Yahusu kuchanjiwa muku

Mambo ya kuchanja machale ni Ushirikina unajikabidhi kwa miungu itakayokutaabisha miaka yote!
 

Dawa hiyo yaitwa MAVUNE. ni hatari sana haya mambo. sisi wadigo wa Tanga tuliyaona haya mambo kwa wazee wetu, na kama kuna mtu anafikiri kuwa hizi ni fix tu anajidanganya au nikama alivyosema mshana kuwa ukiwa umezaliwa muhimbili, ukasomea azania na chuo udsm na sasa unatumbuliwa jipu bandarini huwezi kuyajua haya makitu hata sekunde.

Tanga kuna sehemu alikuwepo babu yetu aliitwa MWAGAUWA, huyu mzee alikuwa hatari sana, aliishi maeneo ya maramba kwa mbele kidogo sehemu inaitwa bwiti. Hao wazee walikuwa wanatisha na hakuna mjusi kuleta jeuri katika koo hizo. mizizi ilikuwa inasemewa ikavimba na kisha ikasemewa ikasinyaa bila yakutiwa maji wala ndimu.

Wanaume walikuwa wanatembea usiku mchana, kifua wazi hakuna cha panya road wala panya railway. ukigusa utapasuka mwenyewe. Madawa haya yaliwafanya watu wazalishe chakula cha kutosha mashambani na wawe na uwezo mkubwa wakufanya shuguli zinazohitaji nguvu hasa na waliweza pia kutembea umbali mrefu bila kuchoka.
 
Inaitwaga kinkuti hyo ya kuwa na mwili mgumu kuna jamaa angu nimesoma nae kigoma alikua nayo hyo kitu sema ilikua inamtesa sana kuna muda ilikua mwili unakakamaa hawez hata simama mpk mumpe dawa fulani ukimmwagia anapona.
Halafu akaongeza nyingne inaitwa tani hiyo anasema unaweza kupotea ukikimbizwa ukikata kona tu watu hawakuon tena. Test alizamishwa mto lueche ndan na mganga for hrs pia akapigwa panga mgongo hamna kitu kapigwa gobore risas mgongon kikatokea kimchubuko kidogo. Kwel dunia inashangaza sema alivunja mashart akamchokoza bwenn jamaa mmoja hv alizibuka haaaaaahaa havikumsaidia. Kwel dunia inashangaza sana hyo technology ipo kigoma imetokea congo naskia
 
Nilishawahi sikia kuwa kuna watu kama anaumwa yuko ndani ya nyumba atakama ana hali mbaya kiasi gani hawezi kufa mpka watoe bati mwanga upite ndo anakufa, hiyo ndo muku mkuu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…