Ya Sajuki na funzo kwa wasanii wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ya Sajuki na funzo kwa wasanii wetu

Discussion in 'Entertainment' started by Paul S.S, May 11, 2012.

 1. P

  Paul S.S Verified User

  #1
  May 11, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Wadau kwa muda sasa kumekuwa kunaendeshwa kampeni kali ya kusaka michango kwaajili ya kukusanya fedha za kugharamikia matibabu nchini India ya Msanii wa filamu nchi SAJUKI ambaye kiukweli anaumwa kweli kweli..

  Tunashuhudia watu mbali mbali wakitoa mchango yao kwenye kampeni hii ya nguvu, lakini hapa kuna funzo kubwa kwa wasanii wetu. kuna watu wengi nchi hii wanaumwa hoi bin taabani wapo vitandani hawana hata pesa ya kununulia asprin wapo wanasubiri kudra za Mungu tu na hakuna hata mtu mmoja anayewaza kuwachangia zaidi ya ndugu zao wa karibu ambao nao wapo hio kiuchumi

  Kwanini SAJUKI au kwanini KANUMBA wapate michango mikubwa kiasi hicho?

  Je wanapokuwa kwenye peack pesa zao wanatumia vipi? Na hasa kwa jamii inayo wazunguka? Natamani basi kuanzia sasa niwe nawaona wasanii hawa wakipishana kwenye vituo vya watoto yatima kutoa misaada, kutembelea mahospitali kugawa vyadarua, kusimama kampeni za malaria, uzazi wa mpango,uzazi salama na mengineyo mengi kusaidia jamii kutokana na vipato vyao na umaarufu wao.

  Pamoja na kuendelea na maisha yao ya kifahari kwa kupanga majumba ya kifahari, kujirusha sana, kubadili magari na vimwana/mabuzi na tegemea sasa watakumbuka pia jamii hii wanayoipa kisogo pindi wanapokuwa juu ndio hii hurudi kuja kuiomba msaada pindi mambo yanapokuwa magumu.

  Mwisho namtakia mafanikio mema bwana SAJUKI afanikiwe kwenye mtihani huu mgumu
   
 2. M

  Mayu JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2012
  Joined: May 11, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Kuna haja kubwa ya wasanii wetu kuutumia umaarufu wao na pesa zao kufanya mambo ya kijamii sasa na sio wakipata pesa wao ni matanuzi tuu na ukiwashauri wakali kweli eti wametafuta pesa kwa jasho lao hivyo wasipangiwe wala kufuatwa fuatwa kwenye matumizi.
  Nadhani watapata fundisho sasa na tunataka kuona akina masanja wakiwarusha wanavyoshiriki mambo ya kijamii
   
 3. KALYOVATIPI

  KALYOVATIPI JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,419
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  pale wanapoweka kalikiti na zaazuu vichwani na kupa ma-lipshyn hata mtu ukimjua hataki salam ukikutananae klab matumizi kama msanii wa holywood wakiumwa wanatulayimisha kutoa michango kwenye vifilam vyao wanawataja mapredezye tu mbona awataji hata kituo cha watoto yatima mi sichangi kwanza babu yangu anaumwa zaid nami naitaji nichangiwe yan yakwao yetu sote matatizo yangu ni ya peke yangu hao marafiki zao ni watu wenye pesa si wangemuona papaa musofe, muzamil katunzi, ma akina chif kiumbe sio sisi wanatulazimish au hata wale wahindi wanaowadhulum hivi wana umoja wa kusaka haki zao au umoja wa kuwa makuwadi? Aiwezekani leo Ramsey noah aumwe matibabu mil 25 achangishe shame on you all artist from muv industr kazi yenu kubaka vitoto vidodo na vikijitetea mnajiangusha kwa aibu bahati mbaya mnapasua medula oblangata
   
 4. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2012
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,435
  Likes Received: 1,016
  Trophy Points: 280
  Mwacheni kwanza mchizi apone ndio mumchane na wakati mwingine hamjachangia hata cent. Its happen maradhi yanamkuta mtu yeyote na mengine need external muscle na mengine kimtindo watu wanamaliza. Wote mnajua resources za nchi ni kwa ajili ya viongozi na wasanii kipato chao bado akiendani na kazi wanazofanya kama mnaendelea kugonga copy na kuonyesha kazi zao bila kuwapa hata cent watatoka vipi.
   
 5. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #5
  May 11, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Lakini kweli...
   
 6. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Basi wajitahidi kuishi maisha ya kawaida wakikumbuka kuwa kuna matatizo makubwa yanaweza wapata.

  Kuwakumbusha ni muhimu, kwa kipato hichohicho kidogo wajifunze kuweka akiba na si kuiga maisha ya mastaa wa nje na kujitanua bila kujua kesho itakuwaje.

  Pole kwa Sajuki mungu atampa afya njema soon!
   
 7. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #7
  May 11, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,507
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  ni watu wangapi wapo Mhimbili hata madaktari tu kuwatibu imekuwa issue kisa hawana laki mbili za kufanyiwa operation lakini lilipokuja la SAJUKI 25Mil watu wakaweka hadi kipindi clouds na OK kuchangisha......hii inatoa picha gani kwa wagonjwa walio mahututi kitandani hawana hata panado? watanzania ubaguzi utaisha lini?
   
 8. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #8
  May 11, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 280
  NAdhani ulimaanisha "kulazimishwa" , sidhani kama umelazimishwa .... au alikuja mtu kukulazimisha?
   
 9. z

  zamlock JF-Expert Member

  #9
  May 11, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  ni kweli wanatakiwa kujifunza na ukizingatia hawa wasanii wengi wakipata pesa kazi yao kubwa nikutanua kwenye ma club kila mahali
   
 10. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #10
  May 11, 2012
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,716
  Likes Received: 3,125
  Trophy Points: 280
  Nilihoji nami hili lakini sikupata jibu. Vipi wale wasio wasanii waendelee kutaabika na pengine kufa! Nilisema tatizo hapa ni serikali yetu kuboresha huduma za afya kwani na haki ya kila mwananchi kujaliwa afya yake. Ukizingatia swala la Sajuki mpaka wabunge wamechangia mimi ndipo naposhangaa.
   
 11. M

  Mboerap Senior Member

  #11
  May 11, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 156
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kumchangia mgojwa mi naona sio ishu. Mi nashauri kwamba, kwakua kumbe kupitia vitu kama OK inaweza kuhamasisha kwa kiwango cha kufanikisha mamilioni kwa muda mfupi kiasi hicho, basi wangeanzisha kitu kama mfuko maalum hivi wa kuwasaidia sio wasanii tu bali mwana jamii yoyote mwenye tatizo kama hilo nae asaidiwe. Wanaokufa kwa kukosa pesa za matibabu wapo kibao tena hela ndogo tu ya kutibiwa hapahapa muhimbili
   
 12. D

  Don Calvino Senior Member

  #12
  May 11, 2012
  Joined: Mar 3, 2012
  Messages: 115
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  J.B acha pozi,tunakufahamu toka haujulikani mtaani,sasa umejulikana na vijisinema vyako unajifanya kama umetusahau watu wako tukikutana maeneo ya starehe,sisi ndio tutakaokuchangia na kukuzika.Na wasanii au watu maarufu wengine wenye tabia kama hizo.Siyo fresh
   
 13. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #13
  May 11, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hiyo phenomenon inaitwa Philanthropy na kwa bongo bado ipo chini sana
   
 14. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,059
  Likes Received: 6,506
  Trophy Points: 280
  Mnapenda kulaumu pasi kuangalia kwanini hali imekuwa hivi,
  sajuki alipata ajali mchumba/mke akapoteza mguu - je ulimchangia
  sajuki kapata matibabu ya awali pesa imekwisha sijui hata kama umemchangia,
  kanumba alichangia ili afanye nini, mbona hajarudi kama vipi si mngeacha kuchanga.

  Namkubali Zitto Zuberi Kabwe aliyesema wasanii waangalie namna ya kuchangia mfuko
  wa bima ya afya ili walau waweze kupata matibabu kwa urahisi.
   
 15. P

  Paul S.S Verified User

  #15
  May 18, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu Mamndenyi hakuna mtu analaumu hapa, linatolewa angalizo tu hapa
  BTW hivi nchi hii unajua ni watu wangapi wamekatika miguu na ikaoza wakafa kwa kukosa pesa za matibabu?
  wangapi wako hoi kama Sajuki na hawana hata pesa ya panadol wanasubiri kudra za Mola?
  Ujumbe hapa ni kuwa wao wanabahati jamii inawajali kwa kuwachangia hivyo walitambue hilo walau kwa kurudisha fadhila wakiwa nazo kwa kushiriki shughuliza za kusaidia jamii kwa namna moja au nyingine
  Napia kujiwekea akiba au bima za afya
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #16
  May 18, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  I adore people who get everything and leave a humble and displined life. Mambo ya kutaka kukomesha watu mjini hapa ndo tunaishia kujikomoa wenyewe
   
 17. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #17
  May 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,059
  Likes Received: 6,506
  Trophy Points: 280
  Hivi anaendeleaje huyu dogo Sajuki.
   
 18. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #18
  May 21, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  naipenda avatar yako! mama wa YESU, UTUOMBEE! AMINA!
   
 19. P

  Paul S.S Verified User

  #19
  May 21, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mara ya mwisho alionyeshwa yupo airport kuelekea india kwa matibabu
   
 20. gango2

  gango2 JF-Expert Member

  #20
  May 22, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 1,223
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Habari zenu wana JF,

  Ni takribani wiki 2 sasa tangu heka heka za kuomba misaada zilipopamba moto ili kumchangia msanii Sajuki kwenda kupata matibabu india, na ilikuwa inatakiwa takribani tsh 25 mil (samahani kama nitakuwa nimekosea) ili kufanikisha matibabu hayo. kweli mungu mkubwa wadau mbali mbali walifanikisha hilo na leo hii ndugu yetu sajuki yupo India kwa matibabu

  fundisho/lililogundulika
  kweli imetushangaza wengi kuona wasanii wa Tanzania pamoja na kuwa na umoja wenye mbwembwe nyingi (bongo movie au TIFF) wameshindwa kulipia gharama za msanii sajuki mpaka imefika wakati wanaomba msaada kwa wanasiasa au watu wengine???, sitaki kuamini hilo kabisa na inatusikitisha sana. Kila kukicha watu hawa wanafanya mapart mengi mara birthday ya nani, mara sherehe kutimiza mwaka mmoja, mara uzinduzi wa filamu na nyinginezo nyiingi zinazogharimu mamilioni ya pesa. Katika hayo hayo masherehe ndo wanafanya mshindano ya nani katoka na mavazi ya gharama au kaja na gari zuri. Leo mmoja wenu anahitaji matibabu ya tsh 25 mil, mmeshindwa kumsaidia mpaka mnakimbilia kuomba msaada kwa wadau wengina na wanasiasa??

  kweli wasanii wa Tanzania acheni anasa zisizo na maana ambazo haziwasaidii kabisa ni wakati wa kuamka sasa, sijui huo umoja wenu (BONGO MOVIE) unamaana gani kwa sasa, au kuwakusanya kwenye sherehe za birthday na tafrija mbalimbali tuu??. badilikeni sn mmetia aibu katika hili? katika msiba wa kanumba mmeshona MASUTI MAKUUBWAA TENA YA GHARAMA SAAANA ili muonekane mnapendeza na mnaumoja saaana, kitu gani kimewafanya mshindwe kuziuza zile suti mpate hela za kumtibia SAJUKI??

  Wakati ndo huu, badilikeni sasa!!!
   
Loading...