Zitto na Shibuda ndo pekee wenye akili chadema hawawezi kuunga mkono upuuzi
Wewe si CCM wala CHADEMA wala chama chochote. Kama ni CCM, basi uliletewa kadi nyumbani na baba yako aliyeko Statehouse. CCM walisotea kadi zao kwa kujaza fomu, kisha maombi yao kufikiriwa, wana jua kuwa kilichofanywa Arusha ni serikali dhidi ya raia, kimewaadhiri watu wote bila kujali itikadi zao.
Ipo siku, miti itateleza, nguo zitawashuka na mama mkwe mtakutana naye....
Wakeup AFRICA, wakeup Tanzania, ..... wake up CHADEMA, wake up CCM, wakeup TLP, etc, nchi hii ni yetu wote.
Polisi ni watoto wetu, wamezaliwa kwenye familia za vyama mbalimbali... hali kadhalika wanajeshi. Sioni sababu hata moja kwa polisi kutenda aibu hii.
Miaka isiyozidi 3, jijini Paris, waandamanaji waliandamana kupinga ubaguzi wa rangi kwa siku zaidi ya 5, wakichoma hata magari, lakini hakuna hata mmoja aliyepigwa na kuuawa na polisi.
Tena, waandamanaji hao hawakuwa wazaliwa wa Ufaransa, bali waafrika wenzetu weusi. Je, iweje wa Tanzania wenzetu tuwaue? Iweje majambazi wanapotuvamia polisi hawaji? Je, upi ni upuuzi hapa?