Ujio wa wasanii mbalimbali kutoka nje ya bongo, kuna impact yoyote imepatikana kwa wasanii wetu?

Feb 6, 2024
40
50
Leo nilikuwa napenda tulizungumzie hili wadau ujio wa wasanii kutoka mataifa ya nje kuja hapa Bongo kufanya show je? Kuna impact ama faida yoyote imepatikana kwa Taifa letu nje? Ya ongezeko la mapato siku ya show hapa nazungumzia wasanii wetu je? Wamenufaika Ama hapana..

Maana kuna wimbi kubwa la wasanii kutoka nje wamefanikiwa kimuziki Tofauti na wasanii wetu wa Hapo Bongo.

Je? Ina maanisha wasanii wetu hawataki kujifunza mazuri kutoka kwao Ama hili limekaaje?

Thamani ya wasanii kutoka nje? Pale wanapokuja Bongo kufanya show wamekuwa wanapewa Heshima na Thamani Kubwa kuliko wazawa kuanzia malipo nk.

Lakini kwenye upande wa Vibe kwenye stage huwa sioni utofauti.

Lakini pia kitu kingine waandaji wa matamasha mara zote wamekuwa wakicopy na kupaste kile kile kila mwaka . Sijui bajeti / ya uaandaji wa show inakuwa mbovu sijui kikwazo nini hapa.

Ukiangalia matasha ya nje na hapa Bongo kuna utafauti mkubwa sana kuanzia uaandaji , promotion na wasanii wenyewe wakiwa jukwaani kuparform.

Je? Wasanii hawataki kubadilika on stage

je? Kwanini waandaji wa stage/ jukwaaa linakuwa halina mvuto

Je? Wasanii wa hapa Tanzania huwa nao wanapewa respect ama Heshima wakiwa nje ya MIPAKA ya Tanzania kwenye show walizoitwa kama tunavyowapa Heshima wasanii kutoka nje wanakuja hapa Bongo.

Ni jukumu letu zote kupenda na kuthamini kazi za mikono ya wasanii wetu.

Am out ..
images (1).jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom