Mlalahoi,
Ukiwa na bondia wako na unajua ni dhaifu, utaendelea kumpeleka kwenye ulingo bila kumuandaa ipaswavyo kisa ni lazima apigane tuu? Je akipigwa mpaka kuzimia na akizinduka kisaikolojia akawa amedhoofika utaendeleza mbinu na mazoezi yale yale ambayo yalimfanya ashindwe pambano la kwanza hata la saba?
Nimekosoa ile soft approach ya kutotaka kutoana ngeu na CCM, ile soft approach ya kuogopa kunyimwa Ruzuku au mgao wa fedha. Nimewasihi Chadema watunishe msuli kwa kila jambo kila mwaka wa bajeti na kila kisichoeleweka na wasiridhike na kauli nyepesi nyepesi au ahadi mbofumbofu.
Lakini bado wameendelea kuburuzwa na barudhuli CCM, ndio maana nauliza na nakubaliana wakishinda then what ikiwa wao wako defensive na hata wakishinda ushindi wao hautakuwa na nguvu za kutosha kuwaweka kando CCM wasiharibiwe fursa yao ya kutawala?
Sisi kama Taifa, matokeo ya kupata Uhuru tukiwa wachanag tumeyaona, leo hii mkoloni karudi kiulaini kwa mikopo, misaada na uwekezaji. Leo uwezo wa kujitawala hatuna tunamtegemea Mwekezaji na tunaogopa mkorofisha kwa kuwa hatuna nguvu za kusimama wenyewe wima na kujilinda.
This is the fate of opposition ambao bado wanaonyesha woga na udhaifu. Hata huko kujitolea mhanga si kule kwa kusema "kudadeki mpaka tone la mwisho" bali ni kule kwa kuogopa kuiudhi CCM na Serikali yake na kuhofia ubabe wa CCM kama vile walivyofanyiwa Mtikila na Lamwai.
Then you have a serious problem ya watu wasio na uwezo wa kujiamini bila kutegemea. Sasa kama kwa CCM wanahofia, kwa hao wengine Mafisadi, Wawekezaji na mawakala wa Mkoloni watafanyaje , huku CCM naye anawasumbua?
HIvyo tutafakari hayo yote sasa hivi si kwa nia ya kusema tusiendelee mbele na kuing'oa CCM, lakini tujue wazi huko tunakokwenda na tujiandai kikamilifu na si kubahatisha kwa kusema ngoja tufanikiwe kwanza.
Tena kama kauli za uhakika (self assured) zingetoka mapema na hata leo hii kujiuza kwa Upinzani kumpasha Mtanzania kuwa si suala la nia na sababu tu kuwa zipo, bali hata uwezo upo, umati mkubwa wa Watanzania usingeingia mashaka.
Tuna miezi mitatu ya kuuza ujumbe wa tumaini, utakaoonyesha kuwa hili si jaribio tena bali ni kujiamini na tuko tayari kwa lolote na hata kutoa kafara kuing'oa CCM.
Je Upinzani uko tayari kutumia turufu hiyo kwa Mtanzania atakayepiga kura?
Ni sumu tena kali Mutu lakini kwa JF haimwagiki kirahisi wataimba hadi wachoke wenyewe. Wanatuambia eti tusubiri kwanza tujifunze kutawala ndipo tuing'oe CCM, kwani CCM walijifunza kutawala wapi ndipo wakaingia.Kuna watu wanatisha humu duh ushauri wao ni kama sumu.
Watu wanaandika tu ila wahajuhi what is like to be in the battle field has kwenye inch yenye demokrasia changa kama bongo.
Watu hawa hatuna uhakika kama hata wata piga kura wakiwa ughaibuni....watu hawa ni hatari
Sasa ukitafakari kwa makini, hili la wapinzani na Chadema na mtazamo wa Watanzania wengi kuwa kwanza tuing'oe CCM, lakini inaelekea bado hatujajiandaa vya kutosha kuweza kuongoza tukishaiondoa CCM.
Si kwamba nadai CCM ibakie madarakani au isiondolewe, lakini kama Bibi Ntilie alivyobainisha kwenye barua ya Mnyika, yaelekea Chadema bado hawajajiandaa na hawajiamini kuwa wana uwezo wa kuongoza Taifa. Dua lao ni CCM ianguke, ndipo wao waanze kujifunza na kujipanga ni vipi waongoze Tanzania.
Ndiyo maana Mwanakijiji anauliza, then what?
Ikiwa mfupa wa TAMISEMI ambapo huko ndipo safu ya kwanza ya kuongoza nchi, Chadema walikukwepa wala hawakujituma kupata viti angalao nusu ya mkoa kama Dar, iweje leo tudhanie kuwa wataweza kuwa makini na uwezo wa kuongoza nchi kwenye Serikali Kuu na Bunge?
Makovu haya hayaweza kusawazishwa pamoja na hili la sasa la kuvizia mabaki ya CCM yaanguke ndipo yaingie Chadema na kuhakikisha walau Chadema wanaweza pata viti 70 vya ubunge.
Ni kutokana na hayo, ndio maana nakubaliana na Mwanakijiji kuhoji je tukishaing'oa CCM, then what? Maana inaelekea kama vile tulivyopata Uhuru au vile Kikwete alipata Urais, bado hatujajiandaa kuongoza na hatujiamini kuwa tuna uwezo wa kutawala.
Kila udhaifu wa CCM umetolewa majukwaani, lakini hapajawahi tolewa alternative solution ambayo ikakubalika hata ndani ya Chadema yenyewe, kila mara tunaambiwa "Subirini tuingie Ikulu". Je ina maana Chadema na Upinzani hauwezi kuanza kuleta maendeleo Tanzania mpaka viingie Ikulu?
Miaka mitano, bajeti ya nchi imekuwa ikiongezeka na matumizi ya hali ya juu. Ripoti ya mkaguzi mkuu CAG kwa miaka mitatu inaonyesha udhaifu wa Serikali kuu ambao umeimarisha ubadhirifu na rushwa. Lakini sijasikia hata siku moja hoja ya kutungwa Sheria au kusitisha Bajeti kutoka kwa Upinzani ili Serikali ijirudi na kurekebisha mfumo wake wa matumizi na hata kubana matumizi. Je wajibu huu ambao kawaida hufanywa na Chama cha Upinzani kama haukufanywa na Chadema na wenzao, bado mtasema tusubiri wakiingia madarakani?
Labda nihitimishe kwa kutoa mtazamo mwingine. TUfanye kwamba Upinzani umeshinda Uchaguzi Mkuu kwa asilimia 51% hiyo 49% ni ya CCM, pale Bungeni na hata Urais ni wa Upinzani. Inapokuja kwenya ufanyako kazi na utekelezaji hasa kwenye ngazi za Tawala za Mikoa (TAMISEMI), watendaji wengi wa kisiasa takriban asilimia 95% ni CCM ambao walishinda Udiwani na uchaguzi wa TAMISEMI 2009. Je Upinzani utawezaje kufanya kazi yake kwa ukamilifu bila mvurugano na hawa watu wa CCM ambao watakuwa wakisikiliza sauti za wale 49% walioko Bungeni?
Kila mtu anataka CCM iondoke, lakini hatuko tayari kukipa chama nafasi eti kikajifunze kazi kama Kikwete alivyofanya au kuwa ni Chama kisicho na wenye uwezo wa kutosha kuongoza na kufanya kazi kitendaji kama zile Tanzania ilivyopata Uhuru wake.
Baya zaidi, bado mpaka leo Chadema na Upinzani havieleweki Ki-Sera kwa Watanzania na hatujui watakuja na mipango gani ya Kisiasa na kimaendeleo kwa kueleweka kuliongoza Taifa la Tanzania.
Hivyo basi, inabidi tujiulize, je tuko tayari kuendelea kubahatisha kama Kikwete kwa miaka miwili ili kuelewa nini wajibu wa kuongoza nchi na kuwa na sera zinazoeleweka au ni lazima tujiamini na kuingia tukiwa tayari na Sera zetu zikieleweka kwa Wananchi ambao hawatahitaji miaka miwili kuzielewa na kuanza kuzifanyia kazi?
Ni sumu tena kali Mutu lakini kwa JF haimwagiki kirahisi wataimba hadi wachoke wenyewe. Wanatuambia eti tusubiri kwanza tujifunze kutawala ndipo tuing'oe CCM, kwani CCM walijifunza kutawala wapi ndipo wakaingia.
Hawajui machungu waliyonayo watanzania, wao wako ughaibuni watoto wao wanasoma kwa benefits hawajui hata kuwa watoto wetu ni jana tu walifukuzwa shule kwa kukosa mchango wa tuisheni wa shilingi mia tano, wao wakikosa kazi wanalipwa Jobseekers allowance.
Ndio hao hao wanatuambia tusubiri hadi machungu yawe makali ndipo tumtafute mganga, je kama ni ugonjwa wa kansa si utakuwa sugu hautibiki tena, uzuri tumewajua na lengo lao tumelijua hawatupi tabu.
Mkuu nimekusoma ndani ya mistari yako.Kama haya maswali waneulizwa kina Nyerere wakati wakipigania kumwondoa mkoloni ingekuwa kazi mubwa..
Hivi kweli wewe Mwanakijiji unafikiria watu wanataka kuiondoa CCM ili iwe nini?...mkuu wangu pengine sikusomi vizuri lakini mtu atataka kuondoa CCM madarakani asijue kwa nini ama kitafuata nini..sasa kwa nini wanagombea madaraka!..Bila shaka Chadema watachukua madaraka na kuhakikisha sera walizouza kwa wananchi na kukubaliwa zinafanya kazi..
Samahani lakini hivi unachotaka wewe ni madaraka yatagawanywa vipi au? maanake hata Ufisadi ni sehemu tu ya sababu za kuing'oa CCM madarakani ndani ya swala kubwa la Katiba yetu..miiko na maadili yapo ktk katiba na haya yote ni maswala yatakayopewa nafasi ktk bunge la kwanza hivyo kama wewe unalo tofali lako beba jiunge na kesho utaingia nalo bungeni kwa sababu tusifikirie kabisa kwamba Chadema wakichukua nchi basi nao watuburuze na sera ambazo wewe Mwanakijiji unazikubali..
Siku zote mhitaji ndiye husema anachokitaka na mbunge ni mwakilishi wa mawazo hayo,hivyo hata ngazi ya Kitaifa Chadema watafanya tu kile kinachohitajika na wananchi wakizingatia titikadi yao itawezesha vipi kupatikana kwake. Kila itikadi mkuu wangu ina mbinu ya kuleta kitu kile kile kinachohitajiwa Kitaifa..
LENGO ni moja isipokuwa kuna njia tofauti za kufikia lengo hilo.. Hata JK na CCM wanafikiria wanakwenda sawa kufikia maisha bora kwa kila mwananchi..Sii Chadema, CCM, NCCR TLP na wengine woote wanaamini adui yetu mkubwa ni Ujinga, Umaskini na maradhi isipokuwa tofauti zao zinakuja ktk mbinu na vipaumbele vya kutokomeza vitu hivi..
Kifupi CCM wanaamini kuvua wao kisha wape samaki maskini wasiojiweza na Chadema wanasema mfundishe maskini kuvua, kesho atakwenda mwenyewe kuvua samaki! Bado una shaka gani? mbona mimi niliwasoma mapema!
Kama wanaandika na wewe umepata kuyasoma waliyoandika,basi yatafakari kwa kina na chukua hatua sahii kutoka kwa kichwa yako.Kuna watu wanatisha humu duh ushauri wao ni kama sumu.
Watu wanaandika tu ila wahajuhi what is like to be in the battle field has kwenye inch yenye demokrasia changa kama bongo.
Watu hawa hatuna uhakika kama hata wata piga kura wakiwa ughaibuni....watu hawa ni hatari
Mkuu kusema ukweli katika hili sinabudi kuunga nawe kwamba kuitoa CCM tu halafu mengine mbele kwa mbele haina tija kwa taifa na si Chadema tu na hivyo vingine pia kwa kukaa na fikra mgando kuwa mipango ya uongozi na maendeleo havifanyiki mpaka wameingia jumba jeupe.Hiyo ni dhana ya kuikimbia kabisa.Nilifahamu juu ya mazungumzo ya baadhi ya uongozi wa juu wa CCJ na Chadema kwa muda kidogo; Yalitokana vile vile na ushauri wa watu mbalimbali kuwa CCJ iunganishe nguvu na Chadema. Hata hivyo hadi hivi sasa kilichofanyika ni baadhi tu yaviongozi wake kujiunga na Chadema na siyo CCJ nzima. Kuna sababu.
Wapo wanaosema kwa vile hawa ndugu zetu wameingia Chadema basi CCJ na wazo la CCJ nalo limekufa kwa hiyo sote tuliounga mkono CCJ tuinamishe vichwa vyetu kwa kushindwa na kujiunga na Chadema. Hizi ni fikra potofu. Ni potofu kwa sababu zinafikiria Chama kikifa au kikishindwa ina maana mawazo yake nayo yameshindwa. Yanafikiria kuwa kama watu wakitoka kujiunga na chama kingine au kutoka katika siasa maana yake siasa za chama hicho nazo zimeshindwa.
Ukweli unabakia kuwa ukweli kwamba siasa za kutaka ushirikiano wenye lengo la kuitoa tu CCM madarakani halafu ndiyo tujue tunataka kufanya nini ni siasa ambazo katika dhamira yangu siwezi kuziunga mkono. Siasa za kutosema nini unataka kufanya, kwa vipi na kwa muda gani ukionesha ukali kuhusu ufisadi miye siziwezi kwa sababu niaamini tatizo la Tanzania ni ufisadi kuliko kitu kingine chochote kile.
Kutuambia kuwa "panya hawakamatani" lakini hutuambii wewe utawakamata vipi na kwa namna gani, haitoshi vile vile.
Chadema ni tumaini kubwa sana kwa wengi wetu na kwa muda mrefu limekuwa kwangu ni tumaini vile vile. Lakini bado haijataka kuvuta mstari ule wa kiungozi kwa miaka kadhaa sasa. Siamini kama ndani ya siku chache zilizobakia wataweza kuvuka mstari huo. Na watakapogundua kuwa walipaswa kuuvuka watajikuta wanagalagazwa kwenye uchaguzi mkuu huku wakilalamika "CCM", "Tume ya uchaguzi", "Wizi wa kura", "Vyombo vya dola".
Ninawatakia kila la kheri wale wanaojiunga na Chadema wakiamini kitabeba matarajio yao. Hiyo ni demokrasia na kwa hakika kabisa nawatakia mafanikio.
Kwangu mimini bora nirudi na kutokuwa na chama nikiendelea kusimamia fikra na itikadi na mambo ninayoyaamini kuliko kupanda treni ambalo siju linakwenda wapi na kwa nini ati kwa sababu wengine wamepanda na wanashangilia!
Kundi zima la wabunge wa CCM wanaweza kutoka baada ya bunge kuvunjwa na kujiunga na Chadema na kutoka hao akapatikana mgombea wa Urais wa Chadema kama inavyotarajiwa. Hii inaweza kuwa habari kubwa sana na mtikisiko kwa jukwaa la siasa. Kwa wengine hilo laweza kutosha kabisa kufanya waamini kuwa saa ya mabadiliko imefika. Kwangu mimi bado nitaangalia kwa macho ya shuku hadi nijue wanataka kufanya nini. Wakisema wanataka tu KUINDOA CCM MADARAKANI au KUONGEZA IDADI WA WABUNGE, nitawaangalia halafu nitacheeeeeeeka!
Chadema kinaweza kabisa kuwa chama ambacho kitachukua uongozi wa nchi mwaka huu, endapo tu KITATAKA.
