Kilio cha maproducers kwa wasanii

Feb 6, 2024
40
50
Producers wengi Tanzania tumekuwa tukitumiwa na baadhi ya wasanii kama daraja la mafanikio yao na kisha kutupaka matope au kuuambia umma kuwa sisi ndio tumewakosea sana na tunawanyonya. Laiti kama wasanii hao wangekuwa wanaeleza angalau mazuri wanayofanyiwa na producers. Kwa bahati mbaya sifa wanazotumwagia tunapokuwa studio tunafanya kazi huishia studio na umma husikia tu wimbo mzuri ukiwa umetoka. Sifa zetu tunazopewa zimekuwa ‘perishable’ ingawa kazi tunayofanya huishi miaka yote na hutumiwa na msanii husika.

Kwa mazoea ya soko la Tanzania, producers wengi huwa na moyo wa mshumaa na hata kuwatengenezea wasanii wetu midundo au nyimbo bure. Lakini wapo pia ambao huwalipisha wasanii kiasi cha fedha ambacho kwa uhalisia wa kazi na matunda ya kazi hii sio halali/sio fair bali ni bei zilizozoeleka tu.

Kwa uhalali wa ‘intellectual works’ wahusika wakuu huvuna matunda pamoja kwa kugawana asilimia kila wakati ambapo kazi hiyo itakapokuwa ikiingiza pesa. Lakini kwa Tanzania ni kama producer humuuzia haki miliki ya kazi nzima msanii kwa shilingi kadhaa au hata bure na kisha msanii kuingiza mamilioni kwa miaka mingi kwa kuuza au ku-perform kazi ile.

Hata kama ni kweli tasnia ya sanaa ya muziki kwa Tanzania bado inawanyonya wadau kwa ujumla, kati ya hao wanaonyonywa tumkumbuke producer ambaye yeye ananyonywa hadi damu ya mwisho na kisha kuchafuliwa pale anaponyoosha mikono yote kutaka mambo yaende sawa.
Hebu fikiria, kama kweli mgao wa matunda ya kazi yangekuwa sawa kwa asilimia kadhaa kwa kila kazi ambayo producer amefanya, producer kama P-Funk Majani angekuwa na maendeleo kiasi gani kutoka kwenye muziki pekee? Sisemi moja kwa moja kama aliofanya nao kazi walimnyonya, inawezekana alinyonywa na mfumo ulivyo.

Lakini ni wasanii wangapi tumeshawasikia wakitaja mafanikio makubwa waliyoyapata kwenye muziki kwa hits chache au hata hit moja tu. Je, umeshajiuliza producer wake alipata nini? Je, ni producers wangapi ambao wametengeneza hits kibao zilizowapeleka wasanii mbali sana lakini wao wamebaki na hali ngumu kimaisha huku wakiendelea kunyonga midundo na kuambulia sifa za studio?
Nyimbo tunazotengeneza nyingi studio tukisubiri msimu wa ‘mvua’ tuupush zinapobaki huwa hasara kwa producer kwani wao wanaweza kwenda kwa mwingine na wakazirudia.

Je, producer anapata faida gani kwa kazi aliyoifanya tayari? Imefika wakati ambapo producer inabidi aheshimiwe kwa sababu bila yeye kusingekuwa na wasanii wengi wanaotamba hivi sasa. Hii itaongeza nguvu pia ya kazi kwa producers wapya nchini.

Producer alipwe vizuri kwa sababu anapolipwa vizuri na yeye ubunifu na utendaji wake wa kazi unakua kwa kiwango kikubwa. Pia atapata uwezo wa kununua vitendea kazi bora zaidi vitakavyomsaidia kuingiza muziki wetu kwenye ushindani wa soko la muziki Afrika na duniani kwa ujumla.

Naamini ipo siku hata haki za producer katika muziki alioutengeneza Tanzania zitazingatiwa ikiwa ni pamoja na kuvuna asilimia fulani ya muziki wake pale unapotumika kwenye miito ya simu, na biashara nyingine.

images.jpeg

View: https://www.facebook.com/100064569174258/posts/pfbid0rf5Fntw1K9A3YzMxJJyP1SQQoka48hn7oVsRoLnQ2GNJtrXovqjN57vcQFMuQGv4l/?app=fbl
 
Kwanini na nyinyi msiwe na viburi muone kama hizo nyimbo wanazotamba nazo mtaani watatamba.

Fanyeni kamgomo ka hata mwezi hivi.
Tatizo maproducer wote wanaoliendesha game la bongo wanalipwa vizuri.
Shida inaanzia kwenu nyinyi maprodyuza njaa njaa a.k.a njaa kali.

Jitafuteni bhandugu angalau mfikie levo ya s2kizzy,abbah,mocco genius,gachi b na baadhi ya wengineo waliojipata.


NB:KUTOBOA SIO MAKALIO KWAMBA KILA MTU ANAYO.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom