kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 17,943
- 17,359
Kodi lazima ilipwe na watu wote wa dini zote, makabila yote na hata mashabiki wa timu zote.
Inafahamika kuwa taifa la Tanzania limegawanyika kati ya wanaume na wanawake, wakristo na waislam na pia mashabiki wa Simba na Yanga. Hii inamaanisha kuwa kwenye jambo la kitaifa usiingize jinsia, ukabila, udini wala ushabiki wa simba na yanga.
Cristine Mwagala msemaji wa timu ya TRA alisema ni heri kufungwa na Simba kuliko kufungwa na Yanga, na kweli walifungwa na Simba magoli 3 kirahisi kabisa. Hii maana yake wanainajisi kazi ya timu ya TRA ya kuhamasisha watanzania wote kulipa kodi zao.
Timu hii ya TRA lazima ibaki neutral kati ya Simba na Yanga ili lengo la TRA kumiliki timu liwe na maana kwenye kuhamasisha kulipa kodi; ilipaswa iwe ni timu ya watanzania wote, inayopendwa na watanzania wote. Hali ilivyo sasa itachukiwa na wanayanga wote ambao ni zaidi ya nusu ya walipakodi Tanzania.
TRA lazima imfukuze kazi Cristina Mwagala na viongozi wengine ambao walikuwa Tabora United kwakuwa bado wana fikra zilezile za Tabora United ambazo zina malengo tofauti na TRA ya sasa. Wanaendesha timu kwa bifu badala ya kuwaleta walipakodi pamoja.