalinda.

Kila kona machinga wanauza bidhaa na hawalipi kodi leo uniambie Samatta /Hamisa atawasihi waliofungiwa biashara zao na machinga walipe kodi?

Serikali inapaswa kuweka mazingira rafiki ya kuanzisha zaidi SMe ili kupanua wigo wa walipa kodi!pia ipunguze mlolongo na utitiri wa kodi ambazo hugeuka mzigo kwa mlipa kodi,badala yake kuwepo na kodi zinazolipika

Cosmetic solution haiwezi kuwa suluhisho,kuwa na mabalozi sio suluhisho unateua Balozi ambaye hajawahi kulipa hata milioni TRA au hajui hata huo mlango wa TRA unafananaje

Wizara ya fedha iache mzaha ndani ya TRA kuna kitengo cha elimu ya mlipa kodi,kitengo hiki kifanye kazi yake kitalaam,kiache kuishi zama za kale

Kama ni lazima sana kuwa na balozi wa kulipa kodi basi Waziri alipaswa kutafuta walipakodi wakubwa ndio wawe mabalozi
 
Nasikia rais ramaphosa wa south Africa amemteua Mohammed dewji kua mshauri wake wamaswala ya uchumi.kwanini sisi tunashindwa kuteua watu wa kada ya mo kuwa wa shauri wetu wa maswala ya uchumi?.
 
Huyu waziri angetafuta wasomi weledi wa kodi ambao wana uwezo wa kuelezea maana halisi ya kodi na umuhimu wake pamoja na faida za mwananchi kulipa kwa taifa ikiwa ni pamoja na kuweka mifumo wezeshi na rafiki kwa mlipa kodi , sasa hawa wateule siwapondi ila wameteuliwa ahawana makosa kwa kuwa wameteuliwa ila hawana ujuzi wala hawajui nini maana ya kodi na hamasisha yao haina tija yoyote kuongeza wingi wa kodi.
 
Huhitaji PhD,Mwigulu ni TATIZO.
Amekiri TRA wananuka rushwa,hajatatua tatizo hilo amekimbilia mabalozi.
Kimsingi hakuna mtanzania asiyejua umuhimu wakulipa Kodi.tatizo ya janjajanja inaanzia kwenye mfumo wa TRA.

Swali ni lini atatangaza mabalozi wakuwaelimisha watumishi wa hazina wanaojilipa kuaandaa mpango kazi na yeye yupo ofisini kimya.
HAO MABALOZI NI NJIA YA TEN PERCENT YAKE.
 
Wizara ya fedha iache mzaha ndani ya TRA kuna kitengo cha elimu ya mlipa kodi,kitengo hiki kifanye kazi yake kitalaam,kiache kuishi zama za kale....!!!

Unajua tazanzani tuna wasomi wengi wasioelimika!
 
Nasikia rais ramaphosa wa south Africa amemteua Mohammed dewji kua mshauri wake wamaswala ya uchumi.kwanini sisi tunashindwa kuteua watu wa kada ya mo kuwa wa shauri wetu wa maswala ya uchumi?.
Sisi tumemteua hamisa mobeto
 
Back
Top Bottom