MM
Inavyoonekana hukumwelewa Nyerere au ulimwelewa ila unataka kupindisha kwa makusudi.Luteni
Nyerere alipouliza Watu wanakimbilia Ikulu kuna nini? Tulifurahia kauli hiyo kuwa lenga kina Kikwete, Lowassa na hata Malecela, Warioba na Msuya.
Sasa leo hii tukiuliza Lipumba n Chadema wanakimbilia nini Ikulu, tunaambiwa aah nyie roho korosho, mko majuu hamjui hali halisi!
Najua hali halisi zaidi yako, usifikiri kukaa nje basi ndio kuwa disconnected, kama niko disconnected as you think, nisingeling'amua la Richmond au Meremeta kuwa ni Uhujumu uchumi na kulipshikia bango!
Luteni
Nyerere alipouliza Watu wanakimbilia Ikulu kuna nini? Tulifurahia kauli hiyo kuwa lenga kina Kikwete, Lowassa na hata Malecela, Warioba na Msuya.
Sasa leo hii tukiuliza Lipumba n Chadema wanakimbilia nini Ikulu, tunaambiwa aah nyie roho korosho, mko majuu hamjui hali halisi!
Najua hali halisi zaidi yako, usifikiri kukaa nje basi ndio kuwa disconnected, kama niko disconnected as you think, nisingeling'amua la Richmond au Meremeta kuwa ni Uhujumu uchumi na kulipshikia bango!
Leo nina furaha kubwa sana na siwezi kuchangia kitu ktk mada hii. Na hakika hata Nyerere mwenyewe alipokuwa akiitangaza TANU walikutana na watu wenye kubeza chama kuwa hakikuwa tayari kuchukua uongozi kwa sababu hawakuona what next baada ya kumuondoa mkoloni.
Nachoweza kusema tu hapa ni kwamba Chadema hawawezi kuongoza kwa katiba yao isipokuwa kwa katiba ya nchi ambayo ndiyo mwongozo na dira ya Utawala. Kama dira hii ilipotoshwa kimazingara inarudishwa..
Ukifunga ndoa kuoa au kuolewa ni wazimu mtu akikuuliza what next kwani yeye alitaka iwe vipi?..
Nadhani itabidi niende ndani zaidi kuelezea kile ninachokiita "Tatizo la Chadema". Natumaini nitaeleweka, na siyotkuwa nimechelewa. Niwatoe hofu kabisa kwangu mimi hata CCM ikiondolewa kesho madarakani sitolia!! Lakini sitorukaruka kwa furaha! Nitauliza swali hili hili ninaloliuliza sasa.. "then what"? Nakataa kabisa kuwa hatuwezi kuwa na ajenda ya uchaguzi inayosema "tuiondoe CCM kwanza"! Hii ni ajenda ya kuondoa chama kimoja na kukiweka kingine. Yatakuwa yale yale ya KANU na RAINBOW coalition! Well RAINBOW walifanikiwa kabisa kuiondoa KANU, lakini is Kenya better today than during KANU's rule? Tutapata majibu tofauti sana kwenye hilo. Je Zambia chini ya Chiluba baada ya kuiangusha ZANU je walikuwa bora zaidi kwa sababu kina Chiluba walitimiza ndoto yao ya kumuangusha Kaunda?
Hili swali hata kama mtalikwepa, mtalibeza au mtajaribu kuonesha kuwa hamlielewi mtalazimika kulijibu tu one of these days. I know you will.
Kwa vile linaonekana ni gumu mno/halielewi au halijaulizwa sawasawa itabidi nilivunje vunje katika vipande vyake vidogovidogo. CHADEMA WAKILIELEWA NA KULIJIBU KABLA YA UCHAGUZI WATASHINDA KWA KISHINDO!
Na wewe tuwe pamoja, usiwatakie kila la kheri tafadhali unga mkono juhudi hizi, tulete mabadiliko.Kwa upande mwingine chadema nao wawe makini wasije wakawa kama NCCR mageuzi ya wakati ule ambapo ilisambaratika baada ya uchaguzi. all in all tunawatakia kila lakheri katika michakato yao angalau wapunguze vijembe na majivuno ya CCM ambayo yanatulaza njaa kila siku.